Mambo ya kuzingatia katika kuchagua pafyum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo ya kuzingatia katika kuchagua pafyum

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Michael Amon, Apr 1, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  UCHAGUZI wa pafyum kwa kawaida huzingatia mambo mengi ambayo si wengi wanaoyafahamu. Mara nyingi watu huchagua pafyumu kwa kusikia harufu kutoka kwa watu wengine ama kuvutiwa na chupa za manukato hayo.


  Lakini je, unafahamu kuwa unatakiwa kuchagua pafyum kutokana na kuridhishwa na harufu yake na si vinginevyo? Suala la kupata harufu halisi ya pafyum imekuwa ni tatizo kwa watumiaji wengi, kwani wengi wao hawaelewi mambo ya kuzingatia wakati wa kuchagua.


  Yapo mambo ya kuzingatia kabla ya kununua pafyum, ambayo endapo yakifuatwa ipasavyo, yatakuweka katika nafasi ya kufanya uchaguzi ulio sahihi. Kwanza kabisa, usinunue pafyum kwa sababu tu ya kujulikana kwa nembo ya bidhaa hiyo au umaarufu wa mbunifu wake. Ili uwe na chaguo bora unashauriwa kwenda kwenye duka la pafyum wakati wa asubuhi. Inaamika kuwa, wakati huo pua yako itakuwa na uwezo mkubwa wa kupata harufu halisi. Ikiwa kwa wakati huo utakuwa na mafua ama utakuwa umechoka, si vibaya ukahairisha na kwenda siku nyingine.


  Jaribu pafyum kwenye ngozi safi ambayo haina manukato. Katika majaribio hayo unaweza kujaribu zaidi ya pafyum tatu, kwani kwa wakati huo pua yako itakuwa na uwezo mkubwa wa kupata harufu na kutofautisha. Usinuse juu ya kizibo cha chupa kwa sababu harufu utakayoipata haitakuwa halisi. Unaweza kupata harufu ya nyingine badala ya ile ya manukato unayokusudia. Usijaribishe pafyum kwa kupaka katika kipande cha karatasi. Unapojipulizia pafyum kwa mara ya kwanza ukiwa na lengo la kupata harufu yake, hakikisha unakaa kwa dakika 30.


  Hapo ndipo utakapopata harufu halisi ya pafyume hiyo. Ikiwa tayari umeamua kununua, hakikisha unachagua chupa ndogo. Kwani kwa kawaida pafyum huisha muda wake miaka mitatu baada ya kutengenezwa. Hata kama huitumii mara kwa mara, inaweza kubadilika na kupoteza harufu yake halisi. Kwa kawaida pafyum hupakwa kulingana na jinsia na umri. Kwani siku zote pafyum za wanawake ni tofauti na zile za wanaume.

  E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
   
 2. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  We kila siku unakuja na post za kike-kike zaidi.
  Kesho utaleta ya namna ya kuchagua wanja na lipstick.
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  @mwali!amekosea?
   
 4. bht

  bht JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Kibongo bongo colognes na perfume zote ni perfumes tu....lol
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  @mwali!amekosea?
   
 6. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hii mada wala sio ya kike kike. Kuna wanaume na wanawake wanapaka perfume mbaya sana. Wengine hawataki kutumia deodorant wala perfume na matokeo yake akija ofisini kwako unaomba amani kwa hiyo harufu anayokuachia. Hawaogi wakatakata na wala hawatumii deodorant au perfume basi ndiyo balaa. Wengine perfume zina harufu kaliiii ofisini, lazima tujifunze mambo haya.

  Asante mleta mada
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Mie nna ugonjwa wa perfumes!
  YM, asante kwa kushare hii. Ni muhimu nadhani kununua tester (inakuwa 1ml, inaweza kugawiwa bure pia) wakati unajaribu uturi mupya. Kuna siku nilinunua ki-uturi kidogo cha 5ml cha christian dior poison, nikakifungua. Keshoye nikagundua ina-melt kifuniko. Nikaogopa kuitumia hadi ikaisha yenyewe. Sijathubutu tena!
   
 8. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,797
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Mkuu uliyosema hapo juu ni kweli kabisa. Tena wale wenye perfum zenye harufu mbaya wanajiona wamepatia kwelikweli, anapulizia kila wakati. Tena kuna perfum moja yenyewe ina harufu ya kikwapa kabisa jina siijui na wala sijaina ila kuna baadhi ya watu wanaipenda sana maana nimeishaisikia kwa zaidi ya mtu mmoja, kweli huwa ina nikerehesha. Kuna mshkaj wangu aliwahi kuitumia ikabidi nimzuge ni ya madem. Akaacha!
   
 9. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #9
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280

  Dear mzima??

  Youngmaster af analalamika kwamba facebook anatongozwa na wanaume..sasa kama huko fb ana post mambo haya watu si watashindwa kutofautisha kati yake na Rio?? umeona avatar yake hayo macho?? ha ha jaman!!
   
 10. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mzima kabisa TBag, mtu Khatar.
  Unataka kunisemesha kitu ambacho sijasema...
  Ila kusema kweli kuna kitu kinanishangaza kwa rafiki yangu YM
  Juzi alirusha uzi wa namna mwanaume anatakiwa kuosha sura
  leo analeta za perfume na colognes (thanks BHT)
  Kesho ataleta nini? he is getting closer and closer.
  Angerusha hata kamoja ambako sio urembo-related
  then after a week or two arushe tena hizi. but kwa sasa...:thinking:

   
 11. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #11
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280

  Hilo nalo neno mwaya..japokua kumwambia kuhusu kutongozwa on fb inatokea mara kwa mara lakini kwa trend hii huko fb si wanakoma? itakua anaweka tu "naosha kucha mwenge" au "having good time with mylove" try get a picture!..nilipata shida sana fb..YM badilika kijana..ohooo
   
 12. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #12
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Kwani perfume wanatumia wanawake tu?
   
 13. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #13
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu kwa kuliona hilo. Mimi nimeona niilete hii mada maana nimeona watu wengi ahwajui kuchagua paerfume matokeo yake tunaishia kuchagua perfume za ajabu ajabu nyingine zinanuka kama bomu.
   
 14. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #14
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Duh! Ulinunua perfume yenye poison? Ulitaka kujiua au?
   
 15. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #15
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Ha ha haaaa!! Duh! Kumbe kuna perfume zinazonuka kama kikwapa? Hii kali.
   
 16. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #16
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Haya maneno umeyatoa wapi? Na mbona facebook nilishajitoa siku nyingi? Na sijawahi kupost mambo kama haya huko.
   
 17. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #17
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Unadhani mimi huwa narusha mambo ya urembo tu? embu angalia my latest threads ili ujue ninachoanzisha before haujacomment.
   
 18. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #18
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  kwani mi na ww tulishawahi kua marafiki fb?? mi nazungumzia kwa reference za JF humu humu..hata mi nili deactivate...salam zako!!
   
 19. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #19
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Naomba unielewe kitu kimoja. Mimi huwa naweka threads ambazo naamini kuwa zitawasaidia wana JF kwa namna moja au nyingine na sidhani kama kuna dhambi kujifunza mambo mbali mbali hasa urembo. Inamaana wale wanaume wanaofanya kazi za urembo masaloon ni wanyama? Wale wanaume wanaopita mitaani na kuwafanyia urembo wanawake na kuwapaka rangi kucha ni mijibwa? Amkeni. Mawazo yenu hayo potofu ndiyo yanawarudisha nyuma kimaendeleo kila kukicha. Wewe weka mawazo yako potofu ubaki nyuma kimaendeleo na sisi tunasonga mbele. Kama wewe hujaipenda thread hii ujue haikuhusu na ni bora ukae kimya kuliko kuharibu reputation ya mtu. Wapo wenye shida nayo ambao wataisoma na itawasaidia. Na hii message iwafikie wale wote ambao wanapinga thread zangu.
   
 20. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #20
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  ha ha ha!! Brother..dont take me wrong..mi sipingi wala nini thread zako bana..ujue nimejikuta nacheka tu ghafla,..pole kama nimekukwaza aixee..ha ha!!
   
Loading...