Mambo ya kuzingatia kabla ya kuchagua wazo la biashara

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
20210114_124134_0000.png

Kuchagua wazo la biashara ni jambo la awali na muhimu kulifanya kabla ya kuingia kwenye biashara husika. Hatua hii inahitaji umakini wa hali ya juu kwakua ukikosea hapa kitakachofuata ni kupoteza muda, nishati pamoja na pesa.

Kabla ya kuchagua wazo la biashara itakubidi kuzingatia mambo yafuatayo:-

Chagua wazo unalolipenda;
Kanuni muhimu ya kufanikiwa katika jambo fulani ni kulifanya kwa mapenzi yote, ikiwa unapenda unachokifanya basi utafanya kwa ufanisi na kwa moyo wote hivyo ni wazi kuwa utafanikiwa.

Chagua wazo unalolifahamu na kulimudu;

Usichague wazo kwakua wengine walichagua na kufanikiwa, chagua wazo kwakua unalifahamu vizuri na unalimudu. Kwa mfano usichagua kuuza chakula ikiwa huna ufahamu mzuri wa mapishi.

Zingatia swala la fedha;

Ni lazima uwe na uhakika kuwa una uwezo wa kumudu gharama za biashara unayotaka kufanya. Kukurupuka kutaka kufanya biashara kwakua uliona wengine walipata faida bila kufahamu gharama walizotumia itakugharimu.

Angalia uhitaji wa soko;

Jifunze kuangalia changamoto zilizopo katika eneo unalotaka kufanyia biashara yako hiyo inaweza kukupa wazo zuri la biashara. Kufanya biashara ambayo inatatua changamoto kwenye eneo husika inaweza kuifanya bidhaa yako ikauzika kiurahisi.

Zingatia Ushindani;

Ushindani ni kitu muhimu kwenye biashara kwakua kinaongeza ufanisi na ubunifu zaidi ili kuweza kuteka soko. Lakini pia ni muhimu kujihusisha kwenye ushindani wenye afya kwenye biashara yako, sio sahihi kushindana na makampuni makubwa ambayo yameenea duniani ikiwa wewe bado ni mjasiriamali mdogo.
 
View attachment 1677204

Asante sana kwa kutuwezesha kujua hadhira
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom