Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,037
- 34,741
- Thread starter
- #221
[h=1]Mama Yangu Adui Yangu -31[/h]
ILIPOISHIA:
Hospitali walisema tatizo la kuchoka sana litaisha baada ya ujauzito kukua, ile hali ilikuwa ya mpito.
Pamoja na kuchoka lakini nilipata huduma zote muhimu.
Mzee Sambi alihamia kwangu kwa wiki mbili akinieleza ameaga kwa mkewe kuwa amesafiri kikazi.
Mtoto wa kike nilinenepa mbona na kuongeza deko, hakuna nilichokitaka nikakikosa.
Siku moja nikiwa nimejipumzisha nyumbani msichana wangu wa kazi alinieleza kuwa kuna mgeni nje.
"Mwanaume au mwanamke?"
"Mwanamke wa makamo."
"Mwambia aingie."
Baada ya muda aliingia mama mmoja aliyekuwa amevaa gauni la kitenge na kingine alijifunga chini na juu alitengeneza kilemba.
SASA ENDELEA...
Vazi lile lilikuwa limempendeza sana yule mama ambaye alikuwa na umri wa dada zangu.
"Karibu dada," nilimkaribisha nikiwa nimejilaza kwenye kochi.
"Asante," alijibu na kwenda kukaa kwenye kochi lililokuwa likitazamana na kochi langu.
"Shikamoo," nilimwamkia huku nikijitahidi kukaa kitako.
"Marahaba, za hapa?"
"Mmh! Nzuri, karibu."
"Asante, mzee Sambi nimemkuta?"
"Ametoka."
"Ametoka saa ngapi?" aliniuliza huku akitembeza macho kila kona ya nyumba kama anakagua kitu.
"Asubuhi lakini hachelewi kurudi."
"Samahani mama unatumia kinywaji gani?" msichana wangu wa kazi alimuuliza mgeni.
"Asante, situmii kitu," mgeni alishukuru. Nilipomuangalia kwa chati mkononi alikuwa ameshika ufunguo wa gari, pia alikuwa na mkufu na hereni za dhahabu na mkononi alikuwa na pete katika vidole vitatu, hakika yule mama alikuwa anaonekana ni mtu mwenye maisha mazuri.
"Mama yangu ungekunywa hata juisi basi," nilimbembeleza mgeni.
"Usihofu, siku nyingine."
"Ulikuwa na shida gani?"
"Aah! Basi nitaonana naye."
"Kwa hiyo akija nimwambie nani aliyekuja?"
"Nitamuona tu wala usihofu, naomba niwakimbie."
"Japokuwa hukutaka kutuambia wewe ni nani, nikuruhusu dada yangu."
Yule mama alinyanyuka na kutoka na kuniacha nikimsindikiza kwa macho. Baada ya kutoka nilijiuliza yule ni nani aliyekuja kumuulizia mzee Sambi.
Alikuwa mtu wa kwanza kuja kumuulizia mzee Sambi tangu nihamie pale, wazo la haraka lilikuwa labda mwenye nyumba ambaye nilielezwa kwamba ni mwanamke ambaye hakai maeneo yale.
Nilijiuliza alikuwa na shida gani kwani kodi yake alishalipwa ya mwaka mzima. Niliachana naye na kuendelea na yangu.
Muda mfupi baada ya yule mama kuondoka, aliingia mzee Sambi. Kama kawaida nilimpokea kwa kujilazimisha huku akinikataza kunyanyuka.
"Aah! Tulia unaenda wapi mpenzi?"
"Mpenzi unafikiri nisipofanya mazoezi si nitalemaa ulimsikia daktari alivyosema?"
"Asubuhi si ulifanya, pumzika sitaki uteseke."
"Sawa, lakini kukupokea ni moja ya mazoezi siyo mateso."
"Haya mpenzi."
Baada ya kupumzika nilimweleza kuhusu yule mgeni aliyefika kumuulizia muda mfupi kabla hajarejea.
"Mpenzi kuna mtu alikuja kukuulizia."
" Mtu?"
"Ndiyo."
"Alikuja kuniulizia hapa?"
"Ndiyo."
"Mmh! Mtu gani huyo anayejua naishi hapa?"
"Kuna mama mmoja alikuja kukuulizia, inawezekana ni mwenye nyumba wako."
"Mmh! Ana shida gani namba yangu ya simu si anayo!"
"Mi nitajuaje."
"Amesemaje?"
"Amesema mtaonana baadaye."
"Hakuacha ujumbe wowote?"
"Hakuacha."
"Kwani yupo vipi?"
"Mrefu mweusi, amevaa vitenge kuanzia juu mpaka chini."
"Ana mwanya?"
"Ndiyo."
"Na ana meno mawili ya dhahabu?"
"Ndiyo, una mfahamu?"
"Ndiyo."
"Ni nani?"
"Achana naye ni mwenye nyumba."
"Sasa mbona amekuja bila taarifa?"
"Nitaonana naye, kama ana shida lazima atanipigia tu."
"Mmh! Inaonekana mwenye nyumba anajipenda sana."
"Kawaida, baada ya kuniuliza ukamjibu sipo alisema kitu gani kingine?"
"Amesema mtaonana."
"Ni hilo tu?"
"Ndiyo."
"Mmh! Sawa."
"Kwani vipi mbona kama umeshtuka?"
"Kawaida tu."
Sikutaka kumuuliza sana niliamini yule ni mama mwenye nyumba. Usiku wa siku ile aliniaga kurudi kwake japokuwa awali alipanga kurudi jioni ya siku ya pili.
"Vipi mbona ghafla?" nilimuuliza.
"Hapana kesho nitarudi."
Pia, sikutaka kumzuia kwa vile nilikuwa naye kwangu kwa wiki moja na nusu kitu ambacho kilikuwa hakijatokea, siku za nyuma alikuwa akilala mara mojamoja na kuondoka siku ya pili.
***
Ilikuwa ajabu baada ya mzee Sambi kuondoka ilipita wiki bila kufika kwangu kitu ambacho hakikuwa cha kawaida. Baada ya wiki moja ndipo alikuja. Vilevile sikutaka kumuuliza niliamini ni mihangaiko na nilizingatia ni mume wa mtu.
Siku aliyokuja tulikutana faragha na saa tano aliondoka kwenda kwake. Nilala vizuri mpaka asubuhi wakati huo nilikuwa nalala na msichana wa kazi kwa ajili ya msaada wa usiku.
Siku ya pili nilipoamka nilipokwenda kuoga nilishtuka kukuta kwenye nguo ya ndani kuna damu kidogo. Haikunishtua sana japokuwa nilijiuliza damu ile ilitokana na nini!
Sikutaka kukaa kimya nilimjulisha mzee Sambi kuhusiana na hali niliyoikuta asubuhi.
"Mmh! Au jana nimetumia nguvu?"
"Walaa, kawaida, mbona nipo sawa tu ila kilichonishtua ni damu kidogo kwenye nguo ya ndani."
"Unasikia mabadiliko yoyote mwilini?"
"Nipo sawa."
"Fanya hivi fika hospitali mara moja mi nitakuja baadaye ila nijulishe maendeleo yako."
"Hakuna tatizo."
"Basi fanya hivyo."
Baada ya kuzungumza na mzee wangu nilioga na kumpigia dereva aliyekuwa akinisaidia kunipeleka popote kwa vile nilikuwa sijajua vizuri gari, pia kutokana na hali yangu ya ujauzito sikutaka kuendesha.
Baada ya kufika nilimweleza anipeleke hospitali.
Sele alinipeleka mpaka Hospitali ya Madona iliyopo Tabata Aroma. Nilipofika nilimweleza daktari hali niliyokutana nayo asubuhi naye alishtuka sana. Lakini baada ya kunifanyia vipimo ilionesha hakukuwa na athari zozote kwenye ujauzito wangu.
Alinipa dawa na kunieleza nisifanye kazi yoyote ngumu kwa kipindi kile. Nilimshukuru Mungu kukuta ujauzito wangu ukiwa salama. Jioni alipokuja mzee Sambi nilimweleza niliyoelezwa hospitali kuhusu ujauzito wangu.
Alinipa dawa na kunieleza nisifanye kazi yoyote ngumu kwa kipindi kile.
"Nina wasiwasi labda nilitumia nguvu bila kujua."
"Mmh! Labda, sasa tutafanyaje?"
"Itabidi tuvumilie mpaka hali itakapokuwa sawa."
Tulikubaliana kutokutana kimwili kwa kipindi kile. Kwa vile muda wake wa kuwepo kwangu uliisha saa nne usiku aliondoka. Kama kawaida niliendelea kulala na msichana wangu wa kazi ambaye alikuwa mtu muhimu sana kwangu kwa kipindi hicho.
Itaendelea Jumapili