Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,713
- 13,464
Prof. Kitila Alexander Mkumbo ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, ambaye kateuliwa na Rais Magufuli hivi karibuni, leo anatembelea Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dar es Salaam Water and Sewage Corporation-DAWASCO).
Bila shaka hii ni ziara yake ya kwanza DAWASCO. Naamini atakuja na mbinu za kutatua upungufu wa Maji katika Jiji la Dar Es Salaam na Maeneo ya Jirani.
Nitawaletea Updates ya kile kitakachojiri kutoka hapa DAWASCO Makao makuu, karibu kabisa na lilipojengo la Water Front. Karibuni.
Prof. Kitila Mkumbo akikagua Idara zilizopo DAWASCO=======
UPDATES;
Uwasilishaji wa DAWASCO:
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo
Kazi za DAWASCO;
1. Tunazalisha maji na kusambaza maji Dar na Bagamoyo na kuunganisha wateja.
2. Tunatengeneza miundombinu na kukusanya bili.
3. Tunadhibiti ubora wa maji.
DAWASCO ina watumishi 1083.
Vyanzo vya maji ni mto Ruvu, mto Kizinga na visima. Ruvu chini inazalisha maji lita 271000 Ruvu juu lita 196000, Mtoni lita 6500 na Visima ni lita 6000.
Shirika limegawanyika mikoa katika 10 ambayo ni Ilala, Kinondoni, Kawe, Tegeta, Magomeni, Kimara, Tabata, Temeke, Bagamoyo, Kibaha na Pwani. Tunahudumia wateja 187087 lengo ni 400000 kufika Juni 2017.
DAWASCO imeunganisha jumla ya vizimba 560 kwa ajili ya watu wasio na uwezo. Katika kukusanya maduhuli, DAWASCO imefanikiwa kutoa elimu ya kutosha. Mwitikio ni mkubwa tumeuza maji bilioni 46.1 ukilinganisha na bilioni 77 kwa mwaka 2015/16.
Changamoto tunazopata ni
1. Maji kupotea
2. Wizi wa maji
3. Miundo mbinu na mita mbovu.
Yamepotea maji 37.96%
MAKUSANYO YA MADUHULI
2014/15 tumekusanya 43.8bil, malalamiko yamepungua yamebaki malalamiko ya bili kubwa. Pesa hii ya maduhuli tunagawana na DAWASA.
Tuna kampeni ya ''Mama Tua Ndoo'' ndani ya siku 90. Malengo ni watu 151,000 wataunganishiwa maji hata kwa mkopo wa miezi 12. Wote wanaopitiwa na bomba la mchina watapata maji, Tabata Segerea Kisukuru, Kimara wote watapata maji.
Tumenunua pikipiki 100 na bajaji 50 na kuajiri vijana 100 kukamilisha hili zoezi.Tuna malengo kuongeza wateja hadi 151,000 na mauzo 7,500,000 m3 kwa mwezi na hivyo kupunguza upotevu wa maji.
MWELEKEO:
Kumtua mama wa kitanzania ndoo kichwani, upanuzi wa mtandao wa maji jumla ya km 1427 zinapanuliwa kuanzia Tegeta Mpiji hadi Bagamoyo kuanzia July 2017, Bilioni 117 zimeshapatikana toka Benki ya Dunia. Wateja 100,000 wataunganishiwa maji baada ya huu upanuzi.
Kupunguza maji yaliyopotea: Kubadilisha mita, kupunguza mgandamizo na maji kuziba mivujo, kutengeneza mita, kukarabati mtandao chakavu. Mivujo ndio inapitisha maji machafu na kutoa masafi. Yote itazibwa.
MIPANGO YA MUDA MREFU: Tutatumia SCADA SCIENTIFIC ACQUISITION OF DATA Technologia hii itasaidia kuyaangalia maji kwa kutumia remote control.
Yellow - ruvu chini
Blue - Ruvu juu
Green - visima
Red - malalamiko
Mtandao wa maji taka umezidiwa, Ulijengwa mwaka 1950 hadi 1970 Mtandao huu una jumla ya km 190 tunatumia mfumo wa asili Mabwawa. Tuna mabwawa 9 Mabibo, Kurasini, Lugalo, Airwing, Buguruni, Vigunguti na Ukonga. Mengine hayafanyi kazi .
Mpango wa kuboresha majitaka tumeanza kukarabatibkwa kutumia fedha za ndani. Vigunguti ilikufa sasa tunaifufua upya.
MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJITAKA DAWASA WANASEMA:
Tunahudumia kutoka Ruvu hadi Temeke. Dar es Salaam water and sewerage authority(DAWASA) iliundwa 4.4.1997, DAWASCO iliundwa 2005.
DAWASCO iliundwa baada ya kuvunjwa kwa mkataba wa City Water Service baada ya kushindwa masharti ya mkataba.
MAJUKUMU YA DAWASA
1. Kusimamia utoaji wa huduma ya maji safi na maji taka
2. Kukusanya maduhuli.
Bei ya maji imegawanyika katika makundi matatu DAWASCO, DAWASA ni 496 DAWASA 1106. Ni bei kwa m3 yaani DAWASA tsh 496 m3.
Kimbiji kuna visima 20, Mpera yatagawa maji kwa maeneo ya Banana haya ni maji ya visima. Mradi wa Ruvu chini umekamilika, Bomba la Ruvu chini tulipata fedha kutoka Marekani, bomba linafanya kazi lakini bado tuna deni tumemaliza upanuzi na mtambo na ulazaji wa bomba na kujenga tenki.
Sasa hivi kuna viwanda hivyo changamoto ni umeme. Ila tumeanza kufanyia kazi tatizo la umeme bomba mtamboni mpaka Kibamba. Na lingine kutoka Kibamba mpaka Kimara. Yote yamekamilika, maeneo yatakayo hudumiwa ni kati ya Mlandizi na Kimara hadi Vgunguti na Uwanja wa ndege.
Maji yapo tatizo ni mfumo wa usambazaji. Kimbiji tunachimba visima 20 na tutafuata na vingine 30. Bwawa la Kidunda unakabiliwa ukame wakati wa kiangazi. Ujenzi wake ni muhimu ili tuwe na uhakika wa kupata maji kipindi chote.
Jiji zima tunataka liwe na mabomba. Tayari hili linasubiri fedha tu tukamilishe. City centre Korea watatoa fedha za kusambaza mabomba hadi Magomeni. Tuna mpango wa kuweka majitaka kati ya Bagamoyo na Kibaha, changamoto ni ukame na uvamizi wa vyanzo.
Katibu wa chama cha wafanyakazi Mzee Jongo anasema ili Wizara itulie ni lazima DAWASCO na DAWASA ifanye kazi vizuri.
Prof. Kitila Mkumbo anaongea...
Sikujua kama kutakuwa na waandishi wa habari. Nichukue nafasi hii kushukuru sana DAWASCO na DAWASA kwa jinsi mlivyojiandaa... nawashukuru kwa kazi kubwa ambazo mnazifanya.
Mimi nilikuwa naifuatilia DAWASCO na baada ya kupewa hii nafasi na Rais, nimesoma zaidi nakiri bado kuna changamoto kubwa za upatikanaji wa maji Dar es Salaam katika siku za karibuni. Kazi kubwa imefanyika kuhakikisha watu wanapata maji Dar es Salaaam inahitaji Lita milioni 510 kwa siku. DAWASCO ndio inaongoza kwa makusanyo nchi nzima.
Hapa kuna suala la uzalishaji na usambazaji, mmefanya kazi zaidi kwenye uzalishaji kuliko usambazaji. Wananchi wanachokihitaji ni usambazaji. Wananchi watatupima kwa usambazaji sio uzalishaji. Ugomvi wangu utakuwa mkubwa na mhandisi ili tuwekeze kwenye usambazaji.
Kwa upande wa serikali tutaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya maji tunaenda kusimamia usimamizi mzuri wa miradi hii kwani imekuwa haiishi kwa muda uliopangwa, tunahitaji tukimbie sio tutembee katika miaka 50 ya uhuru jiji la Dar es Salaam kuwa na uhaba wa maji ni aibu.
Bado kuna ubaguzi, kuna maeneo yanapata maji na mengine hayapati. Yale maeneo korofi changanyikeni, Bonyokwa nk yamekuwa covered. Tunataka maeneo korofi yote wapate maji lugha yetu sasa ni matokeo. Tutafanya michakato lakini wanachi wanataka matokeo. Maji yapo au hayapo yanaonekana.
Kazi ambayo Rais ametupa ni kuhakikisha tunapata matokeo wananchi wa kawaida wanaopata maji wanalipa. Wananchi masikini wanalipa, iwenye taasisi hazilipi? Rais alisema watu wakatiwe umeme, sio umeme tu bali ni huduma zote mbinu ili tupate maji tunahitaji fedha.
Kwenye kulipa tusibague. Taasisi zote zilipe bili ili muweze kufanya haya mnayoyafanya maji mengi sana yanapotea. Ni aibu toeni elimu ya umma watumiaji wengi wanapoteza maji, hata zile kazi wanazoweza kufanya mfano maji yanavuja wanasema ni kazi ya DAWASCO.
Tuwaelimishe wananchi suala maji ni suala la Serikali na wananchi pia tuweke malengo kwamba tatizo la maji Dar es Salaam liishe na life kabla ya 2020, kuna uwezekano wa kumaliza tatizo la maji Dar es Salaam.
Tunataka tuwe na REA ya maji tupeleke maji vijijini. Nawaahidi kwamba nitawapa support yangu kwa kile chochote mnachotaka kwa Katibu Mkuu, ofisi yangu ipo wazi muda wote. Huwezi kukomesha umasikini vijijini wakati wakina mama bado wanahangaika na maji umbali mrefu.
Inabidi tujiwekee mipango ya kulitatua hili tatizo kwa sababu uwekezaji ambao unafanyika ni mkubwa. Hili tunaliweza kazi kubwa tuliyonayo ni kubadilisha mtazamo. Tutoke kwenye makaratasi lengo liwe ni kupata maji ili la maji taka linataka uwekezaji. Lakini tuanze na maji safi na salama kwanza.
Bila shaka hii ni ziara yake ya kwanza DAWASCO. Naamini atakuja na mbinu za kutatua upungufu wa Maji katika Jiji la Dar Es Salaam na Maeneo ya Jirani.
Nitawaletea Updates ya kile kitakachojiri kutoka hapa DAWASCO Makao makuu, karibu kabisa na lilipojengo la Water Front. Karibuni.
Prof. Kitila Mkumbo akikagua Idara zilizopo DAWASCO
UPDATES;
Uwasilishaji wa DAWASCO:
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo
1. Tunazalisha maji na kusambaza maji Dar na Bagamoyo na kuunganisha wateja.
2. Tunatengeneza miundombinu na kukusanya bili.
3. Tunadhibiti ubora wa maji.
DAWASCO ina watumishi 1083.
Vyanzo vya maji ni mto Ruvu, mto Kizinga na visima. Ruvu chini inazalisha maji lita 271000 Ruvu juu lita 196000, Mtoni lita 6500 na Visima ni lita 6000.
Shirika limegawanyika mikoa katika 10 ambayo ni Ilala, Kinondoni, Kawe, Tegeta, Magomeni, Kimara, Tabata, Temeke, Bagamoyo, Kibaha na Pwani. Tunahudumia wateja 187087 lengo ni 400000 kufika Juni 2017.
DAWASCO imeunganisha jumla ya vizimba 560 kwa ajili ya watu wasio na uwezo. Katika kukusanya maduhuli, DAWASCO imefanikiwa kutoa elimu ya kutosha. Mwitikio ni mkubwa tumeuza maji bilioni 46.1 ukilinganisha na bilioni 77 kwa mwaka 2015/16.
Changamoto tunazopata ni
1. Maji kupotea
2. Wizi wa maji
3. Miundo mbinu na mita mbovu.
Yamepotea maji 37.96%
MAKUSANYO YA MADUHULI
2014/15 tumekusanya 43.8bil, malalamiko yamepungua yamebaki malalamiko ya bili kubwa. Pesa hii ya maduhuli tunagawana na DAWASA.
Tuna kampeni ya ''Mama Tua Ndoo'' ndani ya siku 90. Malengo ni watu 151,000 wataunganishiwa maji hata kwa mkopo wa miezi 12. Wote wanaopitiwa na bomba la mchina watapata maji, Tabata Segerea Kisukuru, Kimara wote watapata maji.
Tumenunua pikipiki 100 na bajaji 50 na kuajiri vijana 100 kukamilisha hili zoezi.Tuna malengo kuongeza wateja hadi 151,000 na mauzo 7,500,000 m3 kwa mwezi na hivyo kupunguza upotevu wa maji.
MWELEKEO:
Kumtua mama wa kitanzania ndoo kichwani, upanuzi wa mtandao wa maji jumla ya km 1427 zinapanuliwa kuanzia Tegeta Mpiji hadi Bagamoyo kuanzia July 2017, Bilioni 117 zimeshapatikana toka Benki ya Dunia. Wateja 100,000 wataunganishiwa maji baada ya huu upanuzi.
Kupunguza maji yaliyopotea: Kubadilisha mita, kupunguza mgandamizo na maji kuziba mivujo, kutengeneza mita, kukarabati mtandao chakavu. Mivujo ndio inapitisha maji machafu na kutoa masafi. Yote itazibwa.
MIPANGO YA MUDA MREFU: Tutatumia SCADA SCIENTIFIC ACQUISITION OF DATA Technologia hii itasaidia kuyaangalia maji kwa kutumia remote control.
Yellow - ruvu chini
Blue - Ruvu juu
Green - visima
Red - malalamiko
Mtandao wa maji taka umezidiwa, Ulijengwa mwaka 1950 hadi 1970 Mtandao huu una jumla ya km 190 tunatumia mfumo wa asili Mabwawa. Tuna mabwawa 9 Mabibo, Kurasini, Lugalo, Airwing, Buguruni, Vigunguti na Ukonga. Mengine hayafanyi kazi .
Mpango wa kuboresha majitaka tumeanza kukarabatibkwa kutumia fedha za ndani. Vigunguti ilikufa sasa tunaifufua upya.
Water is human right.
Temina Kasih kamaliza.MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJITAKA DAWASA WANASEMA: