Mambosasa: Tumempuuza Mwamakula na kumuachia baada ya kutimiza masharti ya dhamana

Tumempuuza lina maana gani kwenye hii context
Kujikosha na kuleta propaganda za kipuuzi. Nilipiga kura kwa JPM na nyumbani kwangu nilisaidia kuhifadhi askari aliyekuwa amepangiwa kulinda kituo 'X' Tabata (alikuja akalala kwangu na asubuhi nilienda nae kituo cha kupiga kura).
Nilifanya kosa kubwa sana kuchagua huyu mtu (JPM), tuna Rais ambaye hana QUALITIES za kuwa Mkuu wa nchi.
Kwa utaratibu na tabia zake ndiyo kafanya taasisi zote ziwe zinafanya kazi kwa HOFU na PROPAGANDA.
 
Haka kaaskofu kakimatwa unalalamika, kakiachiwa vile vile unalalamika; wewe vipi wewe


Mnajipatia laana bure. SHauri zenu. Endekezeni sana njaa hadi Ubongo uanze kutoa funza. Huyo Mzee ni umri wa baba yako au baba yako mdogo. Jiamini wewe una mwili mkubwa and you are strong.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemuachia kwa dhamana Askofu Emmaus Mwamakula wa kanisa la Uamsho la Moravian baada ya kufanya upekuzi nyumbani kwake.

Taarifa za kushikiliwa Mwamakula zilitolewa na polisi jana Jumatatu Februari 15, 2021 kupitia mtandao wa kijamiii kabla ya Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuthibitisha kumshikilia.

Akizungumza leo Jumanne Februari 16,2021 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema baada ya jeshi hilo kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake limemuachia baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

“Tumempuuza na baada ya kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake, mchana huu tumemuachia kwa dhamana baada ya kutimiza masharti,” amesema.

Awali polisi walieleza kumshikilia kumshikilia Mwamakula kutokana na taarifa aliyoichapisha mtandaoni iliyokuwa ikihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuandamana kushinikiza kudai katiba mpya jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Mwananchi
Wamempa kiki isiyo ya lazima

Yule Ni wa kuignore tu
 
Hivi polisi kwenda kusachi nyumbani ndiyo action na. one kwenye kila tukio? Yaani tukio wamedai wameliona mtandaoni...

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Baba askofu kesho badili gia angani msifie mzee wa nchi uone utakavyopambwa hadi ulinzi nyumbani kwako utapewa!!

Hii ndiyo Tanzania mpya!! Ni mwendo wa kusifu na kuabudu tu ukienda kinyume....unapimwa mkojo na sachi ya nguvu chumbani kwako!!
 
Back
Top Bottom