Mambo haya yakifanywa uchumi na maisha ya Watanzania yatakimbia 2020-2025

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
946
MAMBO HAYA YAKIFANYWA UCHUMI NA MAISHA YA WATANZANIA YATAKIMBIA 2020-2025

Habarini waheshimiwa.

Ebwana bila kupoteza muda kuna vitu vichache naona nishare hapa,unaweza kuongezea kama kuna kitu cha kuboresha. Naomba moja kwa moja niende kwenye vitu Vinne(4)Vinavyoweza kugusa na kuinua taifa letu kwenda kule tunakohitaji.

1. KUTENGENEZA MIFUMO YA UMWAGILIAJI VIJIJINI
Sote tumekuwa tunajua kwamba taifa linategemea mvua ili kufanya uzalishaji lakini kama tuna malengo ya dhati ya kututoa hapa kutupeleka nchi zenye uchumi wa kati tunatakiwa kuboresha kilimo na kuachana na jembe la mkono twende kwenye kilimo cha uhakika ambacho ni mwaka mzima tutakuwa tunalima hivyo ni vema kila kijiji sasa tungefikiria kukipelekea mfumo wa umwagiliaji. Ni muhimu kwasababu sekta hii inategemewa na wananchi wengi zaidi. Kama umeme inaelekea kufanikiwa hii nayo inawezekana, hapa ukiboresha unakuwa umewagusa na kuwainua wengi sana.

2. KUJENGA RELI YA MTWARA- MCHUCHUMA
Naamini viwanda vya Chuma nchini vitasababisha ujenzi wa viwanda haraka zaidi kwani utengenezaji wa vitu vingi hususani magari,mashine na vingine unategemea chuma.Sasa miundombinu ikiwa imara vikajengwa viwanda hapa vya chuma ni rahisi kuanzisha viwanda vingine kutegemea bidhaa hiyo ambayo hapa ipo kwa wingi tena ukizingatia chuma hiki kinaweza kuchimbwa miaka zaidi ya 100.

Niliwahi kuambiwa mjerumani alishasurvey na kuweka ramani yake ya kusafirisha chuma hiki mpaka Mtwara kutoka mchuchuma.Tutaweza kupata bisdhaa nyingi zinazotokana na chuma kwani viwanda vya Chuma vitakuwa hapahapa hivyo kupunguza gharama ya upatikanaji wa bidhaa hii na kufanya iwe rahisi zaidi.Kwani kuagiza nje kunaliongezea taifa gharama kubwa zaidi

3. MASOKO
Kama nchi itaboresha mifumo ya kilimo,biashara na viwanda ni wazi bidhaa zitahitahi soko hivyo serikali ingesaidia kuboresha na kutafuta masoko kwa za nje.

Tunaona leo mahindi yaliyokuwa bei ya chini kabisa wananchi wameanza kuyakimbilia kulima kwa wingi lakini hii yote ni sababu ya soko la nje linaloonekana la nje kuwekwa vizuri. Lakini kuna nchi nyingi Ulaya zinahitaji Mbogamboga na matunda pamoja na mazao mengine. Tukiboresha miundombinu ya kilimo tujue wazi itabidi kupanua soko zaidi kuliko hata tulivyo sasa.

4. Kuboresha Mifumo Ya Biashara na kuangalia changamoto zinazowakuta Wafanyabiashara na Wajasiriamali wengi huanza na biashara zao hufa.Kwani tukiweza kupunguza biashara zinazokufa tutaongeza pato na kuongeza fursa ya ajira na kukuza sekta nyingine.

0766875334
 
Back
Top Bottom