SoC02 Mambo yanayopaswa kuongezwa kwenye mitaala ya shule zetu

Stories of Change - 2022 Competition

Tyler Durden

Member
Aug 5, 2021
73
114
Ni ukweli usiopingika kuwa mfumo wetu wa elimu unapumulia mashine kwa sasa.
Mazao yanayozalishwa na mfumo huu yamedoda sokoni, Hali si Hali, ni muda sahihi sasa wa kufanya mabadiliko.

Mfumo wa sasa Tunafundishwa mambo mengi yasiyo na tija kwa sasa,tena kwa lugha tusiyoimudu. Tunafundishwa historia za wenzetu na Sayansi za nadharia zisizokubalika nje ya mipaka yetu,
Nimevutwa na kuandika makala haya hasa baada ya kupata taarifa juu ya kifo cha malkia wa Uingereza.

Nikakumbuka wakati fulani nikiwa masomoni kidato cha tano na sita katika somo la historia mbili tulivyokuwa tukifundishwa kinaga ubaga juu ya historia ya falme hizi za bara ulaya.

Hii ilipelekea kukariri sana majina na mambo chungu nzima waliyofanya hawa mabwana.

Tulilazimika kusoma haya kwa sababu tumerithi mitaala hii kutoka kwa hawa waliowahi kuwa watawala wetu.
Tumerithi mitaala hii, siyo Jambo baya lazini swali la kujiuliza ni je? Tumefanya nini kuboresha mitaala hii miaka zaidi ya sitini baadaye?

Kuna tija kweli kusoma kuhusu watawala hawa ambao sio watawala wetu kwa sasa? Hili tutajadili siku nyingine,
Jambo lililonisumbua ni baada ya kugundua hata hawa waingereza waliotuletea mitaala hii hawaitumii tena.!!!

Wamefanya maboresho mengi sana kulingana na nyakati zinavyobadilika.. Ukitaka kuamini haya beba vyeti vyako ukatafute kazi katika nchi zao, kwa kifupi hawaiamini tena elimu yetu, elimu waiyotuletea wenyewe na kutuambia ni bora.

kila uvumbuzi unapofanyika iwe katika teknolojia, tiba, uhandisi n.k wamekuwa wakifanya mipango na kuingiza taaluma hizo katika mitaala yao.

Kwanini sisi nasi tusibadilike.?
Mbali na maboresho tunayotakiwa kuyafanya kwa haraka, sio mbaya kama tukiongeza pia vitu vya kwetu, vinavyotufaa kikwetu kwetu ambavyo tuliviondoa na madhara yake yanaonekana wazi?.

Nchi za bara la Asia mfano Japan au Korea ya kusini ni watu walioakisi sana teknolojia na maendeleo ya nchi za ulaya na marekani, lakini bado wamefanikiwa pakubwa kuhifadhi tamaduni na asili zao ikiwemo lugha, mavazi, nidhamu, heshima, Mila, desturi n.k .

Sisi kwa upande wetu tumepoteza asili yetu, si mavazi, lugha , au tamaduni, yaani tumejaa umarekani,! hahaha.
Wenzetu wa Asia hawa wamewea kulinda tamaduni na maadili yao kwa sababu ni vitu vinavyofundishwa katika mitaala ya elimu zao .

waligoma kupangiwa nini cha kufundisha vizazi vyao. Waliamini katika tamaduni zao na kuambukiza vizazi na vizazi.

Leo hii ukishauri tufundishe staha za kitanzania mashuleni utaonekana punguwani.
Waswahili wanasema kuanza upya si ujinga.
Haya ni baadhi ya mambo yanayopaswa kuanzishwa na baadhi kuongezwa kwenye mfumo wetu wa elimu ili kuweza kukimbizana na kasi ya dunia na kurahisisha maisha ya kila siku.

1. Huduma ya kwanza
huduma ya kwanza huokoa maisha, ni vyema katika somo la baiyologia tukaweka mada ya huduma ya kwanza itakayofundishwa kila mwaka wa masomo mpaka pale mwanafunzi atapohitimu .
Raia wengi tumekuwa mbumbumbu kwenye swala la kutoa huduma ya kwanza kabla ya kufikisha wagonjwa hospitali. Ukizingatia umbali na ubovu wa miundombinu hasa maeneo ya vijijini, ni vyema elimu hii ikaanza kufundishwa Mara moja.

2. Nidhamu na utunzaji muda
Nidhamu ina wigo mpana lakini ni vyema kuwa na elimu ya nidhamu ya fedha, nidhamu ya usafi, majukumu, adabu, n.k. nidhamu huleta mafanikio, hukusaidia kukamilisha mambo yako na kuepusha tabia ya kuahirisha mipango yako.
Watanzania tumekuwa na tatizo la kuheshimu muda, elimu hii ikitolewa italeta tija na kuongeza ufanisi katika kazi.

3. Vipaji na michezo
Kila mwanadamu amezaliwa na kipaji maalumu, inaweza kuwa uchoraji, muziki( kuimba, kupiga vyombo, au ughani wa mashairi) , sarakasi, upishi, umahiri katika mchezo fulani, ucheshi na mambo mwengine mengi, vipaji huzalisha maelfu ya ajira kila kukicha.
Ni shule chache sana za serikali ambazo bado zinafundisha masomo ya vipaji mfano uchoraji na muziki, sasa tunaimba wimbo wa sayansi, sayansi, sayansi, imefika pahala tuna wahitimu wengi wa sayansi hadi wanakosa nafasi wanaamua kugeukia tena vipaji vyao....vipi kama tungeweka usawa katika kutoa elimu hizi?
Naamini tungepiga hatua katika michezo na kutangaza nchi yetu kama wenzetu waliotilia mkazo masomo hayo.

4. Elimu ya fedha na uwekezaji
Elimu hii ilipaswa kuwa lazima kwa kila mwanafunzi, ni mambo yanayogusa maisha ya kila siku, katika elimu ya fedha kuna maswala ya kodi, bima, mikopo, bajeti, n.k.

watu wengi wanaumia kwa kukosa elimu hii mfano riba kwenye mikopo, uwekezaji mbovu, matumizi mabaya ya fedha, na kushindwa kutunza fedha.

Elimu hii ikitolewa kwa wote itasaidia sana jamii yetu kupiga hatua kwenye maswala ya biashara.

5. Elimu ya Mahusiano.
Moja kati ya mambo yanayoathiri maisha ya vijana wengi hasa watoto wa kike ni kutokuwepo kwa somo hili.
Watoto wengi wa kike wamekuwa wakirubuniwa na kuharibu maisha yao kwa kutokufahamu chochote katika masuala haya, watu wengi wanatamani mambo mengi wangefahamu kipindi wakiwa bado wadogo.
Ni muhimu sasa kuwa na somo hili hasa ukizingatia hivi karibuni kumekuwa na visa vya mauaji yanayotokana na mahusiano.

6.Afya ya akili.
Kuna mambo yanatukuta sasa tumekuwa watu wazima hatujui hata tuanzie wapi!
Vitu kama masongo wa mawazo, mkazo, wasiwasi , kuchanganyikiwa , ni mambo yanayotibika kabla ya kuleta madhara,
kuna wataalamu ambao unaweza kuwaamini na kufunguka yanayokusibu, hii itasaidia sana afya ya akili kuwa sawa na kuepuka madhara makubwa yanayoweka kutokea.

7. Kujiamini na kuzungumza mbele ya kadamnasi.
Ndoto nyingi zimepotea, mawazo bora ya biashara yamepotea kwa sababu tu watu wanakosa kujiamini.
Hakuna kitu kibaya kama ukishajiona huwezi, hasa kwa wanafunzi wanaofeli katika masomo yao. Inabidi mwanafunzi waanze kuelezwa umuhimu wao na kwamba kufeli masomo hakuwafanyi kuwa watu wasioweza. Kujiamini peke yake kunaweza kubadilisha maisha ya vijana wengi.
Sanaa nyingine muhimu kufundishwa ni kuzungumza mbele ya kadamnasi tunapoteza viongozi wengi mahiri kwa kutofahamu vizuri jinsi ya kujieleza na kuzungumza mbele za watu.

8. Haki za Raia na sheria
Unaelewa haki zako kisheria kama Raia? Ni Mara ngapi umekuwa ukifahamu Jambo unaloenda kufanya kama linavunja sheria ama la? Hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya uvunjifu wa sheria na haki hasa katika vituo vya polisi.
Raia wengi hawazijui haki zao hivyo wamekuwa wakiona ni sawa. Je tunaelewa kuwa kuna vyombo unaweza kwenda kulalamika ukifanyiwa ukatili wa kisheria?
Ni muhimu mwanafunzi wakaanza kupewa elimu hii ili kila anayemaliza masomo yake awe na msingi wa elimu ya sheria.

9. Elimu ya lishe na mazoezi
Kumekuwa na ongezeko la magojwa yasiyoambukizwa na unene kupita kiasi miongoni wa watanzania hivi karibuni.

Watanzania tumekuwa wavivu kufanya mazoezi sababu sio utamaduni tuliojengewa tukiwa mashuleni.
Ulaji mbovu nao umekuwa tatizo si kwa wenyenazo au walalahoi wote tunakula hovyo. Tunakula sana vikaangwavyo vinavyotukaanga kweli kweli.

Ni muda sasa wa kuanza kupata elimu hii ya lishe na kufanya mazoezi ili kujenga tabia itayosaidia afya za kizazi kijacho.

10. kutangaza, kupatana na kuuza.
Tunaondoka katika uchumi kazi muda sio mrefu tutaamia uchumi wa taaluma hasa baada ya ujio wa mtandao.

Mitandao umekuwa ikiwezesha wataalamu kuuza taaluma zao na kutoka huduma mtandaoni. Ukiwa na elimu ya kutangaza na kuelezea vizuri unachouza itasaidia hasa ukizingatia, tunakoelekea sehemu kubwa ya biashara itakuwa ikifanyika mtandaoni.

11. Pesa za kidijitali.
Nakumbuka mwaka Jana 2021 tajiri namba moja duniani Elon musk, anayemiliki kampuni kubwa ya kuuza magari yanayotumia umeme, alitangaza kampuni hiyo kuanza kupokea sarafu hizi katika mauzo.
Hii inamaanisha pesa hizi zimeanza kutambulika na kutumika, je tunaelewa chochote kuhusu fedha hizi?
Ni muda sasa wa kuanza kutoa elimu hii katika shule zetu ili kuandaa kizazi kijacho wasije achwa nyuma.

12. Kuandaa wasifu wa kazi na usahili.
Wahitimu wengi mahiri wanakosa nafasi za kazi kisa tu wanashindwa kuandika vizuri barua, kuandaa wasifu mzuri wa kazi au kufahamu mbinu za kujielezea mbele ya wanaomhoji.

Elimu hii umekuwa ikitolewa kuanzia kidato cha sita tena kwenye somo la lugha ya kiingreza pekee, vipi wahitimu wasiosoma somo hili? Tunawasaidiaje.

Ni muda sasa kila mwanafunzi aanze kupata elimu hii kwa undani na uzito wa Hali ya juu ili iwe msaada baada ya kuhitimu masomo.

Yapo mambo mengi zaidi yanayopaswa kufundishwa mashuleni lakini tunaweza kuanza na haya machache.
Ni muda sasa wa waziri mwenye dhamana ya elimu kukaa chini na wadau wa elimu ili kuweza kujadili mambo haya na kuanza utekelezaji.

Nakaribisha michango zaidi katika suala hili.

Nawasilisha.
 
Shukran kwa uzi huu mzuri naamini serikali yetu wakiyazingatia haya bs tutakua na taifa lenye kuendana na technologia ya sasa
 
Tatizo wanapita kimyakimya hapa lakini mkuu umenena ukweli mtupu tukiendelea hivi tunaenda kuwa jamii isiyo na historia wala tamaduni na bahati mbaya elimu imegeuzwa kuwa mtaji wa wanasiasa kila siku wanakurupuka na mikakati isiyotekelezeka kifupi hali ya Elimu hapa Nchini ni mbaya mno
 
Umetoa bonge la Uzi ambao MTU yeyote akitulia akasoma,akauchambua na kuufanyia kazi hawezi kutoka Kapa lazima atapata tu Cha kumsaidia kuweka mambo yake vyema! Elimu iliyotolewa miaka ya 1920 mpaka miaka ya 60s na Ile ya 1990 Kuna Utofauti sana kulingana na Muda na mazingira yalivyokuwa. Global World ni Dunia ambayo bila umakini ni pata potea. Tunaposema Elimu ni ufunguo Wa Maisha basi ni wazi kuwa kitasa ni kipi?

Tunashauri watu waliopo Kwenye mamlaka wafanye utafiti wa kutosha kujua Dunia ya Sasa inakoelekea Ili waje na sera nzuri ya Elimu, rafiki na inayoishi Kwa Maisha ya Kila mtanzania.
 
Back
Top Bottom