Mambo ya kuzingatia utapoamua kujiunga na Wahuni au genge la Wanywa Damu za Watu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
MAMBO YA KUZINGATIA UTAKAPOAMUA KUJIUNGA NA WAHUNI ÀU GENGE LA WANYWA DAMU ZA WATU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Sasa umekua Mkubwa. Ni kama maisha huyaelewi hivi. Umejaribu kufuata sheria na formula ulizopewa na wazazi au walezi wako lakini umeona hazifanyi kazi yaani ni useless kama sio irrelevant. Sheria kama uwe mtiifu, sijui fanya kazi kwa bidii, sijui usiibe cha mtu wala kukitamani. Zote zimefeli. Upoupo na mambo yanakuendea vibaya huku dakika zikiwa zinakimbia vibaya.

Upande wa pili, unakuta Watu wanajibamba, Watu wanayaendesha maisha watakavyo kama mashujaa wa Rally. Majumba, magari na anasa zote wanazibomoa na kuzijenga kama hawana akili nzuri. Kihoro kinakukaba, tamaa na uchu wa maisha mazuri vinakusimanga kama binti wa kimanga anayemchamba Mgoni wake.

Unaamua kwenda kuwauliza kulikoni, mbona ninyi hamjambo wakati siye twatema vijambo na mashuzi. Yaani unanuka nje na ndani. Ndio maana wanakujibu huku wameziba pua zao wakisema sisi ni wahuni na wanywa Damu za Watu.

Basi ikiwa utakutana na Watu wa aina hiyo. Na kwa dhati yote ukaamua ujiunge nao. Haya ni mambo muhimu ya kuzingatia;

1. Macho yako usiyakuze, yafinye yawe na umbo dogo au yakwepeshe.
Jicho ni mlango wa roho. Wahuni na waovu wengi wao wanauwezo wa kusoma mawazo yako kwa kukutazama usoni kwenye macho.
Kama Taikon Master ninakushauri unapozungumzia na mtu yeyote Hasahasa mtu mnadi, mhuni hakikisha macho yako mara nyingi yawe katika umbo dogo, yakwepeshe na kama utaweza uwe unatabasamu. Ni rahisi sana kusoma saikolojia ya mtu asiyetabasamu yaani aliye - serious.
Hii italinda moyo na nafsi yako. Watu hawatajua nini unafikiri kirahisi. Hawatajua uhalisia wa reactions zako pale uwapo nao.

2. Chunga Ulimi wako.
Usiwe mtu lopolopo kama Taikon hapa. Huko ni kwa wahuni.
Unganisha ulimi na akili yako. Usipende kumsema mtu mwingine kwa ubaya au uzuri wa mtu yeyote mbele za Watu ilhali mtu huyo hayupo.
Usipende kujieleza eleza na kuombaomba excuse zisizo na kichwa wala miguu.

3. Usipende kujionyesha wala kusema unauwezo kuliko wengine.
Siku zote kama uwezo wako ni 100 basi onyesha nusu yake. Usipende kuonyesha uwezo wako wote wakati kuna kesho na kesho kutwa.
Kikawaida Watu wanaopenda kuonyesha uwezo wao hupoteza mvuto mapema na hivyo value Yao kwenye genge la wahuni na wanywa Damu hawadumu muda mrefu.

Taikon kama mastermind na multiplayer ninakushauri Siku zote uwezo unaoonyesha mbele za Watu hasa Wahuni basi uwe robo au nusu ya kile ulichonacho. Hii itakufanya uwe mtu wa suprise. Wahuni na wanyonya Damu wanapenda Watu wenye suprise, Watu wanaowashangaza, Watu wenye Plan B.
utadumu ukiwa mtu wa Plan B.

4. Usilazimishe kuaminiwa acha wakuamini wenyewe.
Imani kwa asilimia 90 hujengwa kwa Kuona. Yaani Watu wakuone wenyewe na sio ujionyeshe na kulazimisha kuwa unafaa kuaminika.
Kikawaida wahuni na wanyonya Damu wengi wao wanaakili nyingi hivyo sio rahisi kukuamini kwani wao kanuni yao kuu ni Trust no one ingawaje haimaanishi hawana Watu wanaowaamini.
Wao mara nyingi ndio hufanya usajili kwa Watu wanaowaona wanamanufaa kwao. Hivyo kwa vile wewe umeomba kujiunga nao usilazimishe wakuamini. Acha wakuamini wenyewe. Waambie wakupe kazi kisha kwenye hiyo kazi ndio maalezo na maswali yote waliyonayo yatajibiwa humo.

5. Usiwe kwaajili ya maslahi ya yeyote isipokuwa maslahi yako wewe mwenyewe.
Ingawaje kwa nje onyesha unatetea maslahi ya Wahuni na wanyonya Damu.
Hii utaionyesha kwa njia moja tuu nayo ni UPENDO. Igiza kuwa unaipenda hiyo kazi au unampenda sana kiongozi wa genge la wahuni na upo tayari kufanya lolote kwaajili yako.
Upendo ndio hauna maslahi. Wahuni wote wanajua jambo hilo.
Na ndio maana wakitaka kukuumiza hutafuta kile unachokipenda ambacho upo tayari kufanya lolote. Kwani hapo ndipo moyo na maisha yako yalipo na thamani.

6. Elewa lugha za Wahuni.
Kila utakachokiona na kukisikia kwa wahuni na wanywa Damu kina maana yake. Elewa lugha zao hii itakuweka salama.
Kikawaida kabla ya wewe kuuawa au kugeukwa na wahuni basi kuna mambo madogo madogo yatajitokeza ambayo yatakupa maana iliyosalama kwako.

Elewa kuwa mtu au kikundi ulichopo hakiwezi kukushambulia na kukudhuru pasipo taarifa, dalili.
Ni vizuri kujua lugha za mwili (body language) ili kujilinda.

7. Hesabu siku zako.
Watu wenye akili hujua kuhesabu siku zao. Wahuni ni miongoni mwa Watu wenye akili. Ukiwa nao lazima ujue kuhesabu siku zako uwapo nao.
Kila mahusiano yana mwanzo na mwisho wake. Ni vizuri kujua kuhesabu siku na kutambua nyakati uwapo na wahuni.

8. Usiwe na tamaa.
Namaanisha wahuni licha ya kuwa wanatamaa na sio waaminifu kwa asilimia kubwa lakini ndio mabingwa wa kuzuga na kujifanya hawana tamaa.
Uwapo kwenye kundi kaa ukijua wote unaowaona mbele yako wana tamaa mbaya na roho mbaya. Ila ni mabingwa wa kujifanya ni wazuri.
Nawe jifanye huna tamàa na mwaminifu. Hakikisha igizo lako lifanane na wewe. Usigundulike.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kila sehemu katika jiji la DSM, sehemu nyingine hapa nchini sina uhakika, kuna vibao vyenye kutaja namba za wahusika zikiwa na wito wa kujiunga na "Freemason" nyingine zikichagizwa na namba 666 kabisa.

Je! Hawa wajenzi huru ndio sehemu ya genge hilo la wahuni na watengeneza fursa za kutoka kwa vijana, "connection" za maana, ama kuwa na maono ya kisimati cha utajiri, yaani "midas touches"

Tafadhari pata nukuu ifuatayo kutoka katika kipande hiki cha injili,

LUKA 4

5 Kisha shetani akamchukua hadi juu ya mlima mrefu akamwonyesha kwa mara moja milki zote za dunia.

6-7 Akamwambia, “Ukipiga magoti na kuniabudu, nitakupa uwezo juu ya milki zote hizi na fahari yake; maana ni zangu na ninaweza kumpa ye yote nitakaye.”

8 Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake”

Siku zote zingatia hii kanuni ya uharibifu wa Ibilisi

Being used - Kwa mawazo
Being misused - Kwa maneno
Being abused - Kwa vitendo
Being confused - Kwa kutokutimiza wajibu wako.
 
MAMBO YA KUZINGATIA UTAKAPOAMUA KUJIUNGA NA WAHUNI ÀU GENGE LA WANYWA DAMU ZA WATU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Sasa umekua Mkubwa. Ni kama maisha huyaelewi hivi. Umejaribu kufuata sheria na formula ulizopewa na wazazi au walezi wako lakini umeona hazifanyi kazi yaani ni useless kama sio irrelevant. Sheria kama uwe mtiifu, sijui fanya kazi kwa bidii, sijui usiibe cha mtu wala kukitamani. Zote zimefeli. Upoupo na mambo yanakuendea vibaya huku dakika zikiwa zinakimbia vibaya.

Upande wa pili, unakuta Watu wanajibamba, Watu wanayaendesha maisha watakavyo kama mashujaa wa Rally. Majumba, magari na anasa zote wanazibomoa na kuzijenga kama hawana akili nzuri. Kihoro kinakukaba, tamaa na uchu wa maisha mazuri vinakusimanga kama binti wa kimanga anayemchamba Mgoni wake.

Unaamua kwenda kuwauliza kulikoni, mbona ninyi hamjambo wakati siye twatema vijambo na mashuzi. Yaani unanuka nje na ndani. Ndio maana wanakujibu huku wameziba pua zao wakisema sisi ni wahuni na wanywa Damu za Watu.

Basi ikiwa utakutana na Watu wa aina hiyo. Na kwa dhati yote ukaamua ujiunge nao. Haya ni mambo muhimu ya kuzingatia;

1. Macho yako usiyakuze, yafinye yawe na umbo dogo au yakwepeshe.
Jicho ni mlango wa roho. Wahuni na waovu wengi wao wanauwezo wa kusoma mawazo yako kwa kukutazama usoni kwenye macho.
Kama Taikon Master ninakushauri unapozungumzia na mtu yeyote Hasahasa mtu mnadi, mhuni hakikisha macho yako mara nyingi yawe katika umbo dogo, yakwepeshe na kama utaweza uwe unatabasamu. Ni rahisi sana kusoma saikolojia ya mtu asiyetabasamu yaani aliye - serious.
Hii italinda moyo na nafsi yako. Watu hawatajua nini unafikiri kirahisi. Hawatajua uhalisia wa reactions zako pale uwapo nao.

2. Chunga Ulimi wako.
Usiwe mtu lopolopo kama Taikon hapa. Huko ni kwa wahuni.
Unganisha ulimi na akili yako. Usipende kumsema mtu mwingine kwa ubaya au uzuri wa mtu yeyote mbele za Watu ilhali mtu huyo hayupo.
Usipende kujieleza eleza na kuombaomba excuse zisizo na kichwa wala miguu.

3. Usipende kujionyesha wala kusema unauwezo kuliko wengine.
Siku zote kama uwezo wako ni 100 basi onyesha nusu yake. Usipende kuonyesha uwezo wako wote wakati kuna kesho na kesho kutwa.
Kikawaida Watu wanaopenda kuonyesha uwezo wao hupoteza mvuto mapema na hivyo value Yao kwenye genge la wahuni na wanywa Damu hawadumu muda mrefu.

Taikon kama mastermind na multiplayer ninakushauri Siku zote uwezo unaoonyesha mbele za Watu hasa Wahuni basi uwe robo au nusu ya kile ulichonacho. Hii itakufanya uwe mtu wa suprise. Wahuni na wanyonya Damu wanapenda Watu wenye suprise, Watu wanaowashangaza, Watu wenye Plan B.
utadumu ukiwa mtu wa Plan B.

4. Usilazimishe kuaminiwa acha wakuamini wenyewe.
Imani kwa asilimia 90 hujengwa kwa Kuona. Yaani Watu wakuone wenyewe na sio ujionyeshe na kulazimisha kuwa unafaa kuaminika.
Kikawaida wahuni na wanyonya Damu wengi wao wanaakili nyingi hivyo sio rahisi kukuamini kwani wao kanuni yao kuu ni Trust no one ingawaje haimaanishi hawana Watu wanaowaamini.
Wao mara nyingi ndio hufanya usajili kwa Watu wanaowaona wanamanufaa kwao. Hivyo kwa vile wewe umeomba kujiunga nao usilazimishe wakuamini. Acha wakuamini wenyewe. Waambie wakupe kazi kisha kwenye hiyo kazi ndio maalezo na maswali yote waliyonayo yatajibiwa humo.

5. Usiwe kwaajili ya maslahi ya yeyote isipokuwa maslahi yako wewe mwenyewe.
Ingawaje kwa nje onyesha unatetea maslahi ya Wahuni na wanyonya Damu.
Hii utaionyesha kwa njia moja tuu nayo ni UPENDO. Igiza kuwa unaipenda hiyo kazi au unampenda sana kiongozi wa genge la wahuni na upo tayari kufanya lolote kwaajili yako.
Upendo ndio hauna maslahi. Wahuni wote wanajua jambo hilo.
Na ndio maana wakitaka kukuumiza hutafuta kile unachokipenda ambacho upo tayari kufanya lolote. Kwani hapo ndipo moyo na maisha yako yalipo na thamani.

6. Elewa lugha za Wahuni.
Kila utakachokiona na kukisikia kwa wahuni na wanywa Damu kina maana yake. Elewa lugha zao hii itakuweka salama.
Kikawaida kabla ya wewe kuuawa au kugeukwa na wahuni basi kuna mambo madogo madogo yatajitokeza ambayo yatakupa maana iliyosalama kwako.

Elewa kuwa mtu au kikundi ulichopo hakiwezi kukushambulia na kukudhuru pasipo taarifa, dalili.
Ni vizuri kujua lugha za mwili (body language) ili kujilinda.

7. Hesabu siku zako.
Watu wenye akili hujua kuhesabu siku zao. Wahuni ni miongoni mwa Watu wenye akili. Ukiwa nao lazima ujue kuhesabu siku zako uwapo nao.
Kila mahusiano yana mwanzo na mwisho wake. Ni vizuri kujua kuhesabu siku na kutambua nyakati uwapo na wahuni.

8. Usiwe na tamaa.
Namaanisha wahuni licha ya kuwa wanatamaa na sio waaminifu kwa asilimia kubwa lakini ndio mabingwa wa kuzuga na kujifanya hawana tamaa.
Uwapo kwenye kundi kaa ukijua wote unaowaona mbele yako wana tamaa mbaya na roho mbaya. Ila ni mabingwa wa kujifanya ni wazuri.
Nawe jifanye huna tamàa na mwaminifu. Hakikisha igizo lako lifanane na wewe. Usigundulike.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Cc Thadei de Mushi 😭😭😭😭😭😭😭😭
 
Back
Top Bottom