Mambo ya Kuzingatia Unaponunua Simu janja (Smartphone)

Mambo ya Kuzingatia Unaponunua Simu janja (Smartphone)

Mkuu ulichosema ni.kweli hawa tecno kila toleo mpya badala ya kuongeza ubora wanashusha hiyo H7 imezidiwa hata na toleo lililotangulia la P7

Sio kila toleo. Kwani Tecno Phantom Z na Z mini inazidiwa na tecno ipi? Maana hiyo ndio latest.
 
Faidi Htc sense yaache hayo yapigane vikumbo na Tecno... Simu unabonya mpaka vidole vinauma.

Tecno Phantom Z. Ubora na gharama vinaendana. Ni simu nzuri kulinganisha na Simu nyingine za bei yake.

1431862255756.jpg
 
Shukrani kwa kutupanua wigo wa uekewa! mkuu mi nina samsung galaxy lakini namna ya kuangalia Mambo uliyo yataja nashindwa. Hebu endelea kunipa msaada.

njia rahisi kuliko zote ni kujua ni samsung galaxy ipi eg POCKET, S2,S4 chunguza hata kwenye box lake, kisha ingia google, andika hilo jina, utapata specification zote muhimu.
 
Sio kila toleo. Kwani Tecno Phantom Z na Z mini inazidiwa na tecno ipi? Maana hiyo ndio latest.

Mkuu phantomZ sijawahi kutumia na pia ubora wake siujui lakini hizo nilizotaja nimetumia. Kwa kawaida tulitegemea toleo linalofuata lije na ubora tofauti na lililotangulia.
 
MODs,
Lengo la uzi ni kuhabarishana na kusaidiana uelewa katika suala hili muhimu la IT.
Naomba kama inawezekana uzi ubaki jukwaa la habari na hoja mchanganyiko ili usaidie wengi.
Natanguliza shukrani.
 
Mkuu Goodrich,
Kuna ZTE U887 nimeletewa ina specs kama nilivyoambatanisha, kwenye wi fi inafanya vizuri lakini nimejaribu kutafuta 3G network sipati Napata EDGE pekee.
Naomba msaada katika hili
 

Attachments

Kumekuwa na simu nyingi sana za smartphone lakini je, ni ipi yenye ubora?
Wengi tumekuwa tukinunua simu kwa kuangalia mtazamo wa nje yaani jinsi inavyoonekana kwa nje. Lakini kumbe kuna sifa za muhimu za kuangalia ili kuweza kutambua simu yenye ubora kwa matumizi ya mtumiaji
Hizi hapa ni sifa ambazo unatakiwa kuzijua ili kuweza kupata simu iliyo na ubora
========

Katika ulimwengu huu wa kidijitali kuna ongezeko kubwa sana la simu za smartphone ambapo nyingi kati ya hizo nizile zinazotumia mfumo wa Android OS, iOS, Microsoft Phone 7, Blackberry OS, webOS, Symbian. Kutokana na ongezeko la simu za smartphone katika soko kumechangia kuwepo kwa simu zisizokuwa na sifa nzuri japo kimwonekano wa nje zinaonekana ni nzuri, kwa kulitambua hilo leo nataka nikupe ushauri kwa kukutajia sifa ambazo ni muhimu kuziangalia unapotaka kununua simu, hii itakusaidia wewe kupata simu nzuri kwa matumizi yako ya kila siku

Vitu hivyo ni hivi vifuatavyo

UKUBWA WA KIOO NA UIMARA WAKE
Unapo chagua simu hakikisha unachagua simu yenye kioo imara na chenye ukubwa wa kutosha, hii inajumuisha vitu vifuatavyo
  • Size ya kioo
  • Resolution viewing angles
  • Viewing angles
  • coating
  • simu inatakiwa angalau kioo chake kiwe ni inchi 4 na kuendelea.

UNENE WA SIMU NA UZITO
Hii ni sifa nyingine ya kuangalia unapo nunua simu, ni chaguo lako kutokana na mapendekezo yako wewe, lakini nakushauri unapo nunua simu ununue simu yenye unene wa wastani na uzito wa wastani

OPERATING SYSTEM INAYOTUMIWA NA SIMU
Unaponunua simu angalia simu yenye operating system nzuri ambayo itakuwezesha wewe kupata option ya kutumia kila aina ya application
zipo operating system za aina tofauti tofauti kulingana na makampuni ya simu Android OS, iOS, Microsoft Phone 7, Blackberry OS, webOS, Symbian na kadhalika. Lakini iliyo nzuri kwa kutumia ni ile ya Android ambayo ndio inayotumiwa na simu nyingi sana. Hii ni kwa sababu Android itakupa uwezo wa kutumia app nyingi katika simu yako na pia unapo tumia simu zenye mfumo mwingine utakuwa kwenye hatari ya kukosa kutumia WHATSAPP itakapofika mwishoni mwa mwaka huu.

UWEZO WA KU-UPGRADE
Unapo chagua simu hasa kwa simu za windows na android hakikisha unachagua simu ambayo itakuruhusu kufanya upgrade ili kuweza kupata version mpya ya operating system.

Mfano uwezo wa ku upgrade kutoka andriod version 3.2 hadi 4.2 ,4.4 au 5.0 n.k au kwa watumiaji wa windows kuweza kutoka windows 8.0,8.1 hado windows10.

STORAGE YA SIMU
Hakikisha unaponunua simu yako basi iwe na storage ya kutosha, hii inajumuisha RAM, INTERNAL MEMORY. Ushauri ni kuwa simu nzuri ni ile yenye RAM kuanzia 1GB na INTERNAL MEMORY ya Angalau 4GB.

Lakini pia kama simu yako ina support memory card hakikisha iwe na uwezo angalau wa kusapport memory card ya ukubwa wa kuanzia angalau 8GB.

CONNECTION YA INTERNET
Pia hakikisha unaponunua simu yako uangalie uwezo wa simu katika kuunga internet. Simu nzuri ni ile yenye uwezo wa kutumia 2G na 3g kwa pamoja lakini pia kutokana na kuja kwa mfumo wa 4G pia ni vyema ukawa na inayotumia 2G, 3G na 4G kwa pamoja, simu zinazotumia 2G peke yake kwa sasa zimeshapitwa na wakati

UWEZO WA KAMERA
Kamera ni kitu muhimu sana kwenye simu za smartphone hii ni kwa sababu humwezesha mtumiaji kuweza kuchukua matukio mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu na mambo mengine, unaponunua simu basi hakikisha unachagua simu yenye kamera angalau ya kuanzia 5px na kuendelea na kama simu ina kamera ya mbele basi hakikisha kamera ya mbele ina angalau 3px na kuendelea, hii itakuwezesha kuchukua picha zenye ubora wa hali ya juu.

Lakini pia sambamba na hilo hakikisha simu unayonunua ina flash nzuri itakayo kuwezesha kuchukua picha wakati wa usiku.

UWEZO WA BETRI
Betri ni kitu muhimu sana cha kuzingatia unaponunua simu. Hakikisha unaponunua simu unanunua simu yenye betri imara ili usije ukaishiwa chaji haraka, lakini pia hii inaendana na matumizi sahihi ya betri ya simu yako.

IWE ORIGINAL
Hakikisha unaponunua simu ununue simu ambayo ni original ili kuepuka simu yako kuzimwa ikifika siku ambayo simu zimetangazwa kuzimwa.

Zipo sifa nyingi za kufuata ili kupata simu nzuri lakini hizo hapo juu ni sifa muhimu za kufuata. Kumbuka sifa hizi zinapatikana kwenye boksi la simu husika na hakikisha ukiwasha simu sifa hizi za kwenye boksi ziendane na za kwenye kifaa.
 
Kumekuwa na simu nyingi sana za smartphone lakini je ni ipi yenye ubora?
Wengi tumekuwa tukinunua simu kwa kuangalia mtazamo wa nje yani jinsi inavyo onekana kwa njee. Lakini kumbe kuna sifa za muhimu za kuangalia ili kuweza kutambua simu yenye ubora kwa matumizi ya mtumiaji
Hizi hapa ni sifa ambazo unatakiwa kuzijua ili kuweza kupata simu iliyo na ubora

HIZI NI SIFA ZA KUANGALIA KABLA YA KUNUNUA SMARTPHONE AU TABLET - MWANAJAMII Info and Technology Solution
Shukran kwa taarifa
 
Hapo ktk operating system naona haujazungumza kisomi yaan unatumianisha tutumie android kwa kuwa inatumiwa na watu wengi!!! Na ukitumia Os zingine utakuwa ktk hatari ya kutotumia whatsap mwishon mwa mwaka?!!!! Huo ni uongo wa mchana kweupe, nilisoma taarifa juu ya whatsap kutotoa usaidiz wa baadhi ya Os lakin haikulenga mfumo mzima Bali ni version tena ni zile version za zamani sna, kwa maelezo uliyotoa unatuaminsha sisi tunao tumia mifumo ya uendeshaji tofauti na android ifikapo mwishoni mwa mwaka huu hatuwez tumia whatsap huo uongo aisee, na tena kwa swala la system update maslani wanaotumia Window phone wapo vizuri kuliko hao android. Mimi nnayo Samsung ktk swala la system update imegomea kit Kat wakati watu wa wp wanapeta tu kupata latest system update na sasa wanategemea kupata window 10 ata ukiwa na simu ya zamani.
 
Kuna uwezekano mkubwa whatsaap ikabaki kwa android na ios tuu ifikapo mwisho wa mwaka kutokana na maboresho wanayoyatazamia hayatakuwa rafiki kwa os kama symbian, blackberry, java na ndio maana makampuni hayo yameanza kuzalisha cm zitakazo run android. Sio kila usilolijua ni uongo......
 
Kwenye ku UPGRADE iOS iko vizuri maana ni sera ya Apple ku UPGRADE version.Windows pia iko poa.Android inatumiwa Na makampuni mengi Ila ni machache yanajali kama Samsung LG, Na HTC Na Nexus .Tatizo Android wengi ni Tecno,itel ,nk
 
Back
Top Bottom