Mamilioni ya Lowassa yaingia CHADEMA

Mamilioni ya Lowassa yaingia CHADEMA

Hatujadili upuuzi kama huu kwa sasa ni Operation M4C Pamoja Daima.......
 
Kumchinja KOBE kunahitaji Timing sana.


Katika kile kinachoonekana kujihakikishia Urais 2015 aliyewahi kuwa waziri mkuu (sio waziri mkuu mstaafu kwani uwaziri sio nafasi ya kuajiriwa na kisha kustaafu) ndugu Lowasa ameanza ama anaendeleza kazi ya kuwamgia mamilioni viongoz wakuu wa chadema katika kumsafishia njia.
Najua suala hili litashtusha wengi lakini ndio uhalisia kwani tangia mwaka 2010 viongozi wa kitaifa wa CHADEMA wamebakia kuwaandama viongozi wengine wa CCM huku wakifumbia madudu na uchafu anaoendelea kuufanya Lowasa kama kwamba hawaoni hadi hatua ya wanachama na wapenzi kuanza kuhoji kwa nn Lowasa hazungumziwi? ambapo majibu rahisi na yasiyo na mshiko kutoka kwa viongozi wa chama ni kwamba Lowasa kwa kuwa atapishwa na CCM mwaka 2015 kugombea urais sio sawa kumzungumzia kwa sasa kwani kutampa mwanya wa kujisafisha katika kashfa zake na hivo kukosa hoja za kumchafua kwa wananchi kama ilivyo kawaida ya siasa za Tanzania ili upendwe unatengeza fitina mwenzio achukiwe.
ukweli ni kwamba Lowasa amekuwa akiwapa mamilioni viongozi hao ili kuwadhoofisha wapinzani wake na hatimaye kujihakikishia kupitishwa na chama chake kugombea uraisi.

Lowasa na Zitto kabwe.
kuna taarifa za chinichini kuwa kufukuzwa kwa Zitto kabwe pia kuna mkono wa Lowasa amabaye ni mmoja wa vigogo walioficha pesa nje na hivyo kama njia ya kudhoofisha mjadala wa pesa hizo kurudishwa ni kumuudhofisha mtoa mada na hivyo Lowasa alimwaga pesa zilizotumika kushawishi wajumbe wa kamati kuu ya CHADEMA kumuondoa Zitto na kufanikisha mikutano nchi nzima ya kuweka upepo sawa kujinuru na kifo cha mpasuko wa chama.

CHADEMA WAANZA KUMPIGIA KAMPENI LOWASA.
Hivi karibuni licha ya kutokuzungumzia rushwa za kutisha ambazo lowasa anazitoa, viongozi wa chadema wameanza kumpigia debe kiaina lowasa kwa kuueleza umma kwamba anachotoa lowasa ni misaada na isiwafanye wamuunge mkono. Chadema wanasema wananchi wamuunge mkono lowasa kama ataamua kugombea kupitia chama kingine ambacho si CCM na kwa maana hii Chadema wako tayari kumpokea mtu huyu ambaye miaka mitatu minne iliyopita walimandama kwa kumwita FISADI wa Richmond na mengine mengi. Ama kweli PESA SABUNI YA ROHO!!!!!!
katika operesheni ya chadema ya sasa Lowasa ananadiwa LIVE na ukitaka ushahidi wa wazi rejea gazeti la leo la mwananchi 24/01/2014 "CHADEMA: BODABODA ACHANENI NA LOWASSA" Ambapo chadema kinadai "MUNAWEZA KUMUUNGA MKONO KAMA AKIACHANA NA CCM NA KUAMUA KWENDA CHAMA KINGINE".
Hakuna kama pesa, hakuna kama rushwa, tuna safari ndefu sana kupata upinzani wa kweli na kupata viongozi sahihi. ninchojiuliza ni Haya mamilioni yanayopelekwa chadema na sehemu nyingine yatarudishwaje? na hizi hasira na usongo wa uraisi anaoukimbilia lowasa akipita nini kitajr?
 
Uandishi wako ukiutafakari dhahiri unaonyesha upo kambi ambayo Lowasa ameibana kila kona.
Tutarajie mengi kabla ya December
 
Kama na wewe unazitaka jipange msikitini au kanisani fungu litakupitia .. Akitoa kwenye chaguzi tunazila zote bure
 
Uandishi wako ukiutafakari dhahiri unaonyesha upo kambi ambayo Lowasa ameibana kila kona.
Tutarajie mengi kabla ya December

tena itakuwa ni ile kambi ya membe,lowassa kawabana mbavu,hakuna anayepumua
 
Hivi kutaja majina walioficha mapesa akaunti za nje ni sharti zzk angebaki na uongoz ndan ya cdm na si ubunge? Kama si lazima awe kiongozi ndani ya chama mbali na ubunge basi hoja haina mashiko mkuu.
 
Halafu kuna Wapuuz.i wamekugongea like.
 
Kama nyie CCM mumeshindwa kumvua gamba Lowasa mnataka Chadema ndiyo wafanye kazi hiyo? Na kwa vile JK anamgwaya Lowasa basi naye ni Chadema? Mnae huyo na atawapelekesha kama gari bovu. Chadema hawarembi kiongozi akileta ujinga anapigwa chini tu.
 
We ni mbumbumbu kichwan. possiblely hata drs la kwanza hujaingia.hizo buku7 za lumumba zina kusumbua
Kwa neno hilo hapo kwenye nyekundu wewe ndio unaonekana Mbumbumbu zaidi......Kwa nini usiandike Kiswahili tu kama Lugha ya Malkia hauiwezi?
 
Halafu kuna Wapuuz.i wamekugongea like.
Kugongewa Like ndani ya JF kuna maana nyingi sana mkuu tofauti na unavyodhani......Si Busara hata kidogo kusema 'kuna wapuuzi wamemgongea Like'.....
 
Kugongewa Like ndani ya JF kuna maana nyingi sana mkuu tofauti na unavyodhani......Si Busara hata kidogo kusema 'kuna wapuuzi wamemgongea Like'.....

Mkuu hebu share hizo maana...
Other wise, statement yangu ina hold
 
Yaani Lowassa awashinde CCM halafu mtarajie CHADEMA iwasaidie? Shughulikeni na mtu wenu huko, akiwashinda shauri yenu.
Tiba

Kweli CCM kweli ni Chama dhaifu! Yaani baada ya kushindwa kumsughulikia Lowassa, sasa wanaomba msaada "KIANA" CDM iwasaidie? This is unbelievable. BTW, Sala za CDM siku zote imekuwa ni CCM wafanye kosa la kiufundi wamsimamishe Lowassa kugombea Urais. CDM kwenda Magogoni itakuwa kama vile kusukuma mlevi.
 
ni wazi kuwa sasa CDM imeishika CCM kubaya..sasa makundi ya CCM yanaongozwa na CDM
 
Katika kile kinachoonekana kujihakikishia Urais 2015
aliyewahi kuwa waziri mkuu (sio waziri mkuu mstaafu
kwani uwaziri sio nafasi ya kuajiriwa na kisha kustaafu)
ndugu Lowasa ameanza ama anaendeleza kazi ya
kuwamgia mamilioni viongoz wakuu wa chadema
katika kumsafishia njia. Najua suala hili litashtusha
wengi lakini ndio uhalisia kwani tangia mwaka 2010
viongozi wa kitaifa wa CHADEMA wamebakia
kuwaandama viongozi wengine wa CCM huku
wakifumbia madudu na uchafu anaoendelea kuufanya
Lowasa kama kwamba hawaoni hadi hatua ya
wanachama na wapenzi kuanza kuhoji kwa nn Lowasa
hazungumziwi? ambapo majibu rahisi na yasiyo na
mshiko kutoka kwa viongozi wa chama ni kwamba
Lowasa kwa kuwa atapishwa na CCM mwaka 2015
kugombea urais sio sawa kumzungumzia kwa sasa
kwani kutampa mwanya wa kujisafisha katika kashfa
zake na hivo kukosa hoja za kumchafua kwa wananchi
kama ilivyo kawaida ya siasa za Tanzania ili upendwe
unatengeza fitina mwenzio achukiwe. ukweli ni
kwamba Lowasa amekuwa akiwapa mamilioni viongozi
hao ili kuwadhoofisha wapinzani wake na hatimaye
kujihakikishia kupitishwa na chama chake kugombea
uraisi.

Lowasa Na Zitto Kabwe.

kuna taarifa za chinichini kuwa kufukuzwa kwa Zitto
kabwe pia kuna mkono wa Lowasa amabaye ni mmoja
wa vigogo walioficha pesa nje na hivyo kama njia ya
kudhoofisha mjadala wa pesa hizo kurudishwa ni
kumuudhofisha mtoa mada na hivyo Lowasa alimwaga
pesa zilizotumika kushawishi wajumbe wa kamati kuu
ya CHADEMA kumuondoa Zitto na kufanikisha mikutano
nchi nzima ya kuweka upepo sawa kujinuru na kifo cha
mpasuko wa chama.

CHADEMA WAANZA KUMPIGIA KAMPENI LOWASA.

Hivi karibuni licha ya kutokuzungumzia rushwa za
kutisha ambazo lowasa anazitoa, viongozi wa chadema
wameanza kumpigia debe kiaina lowasa kwa kuueleza
umma kwamba anachotoa lowasa ni misaada na
isiwafanye wamuunge mkono. Chadema wanasema
wananchi wamuunge mkono lowasa kama ataamua
kugombea kupitia chama kingine ambacho si CCM na
kwa maana hii Chadema wako tayari kumpokea mtu
huyu ambaye miaka mitatu minne iliyopita
walimandama kwa kumwita FISADI wa Richmond na
mengine mengi. Ama kweli PESA SABUNI YA ROHO!!!!!!
katika operesheni ya chadema ya sasa Lowasa
ananadiwa LIVE na ukitaka ushahidi wa wazi rejea
gazeti la leo la mwananchi 24/01/2014 "CHADEMA:
BODABODA ACHANENI NA LOWASSA" Ambapo chadema
kinadai "MUNAWEZA KUMUUNGA MKONO KAMA
AKIACHANA NA CCM NA KUAMUA KWENDA CHAMA
KINGINE".
Hakuna kama pesa, hakuna kama rushwa, tuna safari
ndefu sana kupata upinzani wa kweli na kupata
viongozi sahihi. ninchojiuliza ni Haya mamilioni
yanayopelekwa chadema na sehemu nyingine
yatarudishwaje? na hizi hasira na usongo wa uraisi
anaoukimbilia lowasa akipita nini kitajr?

Hekaya za Abunuasi hizi.
 
Kwa kifupi mtoa mada anataka cdm ifanye kazi ya kumdhibiti lowasa baada ya ccm kushindwa!
 
Kuna watu wanadhani hii mada nimeileta kishabiki bila utafit na wengine kuhoji elimu yangu. Mara nying msomi hawez kuwa na mawazo dhaifu ya kuhoji mtoa mada au mchangia hoja ana elimu gani, na ndio maana vitabu vingi vinavyoandikwa na wasomi hutakuta baada ya jina la mwandishi aandike yeye ni profesa au dk. ndo uamini yale aliyoyaandika. Kuna aina nyingi za ushahidi ukiwemo wa kimazingira na mada hii au utata wa pande hizo unathibitishwa kimazingira kwanza. Hii ni kwasababu mipango michafu huwa haisaniwi kwa mikataba ya kuitwa waandishi. kikubwa wanajamvi msiukimbie ukweli. Pokea taarifa mpya endeleza uchunguzi kisha fanya maamuzi sahihi. KUMBUKA TANZANIA TUITAKAYO HAIWEZI KULETWA NA MAFISADI WALEWALE KWA POROJO ZILEZILE. matokeo ya uongozi uliopo sasa huwezi kuyatenganisha na lowasa. Tusijifanye vipofu kwenye zaidi ya bilioni 200 za RICHMOND na bilioni 133 za EPPA.
Weka facts hapa sio ngonjera
 
Back
Top Bottom