Dr am 4 real PhD
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 6,469
- 11,912
Mama yangu angefikiria nini?"
"Katika mbio, (angalia picha), mwanariadha Abel Mutai anayewakilisha Kenya, alikuwa miguu michache kukata utepe kumaliza mbio AKIWA mshindi wa kwanza, lakini gafla aligafirika na kushindwa kutambua sign na aliacha kufikiria alikuwa anamaliza mbio hizo.
Mwanariadha wa Uhispania, Ivan Fernandez alikuwa nyuma yake na kugundua kile kilichokuwa kikiendelea, akaanza kupiga kelele kwa Mkenya ili aendelee kukimbia kuelekea kumaliza mbio izo AKIWA mshindi wakwanza, lakini Mutai hakujua Kihispania hakuelewa. Ili mbidi Mhispania huyo kumsukuma mkenya kwa nyuma ili kumsaidia aibuke na ushindi.
Mwandishi wa habari akamwuliza Ivan, "Kwanini alifanya hivyo? "Hivyo?"
Ivan akajibu, "Ndoto yangu ni kwamba siku moja tunaweza kuwa na aina ya maisha ya "Community life".
Mwandishi wa habari alisisitiza "Lakini kwanini umwachie Mkenya kushinda?" Ivan akajibu, "Sikuweza kumshinda, alikuwa atashinda". Mwandishi wa habari alisisitiza tena, "Lakini ungeshinda!" Ivan alimtazama na akamjibu,
"But what will be my victory? Is it What will the honor of that medal be?
Mama yangu angefikiria nini? "
Tumerithishwa Mila na desturi mbali mbali kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine. Je! Tunawafundisha watoto wetu maadili gani? Kitu kikubwa tusifundishe watoto wetu njia mbaya na ovu ilimradi tu kuupata ushindi "
Wasalaam,