Wema bado wapo

Wema bado wapo

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
370,426
Reaction score
857,699
Mwanariadha wa Kenya Abel Mutai alikuwa karibu na mstari wa kumaliza mbio, akachanganya alama za kumaliza mbio na kusimama akifikiri ameshaliza na ni mshindi, ingawa hakuwa amevuka mstari ili kuwa mshindi wa kwanza, mita kumi kabla ya finish line. Mwanariadha wa Hispania Ivan Fernandez alikuwa nyuma yake na akagundua Mutai amechanganya na kusimama kabla va kuvuka mstari wa ushindi.

Angempita na kuvuka mstari ili awe wa kwanza? Aliamua kumkumbusha bado hajavuka mstari wa ushindi na kumtaka amalize, akimwambia kwa Kihispania ambacho Mutai hakuwa anaelewa hivyo alitumia nguvu ya ziada hadi kumsukuma avuke mtari ndio afuate yeye katika nafasi ya pili.Fernandez alimpelekea Mutai kumaliza mbio zile na kuwa wa kwanza na yeye wa pili.

Alipoulizwa kwa nini alimsadia Mutai na yeye akawa wa pili licha ya kuwa na nafasi ya kuwa wa kwanza akasema "Ndoto yangu ni siku moja kuwa na maisha kwenye jamii inayoweza kusaidiana na kusukuma kwenye mafanikio" "Sijamfanya ashinde, hizi zilikuwa mbio zake, alistahili kushinda yeye kwani alikuwa na nafasi ya kufanya hivyo" "Nini faida ya ushindi huu? Heshima ya medali hiyo itakuwa wapi? Mama yangu atanichukulia vipi?"

"Wengi wetu tunajinufaisha na madhaifu ya wenzetu badala ya kuchukua nafasi hiyo kuwapa nguvu na kuwafanya kuwa Bora" Hii ilitokea kwenye mbio za Burlada, Hispania mwaka 2012. Ivan hakushinda mbio hizo kuwa wa kwanza lakini alishinda mioyo ya wengi. Angeshinda huenda asingekumbukwa kama anavyokumbukwa kwa alichokifanya kwa Mutai. Watu wema hawajaisha, tenda wema!
FB_IMG_1694680947748.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania ukitaka watu wakuite ''yule aliyezubaa'', basi uwe mwema. Na ukiwa laghai lghai utasikia ''yule mjanja mjanja''
Mwajiriwa wa umma anayemiliki mali nyingi zaidi ya kile cha halali anaitwa mjanja.

Mwajiriwa wa umma anayemiliki kile cha halali tuu na anayeonekana kutokuwa na mali anaitwa fala.

Mwizi/fisadi/tapeli ndiye anaheshimika.

Muaminifu/Mcha Mungu/raia mwema /muadilifu anatukanwa na kudharaulika.

Tanzania imekuwa na watu wa hovyo kuliko choo cha stand.
 
Mwajiriwa wa umma anayemiliki mali nyingi zaidi ya kile cha halali anaitwa mjanja.

Mwajiriwa wa umma anayemiliki kile cha halali tuu na anayeonekana kutokuwa na mali anaitwa fala.

Mwizi/fisadi/tapeli ndiye anaheshimika.

Muaminifu/Mcha Mungu/raia mwema /muadilifu anatukanwa na kudharaulika.

Tanzania imekuwa na watu wa hovyo kuliko choo cha stand.
Tanzania imekuwa na watu wa hovyo kuliko choo cha stand[emoji3064][emoji3064][emoji3064]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom