Habari wana JF
Katika pita pita zangu nimekutana na haya wanaume wengi wanalalamikiwa na wanawake au mabinti kuwa tabia zifuatazo zinawakera kwa kuwa nina mapenzi na rafiki zangu JF hasa MMU kama unatatizo kati ya haya baadhi nitakayotaja jirekebishe ni upendo wangu tu kwenu.
- Kutokubali majukumu , mwanaume umeamua kuwa na mpenzi kuwa responsible na take care of your famili kama ukibahatika kupata mtoto. kwa wadada ukiona mwanaume hayupo responsible ukiwa nae jua hadi kitandani ni mvivu wa kutupa ndio wa kwanza kulalama mmh ujui kukata kiuno. Kukiss ujui akilalamika hivyo kaa kimya uone kama anaweza kazi..... utasikia wanawake wanachuna tutaachaje kuchuna wakati kutoa kwa hiyari amtaki mjifunze.
- Kujinunisha hovyo hovyo hivi mwanaume unasusa ili iweje ... he he susa wenzio wala.
- Kuwa mchoyo.. unakuta mwanaume ni mchoyo kiasi kwamba hata kuhudumiana ni tatizo... mwanume pesa yako vitu vyako ni tatizo sasa maana ya mimi kuwa mpenzio au mwili mmoja ni ipi kama unaniwekea demacation kwenye vitu vyako... yani hawa hadi kutoa mawazo ni kazi anaona utafaidi...
- Mwanume mbahili yani hadi anaumwa au unaumwa kutoa hela ya kutosheleza matibabu hato ... yani sasa huyu wimbo wake wa kila siku utasikia sina hela.. hivi kutokuwa na hela ni sifa au ni uvivu basi tuone unafanya jambo la maana upuuzi mtupu
- Mwanume kuendekeza pombe na marafiki yani unatoa kipao mbele rafiki zako kuliko mpenzio ukiona hivyo ujue huna future nzuri.... baadhi ya maandiko yanasema "ajifanyie rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe though rafiki anweza kuwa kama ndugu" tafakari.
- Wivu uliopitiliza hapa wengi ni 25 na 30 sana hawa ndio tatizo utasikia baby tuma picha ... tuma picha unatuma bado tena tuma picha ... hivi niwaulize mnatengenezea movie hizo picha ni nini tatizo?...
muhimu: jitahidini kutafuta pesa kwa bidii na kufanya mazoezi ya viungo. siku njema rafiki