Mama yangu adui yangu

Mama yangu adui yangu

[h=1]Mama Yangu Adui Yangu -30-[/h]
ILIPOISHIA:
Mabadiliko ya hali yangu yalinishtua kidogo, nilimweleza mwenzangu ambaye alinishauri twende hospitali kuangalia afya yangu. Nilikwenda hospitali na kufanya vipimo, tena nakumbuka siku ile nilikuwa na mzee Sambi. Baada ya daktari kuangalia majibu ya vipimo alivyonieleza nikapime alisema:
“Vipimo vinaonesha upo sawa, ila...”
Alishusha pumzi na kututazama usoni na kutabasamu kitu kilichonifanya nijiulize mbona anatabasamu ameona nini.
“Ila nini dokta?” mzee Sambi aliuliza wakati huo nilikuwa nimemuegemea begani.
“Hongereni.”
SASA ENDELEA...

“Hongera ya nini?” mzee Sambi aliuliza.
“Inaonekana mambo si mabaya.”
“Kivipi?” safari ile niliuliza mimi.
“Inaonesha wewe ni mjamzito.”
“Nooo...nooo,” nilijikuta nikitikisa kichwa kukataa kama vile dokta ni muongo.
“Kwa nini unakataa?” aliniuliza akinishangaa.
“Hata siamini.”
“Kwa nini huamini.”
“Nimeitafuta sana mimba, siamini kama kweli Mungu kasikiliza maombi yangu.”
“Basi mama hongera sana kweli una ujauzito.”
“Nashukuru Mungu,” nilisema kwa sauti ya kilio, furaha ya ujauzito ilinifanya niangue kilio cha kwikwi.
“Basi mpenzi, tumshukuru Mungu kwa kila jambo,” mzee Sambi alinibembeleza.
Baada ya maelezo ya daktari jinsi ya kuitunza mimba changa tulirudi nyumbani. Njiani nilibakia na maswali ujauzito ule ni kudra za Mungu au dawa za mganga mama Amina ambaye naye alimuomba Mungu?
Lakini kwa upande mwingine nilikubaliana kuwa mama Amina ni mganga wa kweli kwa jinsi alivyonieleza ndivyo ilivyokuwa. Nilipanga kumpelekea zawadi kubwa kwa ujauzito ule, pia zawadi nyingine kama nikijifungua.
Kwa kweli ilikuwa furaha kubwa moyoni mwangu kushika ujauzito. Nilipofika nyumbani nilimjulisha da’ Suzy ambaye naye alifurahi sana. Nilimsikia akipiga vigelegele upande wa pili kuonesha naye alifurahia shoga yake kupata ujauzito.
Ujauzito wangu ulifanya nigeuke malkia kwa mzee Sambi, muda mwingi alihakikisha yupo karibu yangu huku akihakikisha sifanyi kazi yoyote ngumu mpaka nitakapojifungua.
Nilimfikishia taarifa mama kuhusiana na ujauzito wangu, alifurahi sana mwanaye kupata ujauzito. Furaha ya mama ilinifariji na kujisikia faraja moyoni mwangu.
“Mwaija angalie usirudie makosa ya awali ya kupoteza ujauzito wako,” mama alinionya.
“Mama sasa hivi nazingatia maelekezo ya madaktari ili kuifanya mimba yangu ikue vizuri.”
“Kama hivyo ni vizuri, mama yako nina hamu ya mjukuu.”
“Najua mama, tumuombe Mungu akupe mjukuu.”
“Inshaallah.”
Ukaribu wa mzee Sambi uliongezeka, muda mwingi hakucheza mbali na mimi huku akiniahidi ujauzito ukifika miezi minne angenipeleka Afrika Kusini na kukaa huko mpaka nitakapojifungua.
“Mwaija, katika kitu ambacho nilikiomba usiku na mchana basi ni hiki cha wewe kubeba ujauzito. Ujauzito ukifikisha miezi minne nakupeleka Afrika Kusini ambako utakaa mpaka utakapojifungua.”
“Kwani hapa kuna nini?”
“Katika kitu chenye thamani chini ya jua, ni hilo tumbo lako ambalo nataka nilitunze kuliko hata mboni za macho yangu.”
“Mpenzi unataka mtoto gani?”
“Japokuwa nataka wa kiume lakini yeyote atakayezaliwa ni zawadi yangu.”
Ukaribu wa mzee Sambi ulinifanya nikose muda wa kurudi kwa mganga kumueleza matokeo ya dawa aliyonipa ilinisaidia kushika ujauzito. Sikupenda kumweleza bwana ‘angu kuwa ujauzito wangu ulipatikana kupitia kwa mganga.
Wakati huo mzee Sambi alikuwa ameninunulia Rav 4 kwa ajili ya kunipeleka popote kama hayupo. Kwa vile nilikuwa sijajua kuendesha gari vizuri alinitafutia dereva kijana mmoja jirani yetu.
Muda mwingi alikuwa kijiweni nikiwa na shida nilimpigia na kuja mara moja kunisikiliza. Niliendelea kuona neema ya Mungu ikinifungukia kwa mambo yangu kuninyookea.
Miezi miwili ilikatika huku maendeleo kwenye ujenzi wangu yakipungua kasi japokuwa ilikuwa kwenye hatua za kumalizia. Mzee Sambi alinieleza nisiwe na wasiwasi muda si mrefu nyumba yangu itaisha.
Hali yangu ya ujauzito ilifanya niwe mtu wa kupumzika nyumbani, hata kwenye ‘super market’ yangu nilichelewa kuifungua mpaka hali yangu itakapokuwa vizuri, lakini kwa shauku ya mtoto aliyokuwa nayo mzee Sambi niliona mpaka nitakapojifungua.
Hospitali walisema tatizo la kuchoka sana litaisha baada ya ujauzito kukua, ile hali ilikuwa ya mpito. Pamoja na kuwa nachoka lakini nilipata huduma zote muhimu.
Mzee Sambi alihamia kwangu kwa wiki mbili akinieleza ameaga kwa mkewe amesafiri kikazi. Mtoto wa kike nilinenepa, mbona nilideka! Nini nilichokitaka nikakosa.
Siku moja nikiwa nimejipumzisha nyumbani, msichana wangu wa kazi alinieleza kuna mgeni nje.
“Dada kuna mgeni.”
“Mwanaume au mwanamke?”
“Mwanamke wa makamo.”
“Mwambie aingie.”
Baada ya muda aliingia mama mmoja aliyekuwa amevaa gauni la kitenge na kitenge kingine alijifunga chini na juu alivaa kilemba.

Itaendelea Alkhamisi ijayo....
 
mtihani tena huo diiiih .. ahsante kaka - MziziMkavu hakika tunakushukuru kwa mda na nguvu zako hapa
 
Binti wee yaani 'unaangamia kwa kukosa maarifa'. Mamiyo mwanga wa kutupa halafu eti chereko chereko unamwambia ati sasa wewe ni mja mzito subiri kupigwa hilo 'zaiko' jingine mimba hiyo iishie kuliwa na jini
 
Kwaajili ulikosa kuendeleza hii hadithi kwa siku kadhaa ilikubidi uweke parts tatu kwa mpigo:A S shade:
 
hapo hakuna mimba wala nyumba.na huyo binti hamnazo kwel.amesahau alichoambiwa na mganga.nice story
 
[h=1]Mama Yangu Adui Yangu -30-[/h]
ILIPOISHIA:
Mabadiliko ya hali yangu yalinishtua kidogo, nilimweleza mwenzangu ambaye alinishauri twende hospitali kuangalia afya yangu. Nilikwenda hospitali na kufanya vipimo, tena nakumbuka siku ile nilikuwa na mzee Sambi. Baada ya daktari kuangalia majibu ya vipimo alivyonieleza nikapime alisema:
“Vipimo vinaonesha upo sawa, ila...”
Alishusha pumzi na kututazama usoni na kutabasamu kitu kilichonifanya nijiulize mbona anatabasamu ameona nini.
“Ila nini dokta?” mzee Sambi aliuliza wakati huo nilikuwa nimemuegemea begani.
“Hongereni.”
SASA ENDELEA...

“Hongera ya nini?” mzee Sambi aliuliza.
“Inaonekana mambo si mabaya.”
“Kivipi?” safari ile niliuliza mimi.
“Inaonesha wewe ni mjamzito.”
“Nooo...nooo,” nilijikuta

Ah Mzizi/mzinzi,ulianza kudo kidato cha pili,....
 
[h=1]Mama Yangu Adui Yangu -30-[/h]
ILIPOISHIA:
Mabadiliko ya hali yangu yalinishtua kidogo, nilimweleza mwenzangu ambaye alinishauri twende hospitali kuangalia afya yangu. Nilikwenda hospitali na kufanya vipimo, tena nakumbuka siku ile nilikuwa na mzee Sambi. Baada ya daktari kuangalia majibu ya vipimo alivyonieleza nikapime alisema:
“Vipimo vinaonesha upo sawa, ila...”
Alishusha pumzi na kututazama usoni na kutabasamu kitu kilichonifanya nijiulize mbona anatabasamu ameona nini.
“Ila nini dokta?” mzee Sambi aliuliza wakati huo nilikuwa nimemuegemea begani.
“Hongereni.”

SASA ENDELEA...

“Hongera ya nini?” mzee Sambi aliuliza.
“Inaonekana mambo si mabaya.”
“Kivipi?” safari ile niliuliza mimi.
“Inaonesha wewe ni mjamzito.”
“Nooo...nooo,” nilijikuta nikitikisa kichwa kukataa kama vile dokta ni muongo.
“Kwa nini unakataa?” aliniuliza akinishangaa.
“Hata siamini.”
“Kwa nini huamini.”
“Nimeitafuta sana mimba, siamini kama kweli Mungu kasikiliza maombi yangu.”
“Basi mama hongera sana kweli una ujauzito.”
“Nashukuru Mungu,” nilisema kwa sauti ya kilio, furaha ya ujauzito ilinifanya niangue kilio cha kwikwi.
“Basi mpenzi, tumshukuru Mungu kwa kila jambo,” mzee Sambi alinibembeleza.
Baada ya maelezo ya daktari jinsi ya kuitunza mimba changa tulirudi nyumbani. Njiani nilibakia na maswali ujauzito ule ni kudra za Mungu au dawa za mganga mama Amina ambaye naye alimuomba Mungu?
Lakini kwa upande mwingine nilikubaliana kuwa mama Amina ni mganga wa kweli kwa jinsi alivyonieleza ndivyo ilivyokuwa. Nilipanga kumpelekea zawadi kubwa kwa ujauzito ule, pia zawadi nyingine kama nikijifungua.
Kwa kweli ilikuwa furaha kubwa moyoni mwangu kushika ujauzito. Nilipofika nyumbani nilimjulisha da’ Suzy ambaye naye alifurahi sana. Nilimsikia akipiga vigelegele upande wa pili kuonesha naye alifurahia shoga yake kupata ujauzito.
Ujauzito wangu ulifanya nigeuke malkia kwa mzee Sambi, muda mwingi alihakikisha yupo karibu yangu huku akihakikisha sifanyi kazi yoyote ngumu mpaka nitakapojifungua.
Nilimfikishia taarifa mama kuhusiana na ujauzito wangu, alifurahi sana mwanaye kupata ujauzito. Furaha ya mama ilinifariji na kujisikia faraja moyoni mwangu.
“Mwaija angalie usirudie makosa ya awali ya kupoteza ujauzito wako,” mama alinionya.
“Mama sasa hivi nazingatia maelekezo ya madaktari ili kuifanya mimba yangu ikue vizuri.”
“Kama hivyo ni vizuri, mama yako nina hamu ya mjukuu.”
“Najua mama, tumuombe Mungu akupe mjukuu.”
“Inshaallah.”
Ukaribu wa mzee Sambi uliongezeka, muda mwingi hakucheza mbali na mimi huku akiniahidi ujauzito ukifika miezi minne angenipeleka Afrika Kusini na kukaa huko mpaka nitakapojifungua.
“Mwaija, katika kitu ambacho nilikiomba usiku na mchana basi ni hiki cha wewe kubeba ujauzito. Ujauzito ukifikisha miezi minne nakupeleka Afrika Kusini ambako utakaa mpaka utakapojifungua.”
“Kwani hapa kuna nini?”
“Katika kitu chenye thamani chini ya jua, ni hilo tumbo lako ambalo nataka nilitunze kuliko hata mboni za macho yangu.”
“Mpenzi unataka mtoto gani?”
“Japokuwa nataka wa kiume lakini yeyote atakayezaliwa ni zawadi yangu.”
Ukaribu wa mzee Sambi ulinifanya nikose muda wa kurudi kwa mganga kumueleza matokeo ya dawa aliyonipa ilinisaidia kushika ujauzito. Sikupenda kumweleza bwana ‘angu kuwa ujauzito wangu ulipatikana kupitia kwa mganga.
Wakati huo mzee Sambi alikuwa ameninunulia Rav 4 kwa ajili ya kunipeleka popote kama hayupo. Kwa vile nilikuwa sijajua kuendesha gari vizuri alinitafutia dereva kijana mmoja jirani yetu.
Muda mwingi alikuwa kijiweni nikiwa na shida nilimpigia na kuja mara moja kunisikiliza. Niliendelea kuona neema ya Mungu ikinifungukia kwa mambo yangu kuninyookea.
Miezi miwili ilikatika huku maendeleo kwenye ujenzi wangu yakipungua kasi japokuwa ilikuwa kwenye hatua za kumalizia. Mzee Sambi alinieleza nisiwe na wasiwasi muda si mrefu nyumba yangu itaisha.
Hali yangu ya ujauzito ilifanya niwe mtu wa kupumzika nyumbani, hata kwenye ‘super market’ yangu nilichelewa kuifungua mpaka hali yangu itakapokuwa vizuri, lakini kwa shauku ya mtoto aliyokuwa nayo mzee Sambi niliona mpaka nitakapojifungua.
Hospitali walisema tatizo la kuchoka sana litaisha baada ya ujauzito kukua, ile hali ilikuwa ya mpito. Pamoja na kuwa nachoka lakini nilipata huduma zote muhimu.
Mzee Sambi alihamia kwangu kwa wiki mbili akinieleza ameaga kwa mkewe amesafiri kikazi. Mtoto wa kike nilinenepa, mbona nilideka! Nini nilichokitaka nikakosa.
Siku moja nikiwa nimejipumzisha nyumbani, msichana wangu wa kazi alinieleza kuna mgeni nje.
“Dada kuna mgeni.”
“Mwanaume au mwanamke?”
“Mwanamke wa makamo.”
“Mwambie aingie.”
Baada ya muda aliingia mama mmoja aliyekuwa amevaa gauni la kitenge na kitenge kingine alijifunga chini na juu alivaa kilemba.

Itaendelea Alkhamisi ijayo......
 
Back
Top Bottom