VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Tanzania imetajwa kama moja ya nchi zinazoongoza kwa ujangili na hasa biashara ya pembe za ndovu duniani. Sasa inatajwa kama nchi mojawapo hatari kabisa kwa wanyama wa porini duniani.Nchi nyingine ni Kenya na Uganda.Ikumbukwe kuwa Katibu Mkuu wa CCM,Abdurahman Kinana alishutumiwa waziwazi na Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii,Mchungaji Peter Msigwa, kuwa ni kinara wa biashara ya pembe za ndovu. Nchi zilizotajwa kuongoza katika ununuzi wa pembe za ndovu ni China,Thailand,Vietnam,Malaysia na Ufilipino. Nini kifanyike waungwana ili kuwalinda wanyama wetu hasa tembo? Habari kamili ni kwenye Mwananchi la leo uk wa 1 na 4. Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
Last edited by a moderator: