Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) yasema haikitambui chuo cha Tanzania Aviation College kilichotoa wahitimu tangu 2018

crankshaft

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,410
3,376
Dar es Salaam. Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema haiutambui usajili wa Chuo cha Tanzania Aviation College kilicho na matawi katika mikoa ya Mwanza, Dares Salaam na Arusha.

Chuo hicho ambacho kimekuwa kikitumia usajili namba wa CAA/AT0/050 imebainishwa kuwa usajili wake ulifikia ukomo mwaka 2018.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari inaeleza kuwa kukoma kwa usajili huo kunafanya mafunzo ya usafiri wa anga yanayoendeshwa na chuo hicho kwa kutumia mgongo wa kutambulika na TCAA kuwa ni kinyume na sheria.

“Pia hii inafanya wahitimu wa chuo hiki kukosa sifa za kupata leseni kutoka TCAA hivyo kushindwa kupata ajira,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kufuatia hilo, imeelezwa kuwa kinachofanyika sasa ni kinyume na taratibu za usajili kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Usafiri wa Anga, Sura ya 80 na Kanuni zake, The Civil Aviation (Approved Training Organisation) Regulations, 2017.

“TCAA inatoa wito kwa wazazi na wanafunzi wanaotaka kusoma kozi za Usafiri wa Anga kujiridhisha kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ili kupata uhakika kuhusu uhalali wa vyuo vinavyotambulika, pia orodha yake inapatikana katika tovuti ya Mamlaka,” imeelezwa.

Mwananchi
 
Mbona ni suala la kuketi chini kama taasisi na kusolve iyo issue vijana waendelee kuchota maarifa? Hii Kasumba ya ili uonekane unafanya kazi au wewe ni bossi ni ama umtishie au uharibu image ya upande wa pili au umridishe nyuma. Tabia za NEMC
 
Kwanini kisifungwe? Huu ni uhuni na wizi lakini pia mnaua ndoto na maisha ya vijana uku mkiua chumi za familia. Wa kuchuliwa hatua ni TCAA.
 
Mbona ni suala la kuketi chini kama taasisi na kusolve iyo issue vijana waendelee kuchota maarifa? Hii Kasumba ya ili uonekane unafanya kazi au wewe ni bossi ni ama umtishie au uharibu image ya upande wa pili au umridishe nyuma. Tabia za NEMC
Naunga mkono hoja..hawa jamaa badala ta kuonesha jitohada walizofanya ili kuhakikisha chuo kinaenda..wao wanafikiri watapata sifa kwa kutengua utambuzi wa chuo.

Haya ndo Mwigulu kaongea jana tu...kwa niaba ya mama, kubomoa ni rahisi sana kuliko kujenga.

Unakuta mtu anakaa tu ofisini na hajawahi hata kufungua genge anaona mambo ni rahisi
 
Kwani swala la bandari limeisha ili tuendelee kujadiri ya chuo kilichopo ndani ya nchi kinatoa mafunzo miaka5 bila wahusika kutambua kwamba hawana haki yakutoa mafunzo hayo na bado wapo ofisini wanadunda,,
 
Na wao walikua wapi kufunga hicho chuo tangu kipindi hicho leseni yake ilipo malizika hadi waka acha watu wapoteze muda na fedha 🤔🤔 huu ni upumbavu usio mithirika, wao kama watoa leseni walipaswa kufanya jambo mapema na sio kuja kutangaza Leo wakati wanafunzi wame endelea kuhitimu tangu 2018, na wao pia Wana makosa katika hili
 
Huo ndio utanzania, mamlaka inakuangalia unaanza kuchimba msingi mpaka unamaliza kujenga jengo la gorofa 8, miaka karibu 4, mwisho wa siku unakuta alama ya bomoa. Ukiuliza kuliokoni unaambiwa umejenga eneo lisiloruhusiwa...
 
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema haiutambui usajili wa Chuo cha Tanzania Aviation College kilicho na matawi Mikoani, Mwanza, Dar es Salaam na Arusha, kinachotoa mafunzo ya usafiri wa anga

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema leseni ya usajili wa chuo hicho uliisha 2018 hivyo mafunzo ya usafiri wa anga yanayoendeshwa na chuo hicho ni kinyume na sheria, na hivyo wahitimu wanakosa sifa za kupata leseni kutoka TCAA hivyo kushindwa kupata ajira

Amesema, “TCAA inatoa wito kwa Wazazi na wanafunzi wanaotaka kusoma kozi za Usafiri wa Anga kujiridhisha kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ili kupata uhakika kuhusu uhalali wa vyuo vinavyotambulika, ambayo
orodha yake inapatikana katika tovuti ya Mamlaka,”

Chanzo: Mwananchi
 
Halafu bado hamtaki wawekezaji,
Watanzania hatuwezi kujiendesha wenyewe hilo liko wazi, ni ujanja ujanja na roho mbaya ndio tunaweza.
 
Hii nchi hii,

Sasa wao kama viongozi wa taasisi inayosimamia hayo mambo walikuwa wapi miaka yote hiyo leo ndio wanagundua?

Hata wao watakuwa wameshiriki au kuna asilimia fulani wanapata mana huwezi kuona kitu kinaenda kinyume na mamlaka ya kurekebisha na wajibu unao halafu uache tu.
 
Back
Top Bottom