Mambo yanayoiaibisha Marekani kwenye vita vya Ukraine na Urusi

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,194
10,929
Kwanza ni nia ya Maarekani kupunguza uzalishaji wa hewa chafu ya Carbondioxide. Ili kuwezesha azma hiyo ni lazima Marekani iongeze uzalishaji wa nguvu za nyuklia kwa matumizi ya viwanda vyake.

Kazi hiyo huwa ni ngumu kwani kampuni inayouza mafuta ya kutengenezea nguvu za nyuklia kwa matumizi hayo ni moja tu ROSATOM ambayo ni ya Urusi.

Jengine Marekani imepeleka agizo jipya kwa kampuni ya Martin ili iongeze kasi ya kutengeneza silaha za makombora ya masafa marefu ili kuziba pengo haraka la zile silaha ilizozigawa kwa Ukraine.

Marekani hiyo hiyo imevunja katazo lake la kuisaidia silaha Cyprus katika ugomvi wake na Uturuki. Ilifanya hivyo kwa takriban miaka 20 ili visiwa hivyo visijejiunga na mrengo wa Urusi.

Sasa pamoja na kwamba inapingana na sera ya umoja wa NATO kumsaidia adui wa mwenzao imebidi ifanye hivyo ili kuongeza biashara ya silaha.

Katika mfululizo wa aibu hizo taifa la Marekani limeonekana kujali sana droni za Iran na kuamua kutoa wito kwa mataifa yote washirika wailaani Iran na pia waiwekee vikwazo vya kiuchumi kwa madai kuwa inaisaidia Urusi kuipiga Ukraine.

Hilo linashangaza wakati wao wanaisaidia Ukraine wazi wazi kuipiga Urusi...... Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu.

1666340749550.png
 
Mabeberu hayaja wahi kuwa na akili🏃
 
Back
Top Bottom