Mambo Makubwa yaliyoondoa credibility ya CHADEMA!

Mambo Makubwa yaliyoondoa credibility ya CHADEMA!

Kijana naona umevimbiwa rambi rambi. Ww mchwa kakojoe ukalale
Jingalao ww
kwa mwendo huu Jingalao na wenzake watatumwa kuhamisha reli ili wapate hela za kufanyia kampen 2020
 
Kule Arusha tunasikia Chadema imechanga kama milioni 50 hivi na wako katika mchakato wa kutoa rambirambi hizo kwa wafiwa huku kukiwa na waandishi wa habari.

Ni huko huko Arusha ambapo mbunge wake ndugu Lema aliahidi kujenga jengo la wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Machinga Complex ahadi ambayo haijatimizwa hadi leo.

Nawashauri hawa matajiri wa rambirambi waelekeze hizo milioni 50 kwenye ujenzi wa Machinga Complex ili kujichukulia ujiko na sio KIKI ZA RAMBIRAMBI.

Chadema Arusha Machinga Complex lini???

[HASHTAG]#kikizamsiba[/HASHTAG]
Afadhari ya hao wanaozifikisha kuliko ccm wanaozitafuna na kuzitafutia matumizi mengine! Hakika ccm ni janga la taifa hili.
 
Kwa hiyo nyie kazi yenu ni kusubiri misiba tu....mara Mwangosi...Mara ...Mawazo ...na leo kwa watoto yaani hamasa yenu ni kwenye mazishi tu...tekelezeni ahadu yenu ya Machinga Complex achaneni na michango ya vifo tu.
Naona avatar yako ina akisi kilichomo kichwani mwako! Kweli wewe ni jingalao
 
Na mimi siwaoni wala siwasikii
January Makamba
Ole Sedeka
Abdurahman Kinana
Mwingulu Nchemba
Rizwan Kikwete
Nchimbi
Kabla huja angalia chadema anza na wa Lumumba.


Ndukiiiii
Nadhani utakuwa umewasikia sasa
 
kiki ya msiba imebuma kudadadeki
 
Ding Ding Dong...keep ya head ringing!
 
Nimehangaika sana kutafuta point kwenye Article yako waaaalllllah sijaona.

Andika maelezo mapya

Huwezi kuona chochote katika points alizojitahidi kuweka. Zipo nyingi zaidi ambazo nadhani kahifadhi. Sisi ambao tulikuwa chadema tangu mwaka 1994 mpaka tuna achana na Chama cha Mbowe 2017, tunajuwa tofauti ya Chadema iliyopita na CHADOMO ya leo.

Na wanaenda kupotea kama vyama vingine vilivyopotea baada ya uchaguzi 2020. Tumefikia kutembeza bakuli viwanjani wakati tulikuwa tunachangisha kwenye mahoteli makubwa.

Tulikuwa tunajaza viwanja kama mwembe Yanga -Temeke, leo hii hata Segerea shule ya msingi viwanja havijai, na tunawadanganya Watanzania ati tuna wana chama kila kitongoji, AIBU KUBWA HII.
 
Huwezi kuona chochote katika points alizojitahidi kuweka. Zipo nyingi zaidi ambazo nadhani kahifadhi. Sisi ambao tulikuwa chadema tangu mwaka 1994 mpaka tuna achana na Chama cha Mbowe 2017, tunajuwa tofauti ya Chadema iliyopita na CHADOMO ya leo.

Na wanaenda kupotea kama vyama vingine vilivyopotea baada ya uchaguzi 2020. Tumefikia kutembeza bakuli viwanjani wakati tulikuwa tunachangisha kwenye mahoteli makubwa.

Tulikuwa tunajaza viwanja kama mwembe Yanga -Temeke, leo hii hata Segerea shule ya msingi viwanja havijai, na tunawadanganya Watanzania ati tuna wana chama kila kitongoji, AIBU KUBWA HII.
mwaka huu sijawaona wakienda serena...watasingizia corona
 
Habari zenu wadau!

Niende kwenye mada moja kwa moja...

Inasemekana kuwa Chadema ni moja ya Chama ambacho kilipoanzishwa kiliogopewa sana hata na hayati mwalimu Nyerere.

Kuogopwa huku kulitokana na katiba na mikakati iliyojiwekea kipindi kile wakati inaanzishwa.

Ni vyema sisi wadau wa siasa za Tanzania tukajadili kwa nini Chadema imeangukia kwenye kapu lile lile la vyama laghai vya kisiasa nchini ?

Yafuatayo ni mambo makubwa ambayo sio propaganda yaliyoifanya Chadema kuwa au kuangukia kwenye vyama vya siasa ambavyo ni uchwara.

1- Chadema kushindwa kuonesha utofauti kwenye halmashauri au majimbo iliyoyashika.hapa naongelea majimbo ya moshimjini,Tarime na Karatu.
sana sana moshi mjini na hasa karatu ambapo imegeuka kuwa halmashauri ya kifisadi kuliko zote kwa mujibu wa CAG.
Ukiacha ufisadi ...bado hatujashuhudia utofauti wa kimaendeleo katika halnashauri hizi pamoja na kushikiliwa na Chadema ambao walijinadi kuwa ni mahiri katika maendeleo na udhibiti!

2-Kumpokea lowasa na kumfanya mgombea uraisi bila kufuata taratibu za chama.hili lilliwafanya waonekane kuwa ni chama kichanga kinachotegemea CCM wagombane ili wapate mgombea uraisi.

3-Kuachana na vita ya ufisadi,ubadhirifu,uzembe na ukwepaji kodi.
Baada ya kumuweka mgombea urais mwenye tuhuma nyingi za ufisadi na ubadhirifu Chadema ilipoteza uaminifu kutoka kwa jamii inayojitambua!
Baada ya kumuweka mtu waliyemtukana kwa miaka zaidi ya mitano kuwa mgombra urais basi kila anayejitambua aliwapa mkono wa kwa heri.

4-Ugomvi na Dr Slaa
Huyu alikuwa ni think tank na mtendaji wa kipekee ndani ya Chadema.Kushindwa kumshawishi abaki ndani ya Chadema pamoja na kupiga goa za anga lilikuwa ni kosa kubwa sana

5- Kutetea yale waliyokuwa wanayapinga na kuyapigia kelele
Hapa wananchi na wasomo wanaojitambua wamechanganywa vilivyo baada ya kuwaona Chadema wakitetea ufisadi,uzembe kazini na hesitationa ya kuchukua hatua.yaani chadema ina-sympathise na wakwepa kodi waliopelekwa mahakamani na wafanyakazi wazembe waliotumbuliwa.

6-Uteuzi wa nafasi ndani na nje ya Chama.Hapa malalamiko yapo kwenye uteuzi wa wabunge wa viti maalum ambao haujazingatia weledi au uzoefu ndani ya chama.wapambanajoi wanapigwa chini halafu ndugu na vimada wanapewa nafasi.

Haya ni machache tu kati ya mengi makubwa ambayo yanaoangusha Chadema na kuifanya kuwa CCM ile ya zamani (sio hii ya Magufuli)iliyochikiwa na wananchi.

Haya ni maoni ya Mwanachadema asilia niliyeongea naye..!

Ukiwa na sababu zaidi ya hizi share with us!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Hakuna uchaguzi huru ni wizi mtupu CCM inaongoza Nchi pasipo idhini ridhaa ya wapiga kura, sasa CCM imesimikwa na NECCCM Tumeccm na Polisiccm kwa njia haramu za kishetani hakuna mwananchi mwenye Akili timamu kaipigia CCM kura
 
Hakuna uchaguzi huru ni wizi mtupu CCM inaongoza Nchi pasipo idhini ridhaa ya wapiga kura, sasa CCM imesimikwa na NECCCM Tumeccm na Polisiccm kwa njia haramu za kishetani hakuna mwananchi mwenye Akili timamu kaipigia CCM kura
Hata mawakala mmekosa
 
Back
Top Bottom