Mambo si shwari tena Tanzania vs USA

Mambo si shwari tena Tanzania vs USA

Binafsi nimechoka na "kwa wahisani ya watu wa marekani", bora ije "kwa hisani ya Urusi" tuachane kabisa na masharti ya kuunga mkono ushoga wa Obama na wenzake. Masuala ya kumegwa kama Apple siyataki kabisa.
 
Jamani hebu nisaidieni... baba Riz amepewa uprof na chuo gani huko china? leo wakati anahutubia huko dodoma TBC wameendelea kumwita Doctor, sasa kama ni prof. na TBC bado wanamwita Doctor hilo sio kosa la jinai aisee?
 
east daima,nani aende west ,unapewa condom kisha masharti kibao.

Hata East wana masharti wewe sema hujui kinachoendelea kati ya viongozi wako na watu wa East. Ulishawahi kupewa mkataba kati ya Tz na China au Tz na Oman ukaona masharti yake?
 
siyo kweli ni maneno ya vilingeni hayana ukweli wowote.
Waziri mkuu hukumsikia analalama BBC kwa nini wamekataa kutoa hela zimekwamishwa na escrow?
 
Mimi nashangaa kitu kimoja pesa ya afya inatoka west, pesa ya barabara inatoka west (MCC) na Japan, pesa ya kuweka umeme vijiji (MCC) masharti ni demokrasia na rushwa tu. China wanatoa mikopo na wanajenga wenyewe hivyo pesa yao inalipwa kwa vitu kutoka china, kwa wafanyakazi wa kichina, kodi inarusi china na sisi tunalipa mkopo hata kama ni wa nafuu pesa yao imeshajilipa. Kama wangekuwa wanatoka mikopo bila kuhimiza wenyewe kujenga na vitu kutoka kwao ingekuwa poa bandari wanajenga wenyewe, bagamoyo wanajenga wenyewe, pipeline ya mtwara wanajenga wenyewe na ndiyo maana hawapendwi na west.
 
viongozi wa tanzania ni wavivu wa kufikiri.

leo hii tunapaswa kuomba teknolojia huko ili zituletee tija,China na Japan hawana uhusiano mzur na China alitawaliwa na Japan,leo hii they are almost the same,China na India walishindana kusomesha vijana wao,leo hii mpaka gas inagundulika ndo vijana wanapelekwa wakasome,too late,hakuna wanasheria wa mambo ya Petroleum hakuna wataalam wa kutosha,sera za elim za China na India ilikua ni HUMAN CAPITAL DEV,kuendelea kuomba misaada uchina ni fedheha,now tunaaminishwa kuwa gas itatuendeleza,lakin nchi inaendelea iwapo kuna rasilimali watu yenye tija(yenye elim na afya bora)
 
safi sana kinuke tu na marekani watugomee hiyo misaada haiwezekani bajeti ya mwaka mzima iliwe na mtu mmoja
 
wote tuna wasiwasi huohuo,kama sio kututwanga kutugombanisha

sure, tena ni bora atutwange, sababu atarusha vikombora viwili vitatu huyu mzembe akikimbia analeta majeshi hapa anany'onga wajinga wawili watatu anasepa.

akitugombanisha, hapatatosha.

sababu utastukia eti Singida kuna wazungu nao wanapigana wao kwa wao

wamarekani wakati mwingine bwana.
 
hali ni mbaya eti eeeeeeh!!!!!.ila njaa zingine bwana!!,ccm mmezidisha umalaya, hivi mnataka muolewe na wanaume wangapi?,sasa mmeona matokeo ya kupenda pesa za wanaume yalivyo mabaya?.marekani na uingereza wanataka kujitoa kwenye hiyo ndoa.cjui itakuwaje jamani???.
duh nilikuwa nimesha log out hapa janvini imebidi nirudi kidogo baada ya kuona hii heading. Ila ikingo acha uoga wa kutopata misaada toka usa na uingereza tunaweza kurudi kwa enzi za mwalimu na tukaheshimika duniani kote.
 
Tatizo nchi yetu ipo uchi kwa hawa jamaa wa west , usidhani waingereza na wamarekani sio corrupt , pengine ni corrupt kuliko viongozi watanzania tofauti tu corruption zao zinafanyika kwa manufaa ya nchi zao na viongozi wanafaidika kupitia wabia wao wa biashara , sisi viongozi wanapiga alafu nchi haifidiki lolote , angalia contracts za BAE na saudi arabia jinsi tony blair alivyoizima , kitendo cha sisi kutegemea misaada kinauma sana , kwani hizi nchi zinatumia kama fimbo ya kufanya tuwasikilize , waingereza ndio wanaongoza kwa uwekezaji Tanzania hata kama hela zao zimepigwa kuna kitu zaidi mi nafikiri ambacho wanakitaka hivi ndivyo nchi za magharibi zinavyofanya kazi ila kama ni corruption kusema ukweli hamna nchi corrupt kama hizi za magharibi , ni kama vile foreign policy ya ufaransa kuendelea kuwa na influence kwenye zile nchi walizotawala , angalia nchi zote wafaransa walizotawala africa shida zilizopitia-congo/ivory coast/congo brazaville/gabon/ nk......ni lazima tujipange kujitegemea wenyewe hawa watu hawana nia ya kutusaidia wala kupigania sijui rushwa afrika au Tanzania kuna kitu wanataka na hii ndio weapon yao
 
sisi sera yetu ni kutofungamana na upande wowote kwahiyo kama marekani akiona nguo imebana aivue asepe mapema kabisa sisi hatuchaguliwi rafiki.

Ni kweli kabisa hata kwenye foreign policy yetu inasema hivyo hatufungamani na upande wowote.
 
hivi mtu akija kukuomba msaada wa hela mara 50, si utamuona kama si chizi ana matatizo yoyote ya akili, sisi tumeomba miaka 50 na hatujui tutaacha lini kuomba tueleweke vipi? maana spidi ya nchi imezidi ya matonya! halafu ombaomba wanaonekana uchafu mjini.
 
Back
Top Bottom