Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA): Hakuna utoroshwaji wa wanyama pori kwenda Falme za Kiarabu

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
15,167
16,254
DAR ES SALAAM: Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) imesema hakuna utoroshwaji wa wanyama pori kwenda Falme za Kiarabu kama taarifa za upotoshwaji zinavyodai.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari leo kuwa kama Mamlaka inayohusika na kutoa vibali kwa ndege za mizigo na abiria zinazoingia katika anga la Tanzania kuwa hakuna ndege ya mizigo iliyoingia nchini kwa kazi hiyo.“

Taarifa za utoroshaji wanyama pori kupitia ndege kubwa ya mizgo kutoka Loliondo kwenda nchi ya Falme za Kiarabu (UAE) hazina ukweli wowote,” imesema taarifa hiyo. “Ndege ya mizigo ya Falme za Kiarabu ilifanya safari yake ya mwisho Julai 19, 2023 kinyume na taarifa kuwa kulikuwa na ndege hiyo Agosti 26, 2023.”

Hamza amesema Mamlaka ina mfumo wa kufuatilia ndege kwa wakati halisi na ndege zote za kimataifa huingia na kutoka kupitia viwanja vilivyoidhinishwa kuruhusu ndege kutoka nje ya nchi kutua na kuondoka kwenda nje ya nchi.

Viwanja vinavyohusika ni pamoja na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Kia, Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume (AAKIA) na vingine vilivyoidhinishwa.Imeandaliwa na Mwandishi Wetu

Habarileo
 
Kwani cargo ikiwa na logo ya diplomatic haikaguliwi. Hata njia hyo inaweza kutumika kufanya smuggling
 
IMG_7921.jpg
 
Back
Top Bottom