'Mambo ya Kinana' yaipaisha Tanzania!

'Mambo ya Kinana' yaipaisha Tanzania!

Tanzania imetajwa kama moja ya nchi zinazoongoza kwa ujangili na hasa biashara ya pembe za ndovu duniani. Sasa inatajwa kama nchi mojawapo hatari kabisa kwa wanyama wa porini duniani.Nchi nyingine ni Kenya na Uganda.Ikumbukwe kuwa Katibu Mkuu wa CCM,Abdurahman Kinana alishutumiwa waziwazi na Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii,Mchungaji Peter Msigwa, kuwa ni kinara wa biashara ya pembe za ndovu. Nchi zilizotajwa kuongoza katika ununuzi wa pembe za ndovu ni China,Thailand,Vietnam,Malaysia na Ufilipino. Nini kifanyike waungwana ili kuwalinda wanyama wetu hasa tembo? Habari kamili ni kwenye Mwananchi la leo uk wa 1 na 4. Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
Tambua kuwa Msomali hata akiendesha baisikeli atagonga watoto mtaani. Kinana ni hatari kuliko shetani, tuombe mungu atunusuru.
 
Mods,

Naomba mtafute Kinana faster aje jukwaani ajibu baadhi ya maswali ya wanajukwaa.

CC: Kinana aka mzee wa biashara haramu
 
huna unachokijua wala huelewi kitu tukupe pole kwa vile hujui kinachoendelea hapa tanzania.

Sio bure lazima una maslahi katika hili. Nchi na dunia nzima wanaongelea tukio hili katika mtazmo huu wewe hujaona kama ni jambo kubwa!
 
Hii ni hatari, kutoka ndovu milioni 5 mwaka 1950. Mpaka kufikia ndovu lakini nne na nusu (450,000) mwaka 1989. Ni lazima kama Taifa tufanye juhudi za makusudi kuhifadhi hawa wanyama!
 
Kinana si mtu wa kupuuzwa, ni strategist na mchapakazi wa kweli, lazima mhangaike kumchafua kwa salama yenu.

anastafu lini huyu jamaa maana ujangili wake sasa unatisha ck hadi ck kadrii anavyokuwa na madaraka serikalini!!!!! Masikini tembo wetu ni nani atakae watetea
 
Dawa ya kupambana na ujangili ni kuwaondoa hawa viongozi makanjanja....kura yako 2015 itaamua, haiwezekani faru amewekewa gps na kikosi maalum cha kuwalinda halafu wanauawa
 
majangili wanatisha wanauwa na kuchukuwa pembe na kula nyama wenyewe wangechukuwa meno nyama watugawiye angalau tungeshika nafasi ya kwanza kwakula nyama za tembo duniani
 
huna unachokijua wala huelewi kitu tukupe pole kwa vile hujui kinachoendelea hapa tanzania.

Eee bhana umesoma Kata gani Aisee ? Umeelewa kweli ? asiyejua yupi sasa , huyo MZEE TUPATUPA AU GAZETI LA MWANANCHI ?
 
Hivi kinana ana familia ? ( bila shaka ana mke ) , ana Watoto au Ndugu wengine ? Kama wapo wanajisikiaje ? Maana sasa ndiyo siri za Mkubwa zinafumuliwa bila wasiwasi wowote ! Dah ! Nawahurumia sana ndugu zake !
 
Kinana si mtu wa kupuuzwa, ni strategist na mchapakazi wa kweli, lazima mhangaike kumchafua kwa salama yenu.
...Ni kweli hatakiwi kupuuzwa na ana strategies kali. Tangu kuua, kung'oa meno hadi kusafirisha hajakamatwa na wala meli zake hazijataifishwa - badala yake waziri anayetakiwa kumkamata anamtetea. Ni watu wachache sana Tz wenye strategies kali kama za Kinana. namfananisha na Chenge wa rada na Lowasa wa Richmond. CCM wamejaa mastrategists kibao.
 
kwahiyo unataka awemo kwenye list ya mashujaa wa nnji hii sio?

Ikiwezekana kwa vile serikali imekuwa teyari kumsafisha kuliko kumchunguza basi ni bora kumtangaza shujaa kama yule police aliyetukuka
 
Ninachomshukuru Mungu mabaya yote haya iposiku atayafumua na kuwaumbua wote hawa kwani haki na usawa siku zote zitakuwa mbele!
 
Back
Top Bottom