matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,596
- 15,393
1: Biblia sio kitabu cha kidini Sio kitabu cha kubishania, Ni maelezo ya Mungu mfalme aliyeumba sio tu dunia bali trillions za sayari zenye viumbe wasiohesabika. Hiyo lazima uyasome kwa adabu.
2: Usiende na ajenda yako mfukoni. Nenda kama mualikwa wa ikulu ya mbinguni kusikiliza hotuba na maelekezo ya mfalme wa wafalme. Hivyo sio kitabu cha wayahudi au wakristo ni cha kila mwanadamu.
3: Anza kwa maombi ili yeye aliyeandika akufunulie mistari itakayokusaidia wewe binafsi.
4: Maneno ya maandiko ni kama vifurushi vya nguvu, au kama zile namba za vocha ukiyaingiza moyoni yanabadilika kuwa nguvu au ujazo unaoleta athali chanya kwenye kila eneo la maisha yako. Soma ukiwa na mtazamo wa kupokea nguvu sio maelezo.
5: Amini kila neno aliloambiwa mtu yeyete katika biblia umeambiwa na wewe. Kila baraka zilizotamkwa ni zako pia. Kabla hujaanza kusoma biblia anza kujiepusha na watu wanaoiponda, mijadala isiyojengefu, watu wanaopenda mizaha na utani hata kama ni watumishi. Hii itakusaidia kuongeza umakini na kuwa na adabu kwa kauli za Mungu.
Ni hayo tu.
Kama umejifunza kitu, usisahau kucomment chochote.