Mama yangu adui yangu

Mama yangu adui yangu

Jamani nimeishiwa na nguvu mwaija alivyomwamBia mama yake. Ameconceive,laiti angejua mama yake ni mwanga


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
aaaahh!! mbona ya leo fupi sana??? dah!! haya Mzizi wewe umeshika penye mpini sie kwenye makali ujanja hatuna, tutasubiria tena.
 
MAMA YANGU ADUI YANGU -33-


Hata baada ya kuacha kazi bado aliendelea kupata usumbufu kutoka kwa Emma kwa kupigiwa simu bila kuzingatia alikuwa na nani. Pia, alikuwa

akimtumia ujumbe wa vitisho kitu kilichosababisha abadilishe namba yake ya simu ambayo hata miye sikuwa nayo.


Taarifa hizo nakumbuka nilipewa na mmoja wa wasichana tuliyekuwa tukifanya naye kazi.


Kwa kipindi kile sikuwa na shida naye kwa vile nilijua ana namba yangu lazima angenipigia na kunipa michapo yote.

Niliamini alichokifanya kilikuwa na masilahi kwake.

Dereva alipofika alinichukua na kunipeleka hospitali. Tulipowasili tuliwakuta wagonjwa wengi, nilisubiri kwa saa nzima ndipo nilipata nafasi ya kuonana na dokta Hindu.

SASA ENDELEA...


“Mwaija usione nimekuweka shoga yangu, nilitaka niwapunguze watu ili nipate nafasi nzuri ya kuzungumza na wewe kwa kina.”
“Hakuna tatizo shoga yangu.”
Sikuwa na maelezo mengine ya kumueleza zaidi ya yale niliyomwambia kwenye simu. Baada ya kuniuliza maswali alinifanyia vipimo vyote kisha alipima ujauzito wangu na kukuta kila kitu kikiwa sawa.
“Mmh! Sasa hiki kitakuwa nini?” dokta Hindu alishtuka.
“Hata najua!”
“Kila kitu kinaonesha kipo sawa, ujauzito pia uko sawa, inawezekana ni hali ya kawaida ambayo haiathiri kitu.”
“Nina wasiwasi hali hii inaweza kuendelea.”
“Mmh! Sidhani kwa vile nimecheki hakuna dalili zozote za damu kuendelea kutoka.”
“Mmh! Ilinitisha sana.”
“Ondoa wasiwasi ujauzito wako upo sawa hata viungo vya karibu na mfuko wa uzazi vipo sawa.”
Baada ya kuona hakuna tatizo nilirudi nyumbani kidogo moyo wangu ulikuwa umetulia. Wazo la kumwambia mama nilikuwa nalo lakini kutokana na maelezo ya daktari niliamini huenda damu iliyotoka usiku wa kuamkia siku ile ilikuwa ya mwisho.
Nilirudi nyumba na kujipumzisha huku msichana wangu wa kazi akitaka kujua majibu ya hospitali.
“Vipi dada za huko?”
“Mmh! Nzuri, majibu ni yaleyale.”
“Unamaanisha nini?”
“Hakuna tatizo.”
“Sasa na hizo damu?”
“Inaonekana zimekata.”
“Ooh! Afadhali yaani hata mimi nilikuwa na wasiwasi sana.”
“Nashukuru kuguswa na matatizo yangu.”
“Yaani dada wewe kama Mungu wangu.”
“Aah! Hapana siwezi kuwa Mungu wako.”
“Kweli dada umeniokoa kwenye mateso.”
“Pamoja na hilo, lakini nitabakia kuwa mwanadamu wa kawaida,” pamoja na wema wangu niliamini siwezi kufikia hata robo ya utukufu wa mitume nini Mungu!
“Basi wewe ni mtu muhimu sana kwangu.”
“Hapo sawa.”
Kwa vile alikuwa ameniandalia juisi alinipatia na kunywa kisha nilijipumzisha. Siku ile nilishinda katika hali nzuri japokuwa wasiwasi wangu ulikuwa ni kuumwa na tumbo, lakini hali ile haikujitokeza mpaka jioni ilipoingia.
Usiku ulipofika nililala vizuri mpaka siku ya pili. Nilipoamka cha kwanza kilikuwa kuangalia nguo ya ndani ambayo nilishangaa kuikuta ikiwa safi. Nilijichunguza na kujiona nilikuwa sawa, nilikwenda kuoga na kuisikilizia ile hali ambayo pia siku ilikatika nikiwa sawa. Mchana wa siku ile dokta Hindu alinipigia simu kutaka kujua maendeleo ya hali yangu nikamjulisha kwamba nilikuwa nikiendelea vizuri.
Sikujiamini moja kwa moja niliendelea kuisikilizia hali ile kwa siku tatu bila kuona mabadiliko.
Wiki ilipokatika bila kuiona damu, niliamini kuwa nimepona na tatizo lile limeisha.
Baada ya wiki ya pili kukatika nikiwa katika hali nzuri, niliamini naweza kukutana kimwili na mpenzi wangu.
Kama kawaida siku hiyo alikuja jioni kabla ya kuondoka nilimuomba akidhi haja zangu.
Japokuwa alitaka tuendelee kusubiri mpaka mwezi ukatike lakini nilimhakikishia kwamba nilikuwa sawa. Alinikubalia na tukakutana, safari ya kwanza tulienda vizuri.
Safari ya pili tukiwa katikati ya tendo nilihisi tumbo likivurugika kama vile nilikuwa nikitaka kuhara na nikamuomba mzee Sambi anyanyuke kwanza.
“Samahani mpenzi hebu toka.”
“Kuna nini?”
“Tumbo limenivurugika ghafla.”
Aliponyanyuka nilihisi kama nimeshikwa na haja ndogo. Nilikimbilia msalani na kuchutama na kusukuma kwa nguvu.
Ajabu haja ndogo iligoma kutoka lakini maumivu ya kutaka kujisaidia yalikuwa makali.
Niliendelea kulazimisha kusukuma huku mvurugano tumboni ukiwa mkubwa. Niliamini lile ni tumbo la kuhara, niliendelea kusukuma haja kubwa ambayo niliamini lazima nitaharisha kutokana na tumbo lilivyokuwa likinivuruga.
Lakini baada ya kujikamua sana nilitoa kinyesi kidogo kama cha mbuzi na kunishangaza, tumbo lilivyokuwa likinivuruga kutoa kinyesi kama kile wakati nilijua nitaharisha.
Niliendelea kujikamua huku haja ndogo ikiuma lakini iligoma kutoka. Niliendelea kujikamua huku maumivu chini ya kitovu yakiwa makali sana.
Nilijiuliza kile ni nini? Nilijuta kulazimisha kufanya mapenzi, japokuwa hayakuwa ya nguvu zaidi ya kufanya kwa tahadhari kubwa.
Mzee Sambi alinifuata msalani baada ya kuniona nimechelewa kutoka na kuniuliza:
“Vipi mpenzi?”
“Yaani hii hali wala siielewi.”
“Kwa nini?”
“Haja ndogo imenishika mpaka kinena kinauma lakini haitoki. Tumbo nalo limevurugika lakini choo hakitoki hata sijui...yaani mbona nateseka mtoto wa kike,” nilisema huku nikiuma meno kwa uchungu.
“Sasa itakuwa nini! Au twende hospitali?”
“Su...su...mmh,” nilisema huku nikiuma meno na kusukuma kwa nguvu baada ya kusikia kama kitu kikisogea mithili ya mtu anayejifungua.
Niliuma meno na kusukuma kwa nguvu zote. Mara kitu kilifyatuka kwa mbele na kufuatiwa na damu nyingi nyeusi.
Niliendelea kujikamua, damu iliendelea kutoka ikiwa mabongemabonge na kufika robo ya sinki la choo.
Ilikuwa damu nyeusi iliyokuwa ikinuka kama kitu kilichokuwa kimeoza.
Wakati huo nilianza kuharisha mfululizo kitu kilichonifanya niishiwe na nguvu na kuanguka msalani.
***
Niliposhtuka nilijikuta nikiwa hospitali, niliponyanyua macho niliwaona watu kwa shida, macho yangu yalikuwa kama yana ukungu.

Hata hivyo, nilibaini kwamba kulikuwa na watu waliokuwa wamejazana kitandani kwangu huku nikiongezewa damu.

Uwezo wa kuona vizuri sikuwa nao kwa vile nilipojitahidi kutizama vizuri niliona kitanda kikizunguka na kunifanya nifumbe macho, nilikuwa nimeshikwa na kizunguzungu kikali.
Niliisikia sauti ya mama ikiniita:
“Mwaija...Mwaija.”
Nilimsikia lakini sikuwa na uwezo wa kufumbua mdomo japokuwa nilijitahidi kuitikia. Nilikuwa najisikia vibaya na kizunguzungu kilikuwa kikali sana.
Nilitulia nikiwa nimefumba macho, kizunguzungu nacho kilipungua taratibu na usingizi ulinipitia.
Niliposhtuka nilijikuta nikiwa kitandani na mama na dada zangu walikuwa pembeni wakionesha kuwa na nyuso zenye huzuni.
Mara aliingia daktari na kusogea kitandani kwangu.
“Mwaija,” aliniita kwa sauti ya upole.
“Abee,” safari hii sauti ilitoka.
“Unajisikiaje?”
“Kizunguzungu.”
“Kitaisha tu, damu uliyopoteza ilikuwa nyingi.”
“Damu!?” Nilishtuka.
“Ndiyo, ulikuja ukiwa na hali mbaya sana, mpaka sasa hivi unazungumza kweli Mungu mkubwa.”

Itaendelea Jumamosi ijayo ....
 
Tatizo hakuzingatia ushauri wa mganga wake wa jadi.
Kipindi kanasa ujauzito alikosa muda wa kwenda kwa mganga kwa kuwa umetoka hapo muda utapatikana!.

Hayo ndiyo matatizo yetu wanadamu kujisahau.
 
duuuhhhh..
Bora angerudi tu kwa yule mganga wake .
hakufuata masharti. aliambiwa arudi baada ya
kupata ujauzito.

Kwa mganga ukienda lazima ufuate masharti au usiende kabisa.
 
MAMA YANGU ADUI YANGU -34-


ILIPOISHIA:
Nilitulia nikiwa nimefumba macho, kizunguzungu nacho kilipungua taratibu na usingizi ukanipitia.
Niliposhtuka nilijikuta nikiwa kitandani na mama na dada zangu walikuwa pembeni wakionesha nyuso za huzuni.
Mara aliingia daktari na kusogea hadi kitandani kwangu. “Mwaija,” aliniita kwa sauti ya upole. “Abee,” safari hii sauti ilitoka.
“Unajisikiaje?” “Kizunguzungu.” “Kitaisha tu, damu uliyopoteza ilikuwa nyingi.” “Damu!?” Nilishtuka. “Ndiyo, ulikuja ukiwa na hali mbaya sana, mpaka sasa hivi
unazungumza Mungu mkubwa.”
SASA ENDELEA...

“Mimba yangu ipo salama?” lilikuwa swali lililonitoka kinywani kwangu, kwani haikuwa tofauti na tukio la awali la kuharibika mimba yangu.” “Bado tunaangalia kwanza hali yako, mengine ata baadaye.” “Mama,” nilimwita mama aliyekuwa amesimama

pembeni ya kitandani. “Abee mwanangu unaendeleaje?” “Kizungumzungu, lakini kwa sasa afadhali kidogo.” “Pole.” “Asante mama.” “Pole Mwaija,” dada zangu nao walinipa pole. “Asante.” Kuna kitu kimoja nilikigundua katika nyuso za mama na dada

zangu. Walionekana wamevimba macho kuonesha kama walikuwa wakilia.


“Mama,” nilimwita kwa kujilazimisha. “Abee mama.” “Mbona kama wote mlikuwa mkilia?” nilimuuliza mama. “Mmh! Wee acha tu

kweli Mungu mkubwa.” “Kwa nini mama?” “Sikuamini kama ungeweza kuzungumza hivi.” “Kwa nini?” “Hali tuliyokukutana nayo

ilituchanganya, mimi ndiye kidogo niliyejitahidi lakini dada zako walipokuona waliangua vilio. Hatukuamini kama utapona.” “Kwani

ilikuwaje?” “Tulipigiwa simu na bwana yako akilia, huwezi kuamini tulivyoondoka nyumbani ndivyo tulivyokuwa, hakuna aliyekumbuka viatu wala khanga ya kujifunga juu.


“Tulikukuta umelazwa sebuleni damu chapachapa huko msalani ndiyo usiombe utafikiri kumechinjwa ng’ombe na harufu kali kama kuna kitu kimeoza.” “Mungu wangu, ujauzito wangu


upo salama?” “Hatujajua, huwezi kuamini mimi na dada yako mkubwa tuna siku ya pili tupo hospitali hatujarudi nyumbani.” “Kwa nini mama?” nilishtuka kwani niliamini tukio lile lilikuwa la siku ileile. “Kwa hali uliyokuwa nayo tulijua umefariki kwani hata mapigo

ya moyo yalionesha kusimama. Pamoja na kuelezwa turudi nyumbani hatukukubali. Tulilala nje ya hospitali kwa siku mbili mpaka ulipofumbua macho lakini hukuweza kuzungumza. “ Lakini tulielezwa kwamba damu waliyokuwekea ungeweza kurudi katika hali

yako ya kawaida. “Damu uliyopoteza ni nyingi sana. Yaani tungechelewa kidogo tungekupoteza kwani ulikuwa umeishiwa damu kabisa mwilini, kwani tatizo nini mwanangu?” mama aliniuliza akiwa ameniinamia. Nilijitahidi kuelezea hali yangu tangu siku ya

kwanza na siku ile nilipotokewa na tatizo lile. “Mmh!” waliguna wote. “Kwa nini ulikaa kimya?” dada mkubwa aliniuliza. “Nilijua labda ni hali ya kawaida kwa vile sikuwa na maumivu yoyote.” Kuguna kwao kulinishtua na kujiuliza kulikoni kuguna wote kwa

mpigo. Nilichowaeleza mbona kilionekana kuwashtua na kutazamana wote. “Jamani kuna nini?” niliuliza baada ya kuingiwa na hali ya woga. “Mwaija hebu kwanza tuangalie tiba za hospitali.” “Kwa nini unasema hivyo mama?” “Kauli yako imenitisha mtu kupatwa

na tatizo baada ya kukutana na mwenzio. Pia hata yule mwanamke nina imani hakuwa mwema kwako.” Kauli ya mama ilinishtua na kunifanya nijiulize inamaa aliyekuja alikuwa mke wa mzee Sambi na kama ni yeye mbona hakuniambia ukweli. Nilikubaliana na kauli ya mama kutokana na mshtuko alioupata mzee Sambi juu ya ugeni ule baada ya kuufahamu wajihi wa mke wake. “Kwani

mama aliyekuja si mwenye nyumba?” “Tutajua tu kama amri ya Mungu au mkono wa mtu.” Jioni alipokuja mzee Sambi kuniona alionesha uso wa furaha baada ya kunikuta nikiwa katika hali nzuri. Niliamini siku mbili nilizokuwa sina fahamu zilimchanganya sana.

“Karibu mpenzi,” nilimkaribisha.“Asante, pole sana.”“Asante.”“Vipi unaendeleaje?” “Sijambo.” “Vipi umekula?” “Ndiyo.” Baada ya muda mama na dada zangu walitoka nje na kuniacha na mzee Sambi. Niliamini ile ndiyo ilikuwa nafasi yangu ya kupata ukweli

kama aliyekuja siku ile alikuwa nani. “Eti mpenzi aliyekuja siku ile alikuwa mkeo?” “Mbona unauliza hivyo?” “Nijibu swali langu,” nilikuwa mkali kidogo. “Ndiyo.” “Ndiyo nini?” “Ni mke wangu kweli.” “Mzee Sambi, mkeo alikuja kwangu kufanya nini?” “Sijui.” Itaendelea Akhamisi ijayo......
 
[h=1]MAMA YANGU ADUI YANGU -35-[/h]
ILIPOISHIA:
"Eti mpenzi aliyekuja siku ile alikuwa mkeo?"
"Mbona unauliza hivyo?"
"Nijibu swali langu," nilikuwa mkali kidogo.
"Ndiyo."
"Ndiyo nini?"
"Ni mke wangu kweli."
"Mzee Sambi, mkeo alikuja kwangu kufanya nini?"
"Sijui."
"Amepajuaje?"
"Hata mimi nashangaa."
"Na kwa nini ulinificha ukanidanganya?"
"Nilihofia kukushtua kwa vile nilikwenda nyumbani tukayamaliza."
SASA ENDELEA...


"Huu ugonjwa wangu nina wasiwasi na mkeo."
"Kafanya nini?"
"Nitajua tu, ila kama ni yeye nitakufa naye."
"Hawezi kufanya mchezo wowote mchafu."
"We mtetee labda nife."
"Mpenzi usiwe na mawazo potofu, kwa vile upo hospitali ngoja tuone kitakachoendelea."
Siku ya pili niliamka nikiwa na nguvu na chupa za damu nilizoongezwa ziliisha na kujiona nikiwa sawa. Nilichotaka kujua ni kuhusu

ujauzito wangu. Majibu ya vipimo yalipatikana jioni ya siku ile baada ya mzee Sambi kuja.
Vipimo vilionesha ujauzito wangu umetoka. Baada ya kupewa taarifa ile nilipata mshtuko uliosababisha nipoteze fahamu.
Baada ya kurudiwa na fahamu na kukumbuka kilichonitokea nililia sana. Niliamini siku ile kama ningekuwa ghorofani basi

ningejitupa au kama kungekuwa na sumu karibu yangu ningekunywa.
Roho iliniuma kama kidonda na kujiuliza hali ile itaendelea mpaka lini.
Nilijiuliza ule ndiyo utakuwa mchezo wa kushika ujauzito na kutoka katika maisha yangu?
Taarifa za kupoteza ujauzito wangu zilimliza mzee Sambi kama mtoto.
Kwa kweli lilikuwa pigo lingine kubwa maishani mwangu. Tangu siku niliyopewa taarifa ya kuharibika kwa ujauzito wangu

mwingine, chakula kilikataa kupita mdomoni japokuwa mama na dada zangu walinilazimisha nile angalau kidogo.
Siku nne kwangu zilikuwa sawa na mwezi mzima kwa mawazo na kushindwa kula, kutokana na kufikiria mateso yanayonipata ya

kupoteza ujauzito wangu kila mara.
Nilikonda kama niliugua kwa muda mrefu. Mama na dada zangu walitumia muda mwingi kuwa karibu yangu huku

wakinibembeleza angalau nile kidogo, lakini wapi chakula kilikataa kupita mdomoni, muda mwingi nilikuwa nikilia tu.
Kingine kilichoniumiza akili kilikuwa ni maumivu ya tumbo na kuendelea kutoka damu kama ya hedhi kwa muda mrefu. Nilikuwa

nashinda na pedi ili nisijichafue.
Ugonjwa wa tumbo ukanitia wasiwasi labda sikusafishwa vizuri. Ilibidi nifanyiwe usafi upya.
Nilimshukuru Mungu kidogo hali ya maumivu ya tumbo ilitulia na kuamini maumivu yale yalisababishwa na uchafu uliobaki.
Kuendelea kutokwa na damu kulinichanganya sana japokuwa haikutoka nyingi lakini bado nilibakia na swali kwa nini iendelee

kutoka.
Nilifanya vipimo vyote lakini haukuonekana ugonjwa wowote. Nilianza kuingiwa na wasiwasi yale ni mambo ya Kiswahili au

kishirikina. Kila kukicha hali yangu ilizidi kubadilika, nikawa siwezi kunyanyuka.
Nikawa mtu wa kulala kitandani, miguu ilikuwa kama vile imepooza. Kutokana kukosa ufumbuzi wa ugonjwa wangu, daktari

mmoja alimshauri mama tuhangaike upande wa pili.
Ilibidi nitolewe hospitali, ungeniona siku ile ungelia kwa uchungu. Nilikuwa nimekwisha kama mgonjwa wa kifua kikuu. Mama

alinichukua na kunipeleka kwa mtaalamu Temeke Yombo.
Mwaija miye nilikuwa wa kubebwa kama mtoto mdogo, sura yangu kwa muda mfupi ilibadilika na kuwa kama mzee, kila aliyeniona

alitokwa na machozi.
Nilipelekwa kwa mganga wa kiume ambaye aliponiona kabla ya kunitibu alishauri kwanza nikapimwe damu kwani nilikuwa na dalili

zote za ugonjwa wa kisasi kama kukonda na nywele kubadilika rangi.
Nilipelekwa hospitali kupima na majibu yakaonesha kwamba sikuwa na tatizo lolote. Mganga baada ya kupata majibu alianza

kunitibu, kwanza kwa kuangalia tatizo langu lilikuwa ni nini.
Japokuwa nilikuwa siwezi kukaa lakini alichokuwa akikisema nilikisikia:
"Mgonjwa wenu amechezewa na mwanamke."
"Kivipi?"
"Ametupiwa jini."
"Na nani?" mama aliuliza.
"Na mwanamke mmoja aliyemtembelea kwake."
Kauli yake iliwafanya mama na dada zangu waangaliane na kushusha pumzi ndefu.
"Ni nani?"
"Mwenyewe anamjua, kuna siku alitembelewa na mgeni saa tano asubuhi akiwa amevaa vitenge kuanzia juu mpaka chini. ni

kweli?"
"Ni kweli kabisa," nilijibu.
"Basi yule ndiye mbaya wenu japokuwa siku ile hakuja kwa shari."
"Ni nani?"
"Huyu ana mwanaume ambaye ana mke na yule ndiye mkewe. Bahati mbaya alikuwa hajulikani ila alitaka kupata ukweli baada ya

kuujua ukweli ndipo alipokwenda kufanya mambo yake.
"Alitumia uchawi wa jini kupitia kwa mumewe, jini lile lilikuwa likitembea naye bila kujua na muda wa kukutana jini lilitangulia

mbele ili kuuharibu ujauzito.
Baada ya kukutana na mwenzako ndipo lilipopata nafasi ya kutangulia na kusababisha utokwe na damu ukiwa mwanzo wa

kuuharibu ujauzito wako.
"Kwa vile ulitokwa na damu hukufahamu tatizo, ulikwenda hospitali na kufanikiwa kuzuia damu isitoke. Kwa vile ulikuwa hujui

kilichokuwa kikiendelea uliamini tatizo lako lilikuwa limekwisha.
"Kwa vile jini lile lilitumia njia ya wewe kukutana na mwenzako, lilisubiri mtakapokutana tena. Siku mliyokutana lilitumia nafasi

hiyo kuharibu ujauzito wako ulioambatana na kutokwa na damu nyingi sana."
"Sasa mbona baada ya ujauzito kutoka kila siku hali yake inazidi kuwa mbaya, damu imekuwa haikomi kutoka?" mama aliuliza.
"Lile jini lililotumwa kwake lilikuwa na kazi mbili kubwa, kazi ya kwanza limeifanya vizuri na sasa linafanya kazi ya pili."
"Kazi gani?" mama aliuliza.
"Kwanza ilikuwa ni kuiharibu mimba, pili kummaliza taratibu mpaka azimike kabisa."
"Mungu wangu! Kwa hiyo bado jini hilo lipo?"
"Ndiyo."
"Kwa hiyo utatusaidiaje?"
"Kumtibu tu."
"Na aliyemfanyia?"
"Ngoja kwanza tumtibu kisha mambo mengine yatafuata."
Nilianza kupata tiba kwa kupewa dawa ya majani mabichi na kutakiwa kuinywa ambayo ilisababisha nitapike na kuharisha. Baada

ya muda nilipewa uji uliochanganywa na dawa.
Baada ya kunywa nilipitiwa na usingizi kwa muda mrefu tangu nianze kuumwa siku hiyo ndiyo niliyopata usingizi mzito.
Nilipoamka nilikuta tayari imeandaliwa nyungu ambayo nilifukizwa kwa kufunikwa na shuka. Kwa vile sikuwa na uwezo wa kukaa

peke yangu nilishikiliwa mpaka huduma ilipokwisha.
Nilirudishwa na kulazwa kwenye mkeka huku nikiwa navuja jasho kama maji mwili mzima kutokana na joto kali la nyungu.
Baada ya mapumziko nilipatiwa chakula, ajabu ni kwamba nilikula vizuri sana.
Siku ile nililala pale na kubaki na dada kwa ajili ya kunisaidia kwa vile miguu haikuwa na nguvu. Nilikaa kwa mganga kwa wiki mbili

nikiendelea kupata tiba.
Tiba ile ilinisaidia, niliweza kusimama na kutembea lakini kwa shida, hata hivyo nilikuwa na mabadiliko makubwa katika afya

yangu, ilikuwa tofauti na nilivyokwenda nikiwa mtu wa kubebwa. Mpaka naondoka kwa mganga damu ilikuwa imekata, hata hamu

ya kula nilikuwa nayo. Tatizo lilikuwa kwenye nguvu za miguu, nilikuwa siwezi kusimama au kutembea kwa muda mrefu.


Itaendelea Jumamosi
 
Back
Top Bottom