Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

wasiishie tu kuwatoa kwenye kamati kuu na kwenye setretarieti wawavue kabisa uanachama na watoswe ubunge. . .halafu wamtose na RA, ooh sorry nimesahau kumtosa RA ni sawa ni kumtosa mwenyekiti, basi yaishe nshaelewa 🙂
 
Labda wabadilishe katiba au waache kumuita WAZIRI MKUU MSTAAFU,
Maana Katiba inasema automatiki MAWAZIRI WAKUU WASTAAF waingia kwenye hizo kamati!

asante kwa angalizo mkuu...unajua humu JF kuna watu wanakurupuka kurupuka tu sijui wakoje...Lowassa anaingia kama waziri mkuu mstaafu(kama wanavomuita wenyewe) sasa nje ya NEC kivipi....by the way JK hana ubavu wa kuamua hayo
 
Mie naamini kabisa kinachoendelea kule Dodoma ni usanii. Kikwete hana ubavu wa kuwafukuza akina Lowassa, Rostam, Chenge na wengineo maana hawa wote wanayajua fika madudu waliyoyafanya na kundi lao la mtandao katika kutafuta mgombea wa CCM mwaka 2005. Rostam ndiye aliyekuwa mweka hazina wa kukusanya mabilioni toka kwa mafisadi mbali mbali wakiwemo wahindi na kisha kuzibadilisha pesa zile toka kwenye za madafu na kuwa dollars au pounds maana wajumbe wengi walionunuliwa ili kumpitisha Kikwete hawakutaka kununuliwa kwa pesa za madafu.

Hivyo kama kweli Lowassa , Rostam na wengineo watafukuzwa na wao kuamua kujibu mapigo ya kumpararura Kikwete basi ndiyo itakuwa ukomo wa Urais wake na si ajabu kusambaratika kwa Chama Cha Mafisadi. Tusubiri tuone kitakachojiri katika kikao hicho kilichojaa usanii.
 
kuna mtu kaiba passworsd ya filed marshal mzee wa sauti ya umeme au labda FM yuko bussy sana
 
Habari za kiintelijensia kutoka dodoma zinasema lowasa katoswa rasmi nec,.na wnegine wanafuatia,.hii nyeti nimeipata kutoka kwa ccm member aliyomo ndani ya hichi kikao cha wanga
Teh teh teh! So lowasa ndio wamesha mtoa msukule.
 
hizo intelligential zako hazitumii mbinu za kisasa; katika hali halisi kumtoa mtu ujumbe wa NEC kuna mlolongo mrefu labda mtu mwenyewe akubali kujihudhuru, jambo ambalo nina uhakika Lowasa hawezi kulihafiki. Katika kukwepa mlolongo huo ndio maana wajumbe wote wa kamati kuu walijihudhuru ili kuwaingiza walengwa kwenye mkumbo huo na hapo baadaye wao warejeshwe.

Nadhani anamaanisha CC
 
Let taarifa sahihi za ukweli kumbukeni hapa si mahala pamchezo kama unaleta taarifa za kupotosha sio tabia ya watu makini na wazalendo kwa taifa na maisha yake yaliobakia mbele yake .nauliza tena Lowassa ametoswa
 
Sahauni kuona waziri yeyote kwenye sekretariati mpya.
 
hizo intelligential zako hazitumii mbinu za kisasa; katika hali halisi kumtoa mtu ujumbe wa NEC kuna mlolongo mrefu labda mtu mwenyewe akubali kujihudhuru, jambo ambalo nina uhakika Lowasa hawezi kulihafiki. Katika kukwepa mlolongo huo ndio maana wajumbe wote wa kamati kuu walijihudhuru ili kuwaingiza walengwa kwenye mkumbo huo na hapo baadaye wao warejeshwe.

Sina tatizo na mchango wako ila una tatizo la kuweka H sehemu ambayo haitakiwi.Hii inapelekea wasomaji kuudharau mchango wako hata kama ni mzuri.May be umesoma english media tangu chekechea hivyo nakushauri utumie kiingereza zaidi na kiswahili utuachie sisi tuliosoma st.kayumbaz
 
Nashangaa kuona baadhi ya yanayoandikwa hapa ni mawazo ya waandikaji lakini si yanayotokea Dodoma. Kuliko kukurupuka kuandika hoja yako binafsi ni bora ukavuta subira kikao kiishe tupate habari iliyoenda shule badala ya udaku
 
Sahauni kuona waziri yeyote kwenye sekretariati mpya.

avatar38074_1.gif.jpg

Duh... kumbe NEC kuna mabwabwa ... teh teh teh
 
Sina tatizo na mchango wako ila una tatizo la kuweka H sehemu ambayo haitakiwi.Hii inapelekea wasomaji kuudharau mchango wako hata kama ni mzuri.May be umesoma english media tangu chekechea hivyo nakushauri utumie kiingereza zaidi na kiswahili utuachie sisi tuliosoma st.kayumbaz

Ni kweli mkuu,uchangiaji unaopotosha lugha mama imekuwa ni tatizo na inaondoa hamasa ya kusoma,tujitahidi kuandika lugha fasaha tunapojadili mada nzitonzito...mawazo ya kila mtu yanaheshimika lakini na lugha pia ieleweke
...wengine hata heading za thread wanakosea na hawataki kuedit,zinabadilisha maana au kusudio la mada
 
Back
Top Bottom