Kuna watu wanadhani hii mada nimeileta kishabiki bila utafit na wengine kuhoji elimu yangu. Mara nying msomi hawez kuwa na mawazo dhaifu ya kuhoji mtoa mada au mchangia hoja ana elimu gani, na ndio maana vitabu vingi vinavyoandikwa na wasomi hutakuta baada ya jina la mwandishi aandike yeye ni profesa au dk. ndo uamini yale aliyoyaandika. Kuna aina nyingi za ushahidi ukiwemo wa kimazingira na mada hii au utata wa pande hizo unathibitishwa kimazingira kwanza. Hii ni kwasababu mipango michafu huwa haisaniwi kwa mikataba ya kuitwa waandishi. kikubwa wanajamvi msiukimbie ukweli. Pokea taarifa mpya endeleza uchunguzi kisha fanya maamuzi sahihi. KUMBUKA TANZANIA TUITAKAYO HAIWEZI KULETWA NA MAFISADI WALEWALE KWA POROJO ZILEZILE. matokeo ya uongozi uliopo sasa huwezi kuyatenganisha na lowasa. Tusijifanye vipofu kwenye zaidi ya bilioni 200 za RICHMOND na bilioni 133 za EPPA.