Una macho lakini bado hauoni bora hata yule ambaye ni kipofuwadau wa jf tuwe na utamaduni wa kupongezana pale mtu anapofanya jambo jema, nadhani jk anastahili pongezi kwangu ni mara ya kwanza kuona anatimiza ahadi zake anazozitoa, hivi karibuni mwezi februari alihaidi kuwa ccm itajivua gamba ili kurudisha taswira yake na mvuto kwa jamii na hili limetimia nadhani wansatahili bravoo
bravoo jk bravoooo,
bravo kwa ccm yenyewe kwa kukubali mabadiloko, daima wamekuwa watu wenye mawazo mgando na chama kushikiliwa na misimamo ya wachache lakini kwa sasa angalau wamekubaliana na kelele za magazeti na wananchi
bravoooooo ccm bravoooo
Halafu wameishaota sugu kabisa kiasi kwamba zinatumika kila njia ili wasigusweNdugu zangu uimara wa chama unategemea sana uongozi thabiti wa mwenyekiti wa chama.Hawa wote mliowalazimisha kujiuzulu walikuwa wanafanya hayo walioyafanya kwa baraka za mwenyekiti!...
Kumbukeni msemo wetu wa enzi zile "Zidumu fikra za mwenyekiti"...hii ilitokana na uongozi dhabiti wa Mwalimu Nyerere katika kukiongoza chama mpaka watu wakatamani fikra zake zidumu.John Chiligati ana upeo na uwezo mkubwa tu wa kiuongozi kuliko hata hawa mlioteuwa,..George Mkuchika vilevile na hata Makamba ambaye aliyokuwa anayafanya alijua mwenyekiti wake atayafurahia!...
Ninachosema hapa ni kwamba mlichokifanya mmetoa jasho na wala siyo gamba!..Gamba lenyewe ni mwenyekiti ambaye marafiki zake ambao ni manyangumi ya ufisadi yanakiyumbisha chama huku yeye akitabasamu.
Ndugu zangu uimara wa chama unategemea sana uongozi thabiti wa mwenyekiti wa chama.Hawa wote mliowalazimisha kujiuzulu walikuwa wanafanya hayo walioyafanya kwa baraka za mwenyekiti!...
Kumbukeni msemo wetu wa enzi zile "Zidumu fikra za mwenyekiti"...hii ilitokana na uongozi dhabiti wa Mwalimu Nyerere katika kukiongoza chama mpaka watu wakatamani fikra zake zidumu.John Chiligati ana upeo na uwezo mkubwa tu wa kiuongozi kuliko hata hawa mlioteuwa,..George Mkuchika vilevile na hata Makamba ambaye aliyokuwa anayafanya alijua mwenyekiti wake atayafurahia!... Ninachosema hapa ni kwamba mlichokifanya mmetoa jasho na wala siyo gamba!..Gamba lenyewe ni mwenyekiti ambaye marafiki zake ambao ni manyangumi ya ufisadi yanakiyumbisha chama huku yeye akitabasamu.
Sijui UVCCM watasemaje maana walimuandama sana Nape Nauye
Kwa upande wake, aliyekuwa Naibu Katibu Bara, George Mkuchika, alisema kuwa muundo wa chama kwa sasa utahakikisha kuwa wajumbe wote wanaoingia kwenye sekretarieti wasiwe wabunge wala mawaziri, ili waweze kufanyakazi za chama kwa ukamilifu.
"Safari hii hatutakuwa na kofia mbili. Awali wajumbe wengi walikuwa mawaziri na wabunge, hali ambayo ilisababisha shughuli za chama kusimama," alisema. Hata hivyo, baadhi ya wanachama walikaririwa wakisema kama lengo la chama ni kutenganisha kofia ili kuleta ufanisi, utaratibu huo uwekwe hata kwa rais ili abaki na kofia moja ya urais.
hii itawezekana kweli? tungoje
Umejitahidi sana kumpigia debe kuhusu Mapokezi..Umeahidiwa Cheo? Ningemwona Kikwete ana Busara na ningeandamana Kumpongeza iwapo angeongoza kikao cha kUMVUA UANACHAMA Rostam Aziz na Edward Lowasa.
Lakina kwa Kujiuzulu kwa CC......Hakuna Cha Kupongeza kwani kwa taarifa za ndani ya Kikao KIKWETE alikuwa anataka Makamba na CC yake waendelee hadi Uchaguzi wa Mwakani..Sioni unataka Kumpongeza kwa Lipi Hapa!