Mambosasa: Tumempuuza Mwamakula na kumuachia baada ya kutimiza masharti ya dhamana

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,504
2,000
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemuachia kwa dhamana Askofu Emmaus Mwamakula wa kanisa la Uamsho la Moravian baada ya kufanya upekuzi nyumbani kwake.

Taarifa za kushikiliwa Mwamakula zilitolewa na polisi jana Jumatatu Februari 15, 2021 kupitia mtandao wa kijamiii kabla ya Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuthibitisha kumshikilia.

Akizungumza leo Jumanne Februari 16,2021 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema baada ya jeshi hilo kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake limemuachia baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

“Tumempuuza na baada ya kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake, mchana huu tumemuachia kwa dhamana baada ya kutimiza masharti,” amesema.

Awali polisi walieleza kumshikilia kumshikilia Mwamakula kutokana na taarifa aliyoichapisha mtandaoni iliyokuwa ikihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuandamana kushinikiza kudai katiba mpya jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Mwananchi
 

Mzee23

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
1,210
2,000
Leo umekumbuka kuweka chanzo cha taarifa... Umekua sasa
emoji847.png
 

Mnondwe

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
3,917
2,000
Sasa wamempuuza halafu wanamuachia kwa DHAMANA,wakati walipasea kumuachia BILA dhamana kama wamempuuza kweli?Hii inamaanaisha WAMEMJALI,haya mambo haya bana,Mr.Jungle.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom