Mama yangu adui yangu

Mama yangu adui yangu

mzizi mkavu akizingua tunaendelea wenyewe na hadithi yetU!!!!

LIPOISHIA;
Vilevile sikuhoji nilitaka nione mwisho wake utakuwa vipi. Gari lilielekea Buguruni, lakini tuliongoza hadi Tabata Dampo. Tulipinda kulia kufuata barabara ya kuelekea Tabata.
Tulipofika Bima alikata kulia kuelekea Tabata Kimanga nami nilikuwa kimya nimetulia nione ananipeleka wapi. Tulipofika Savana alikata kulia na kusimamisha gari nje ya nyumba moja yenye geti na kuteremka kufungua geti.
Aliporudi kwenye gari nilimuuliza.
"Mpenzi wewe si una mke?"
SASA ENDELEA...
"Ndiyo."
"Sasa unanipeleka wapi?"
"Ondoa wasiwasi mpenzi."
"Kama kwako naomba unishushe."
"Hapana mpenzi, kwani nilikuambia nakaa wapi?"
"Sasa huku tunakwenda wapi?"
"Bebi mbona una wasiwasi? Siku zote nayajali sana maisha yako kuliko kawaida."
"Najua lakini naomba uniambie huku unanipeleka wapi?"
"Unaniamini?"
"Nakuamini."
"Basi niachie mimi kila kitu."
"Haya baba."
Mzee Sambi aliliingiza gari ndani ya geti na kulisimamisha mbele ya nyumba nzuri.
"Tumefika," alisema huku akinitazama usoni.
Sikumjibu nilitulia nikimuangalia, baada ya kuzima gari alinieleza:
"Tushuke."
Bila kuhoji kitu niliteremka na kufunga mlango wa gari, nikasimama nje ya gari kusubiri kujua pale nimeletwa wapi. Wazo langu la kwanza labda nyumba ya wageni.
Lakini katika makubaliano yetu ilikuwa mpaka akamilishe kila kitu ndipo na mimi nimpe mwili wangu. Lakini moyoni nilijikuta nikiwa tayari kumsikiliza atakachokitaka na kuusihi moyo wangu kutokuwa na swali kwa lolote litakalokuja mbele yangu.
Mzee Sambi baada ya kufunga mlango wa gari alikwenda hadi kwenye mlango wa nyumba ile na nilishangaa kuona akitoa ufunguo mfukoni na kufungua mlangoni. Baada ya kuzungusha funguo alinyonga kitasa na kuusukuma mlango kwa ndani.
Baada ya mlango kufunguka aliingia ndani na kutoka kisha aliniita.
"Bebi njoo."
Nilimfuata bila kusema kitu nikijua siku ile sikuwa na ujanja wa kukataa kufanya chochote na mzee Sambi, kutokana na kila alichokuwa akifanya mbele yangu kilianza kuivunja ngome ya moyo wangu.
Nilipofika mlangoni alinishika mkono na kuniingiza ndani ya nyumba ile, ambayo sebule yake ilikuwa imekamilika na kuwa na kila kitu kwa mtu mwenye maisha ya juu.
"Karibu mpenzi."
"Asante," nilijibu huku nikipepesa macho.
"Unapaonaje hapa?"
"Mmh! Pazuri."
Alinishika mkono na kunipeleka mpaka chumbani nikajua shughuli imefika, sikuwa na uwezo wa kupinga, kwa vile mpaka kukubali kuingia mle ndani nilikubali kwa hiyari yangu sikulazimishwa na mtu.
"Karibu bebi."
"A..a..sante."
"Mbona una wasiwasi?"
"Walaa," nilikataa tu lakini mazingira yale yalinifanya nipoteze kujiamini.
"Unakionaje chumba?"
"Kizuri," nilijibu kwa mkato.
"Bebi naomba nikuambie kitu."
Nilijua hana cha kuniambia zaidi ya kuniomba kufanya mapenzi kutokana na kunionesha vitu vya kunijali. Lakini bado nilikuwa na maswali pale ni kwa nani?
"Niambie tu bebi."
"Naomba nikuambie toka moyoni mwangu, Mwaija nakupenda."
"Hata mimi nakupenda," nilijibu nikiwa bado sijiamini.
"Nimefurahi kusikia hivyo."
"Hata mimi nafurahi kwa yote unayonifanyia na mengine utakayonifanyia."
"Naomba kwanza tutoke nje."
"Hakuna tatizo."
Tulitoka hadi nje ya nyumba na kunizungusha kuiangalia ile nyumba iliyokuwa kwenye hali nzuri sana. Bado sikumuelewa alinitoa nje kufanya nini.
"Mwaija."
"Abee."
"Hii nyumba unaionaje?"
"Mmh! Nzuri."
"Basi mpenzi kuanzia sasa utakaa hapa."
"Na ile nyumba unayonijengea Boko?"
"Hapa nimekupangia kwa muda wakati unasubiri nyumba yako kuisha ili nami nipate muda wa kuwa na wewe baada ya kazi kwa nafasi."
"Mmh! Asante mpenzi," nilimshukuru kwa kumkumbatia.
"Basi vitu vyote unavyoviona ndani vimenunuliwa juzi na kupangwa jana. Baada ya kuridhika ndiyo nikakuleta ujionee nyumba yako."
"Asante sana," nilijikuta nikiwa na furaha ya ajabu moyoni na kuona kama Mungu kaamua kunifanyia muujiza.
"Haya ni matunda ya msimamo na tabia zako, sijawahi kuona msichana kama wewe katika kipindi hiki."
"Mbona tupo wengi tu basi mmekuwa wavivu kuchagua vinavyong'aa barabarani mkadhani vyote ni dhahabu."
"Nimekubali na kauli yako."
Tulirudi ndani, kwa vile muda ulikuwa umekwenda nilimuomba aniwahishe nyumbani.

HADI ALHAMISI IJAYO:
Erick Shigongo njoo huku ukamate PIRATES.
 
Dah! Hivyo tutashindwa kufuatilia. Kwa sababu inakuwa kama hadithi za magazeti mpaka wiki ijayo tupe mambo! Ila nimeipenda sana

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Dah! Hivyo tutashindwa kufuatilia. Kwa sababu inakuwa kama hadithi za magazeti mpaka wiki ijayo tupe mambo! Ila nimeipenda sana

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Tokea hapo ni ya magazetini (Risasi jumatano na Jumamosi). Ukitaka na pini lingine linaitwa "AIIIII WEWE USITOE BWANA" utalipenda. Babuuuuuu... Babukaaaaaaaa
 
MAMA YANGU ADUI YANGU - 22-

ILIPOISHIA;
Vilevile sikuhoji nilitaka nione mwisho wake utakuwa vipi. Gari lilielekea Buguruni, lakini tuliongoza hadi Tabata Dampo. Tulipinda kulia kufuata barabara ya kuelekea Tabata.
Tulipofika Bima alikata kulia kuelekea Tabata Kimanga nami nilikuwa kimya nimetulia nione ananipeleka wapi. Tulipofika Savana alikata kulia na kusimamisha gari nje ya nyumba moja yenye geti na kuteremka kufungua geti.
Aliporudi kwenye gari nilimuuliza.
“Mpenzi wewe si una mke?”

SASA ENDELEA...

“Ndiyo.”
“Sasa unanipeleka wapi?”
“Ondoa wasiwasi mpenzi.”
“Kama kwako naomba unishushe.”
“Hapana mpenzi, kwani nilikuambia nakaa wapi?”
“Sasa huku tunakwenda wapi?”
“Bebi mbona una wasiwasi? Siku zote nayajali sana maisha yako kuliko kawaida.”
“Najua lakini naomba uniambie huku unanipeleka wapi?”
“Unaniamini?”
“Nakuamini.”
“Basi niachie mimi kila kitu.”
“Haya baba.”
Mzee Sambi aliliingiza gari ndani ya geti na kulisimamisha mbele ya nyumba nzuri.
“Tumefika,” alisema huku akinitazama usoni.
Sikumjibu nilitulia nikimuangalia, baada ya kuzima gari alinieleza:
“Tushuke.”
Bila kuhoji kitu niliteremka na kufunga mlango wa gari, nikasimama nje ya gari kusubiri kujua pale nimeletwa wapi. Wazo langu la kwanza labda nyumba ya wageni.
Lakini katika makubaliano yetu ilikuwa mpaka akamilishe kila kitu ndipo na mimi nimpe mwili wangu. Lakini moyoni nilijikuta nikiwa tayari kumsikiliza atakachokitaka na kuusihi moyo wangu kutokuwa na swali kwa lolote litakalokuja mbele yangu.
Mzee Sambi baada ya kufunga mlango wa gari alikwenda hadi kwenye mlango wa nyumba ile na nilishangaa kuona akitoa ufunguo mfukoni na kufungua mlangoni. Baada ya kuzungusha funguo alinyonga kitasa na kuusukuma mlango kwa ndani.
Baada ya mlango kufunguka aliingia ndani na kutoka kisha aliniita.
“Bebi njoo.”
Nilimfuata bila kusema kitu nikijua siku ile sikuwa na ujanja wa kukataa kufanya chochote na mzee Sambi, kutokana na kila alichokuwa akifanya mbele yangu kilianza kuivunja ngome ya moyo wangu.
Nilipofika mlangoni alinishika mkono na kuniingiza ndani ya nyumba ile, ambayo sebule yake ilikuwa imekamilika na kuwa na kila kitu kwa mtu mwenye maisha ya juu.
“Karibu mpenzi.”
“Asante,” nilijibu huku nikipepesa macho.
“Unapaonaje hapa?”
”Mmh! Pazuri.”
Alinishika mkono na kunipeleka mpaka chumbani nikajua shughuli imefika, sikuwa na uwezo wa kupinga, kwa vile mpaka kukubali kuingia mle ndani nilikubali kwa hiyari yangu sikulazimishwa na mtu.
“Karibu bebi.”
“A..a..sante.”
“Mbona una wasiwasi?”
“Walaa,” nilikataa tu lakini mazingira yale yalinifanya nipoteze kujiamini.
“Unakionaje chumba?”
“Kizuri,” nilijibu kwa mkato.
“Bebi naomba nikuambie kitu.”
Nilijua hana cha kuniambia zaidi ya kuniomba kufanya mapenzi kutokana na kunionesha vitu vya kunijali. Lakini bado nilikuwa na maswali pale ni kwa nani?
“Niambie tu bebi.”
“Naomba nikuambie toka moyoni mwangu, Mwaija nakupenda.”
“Hata mimi nakupenda,” nilijibu nikiwa bado sijiamini.
“Nimefurahi kusikia hivyo.”
“Hata mimi nafurahi kwa yote unayonifanyia na mengine utakayonifanyia.”
“Naomba kwanza tutoke nje.”
“Hakuna tatizo.”
Tulitoka hadi nje ya nyumba na kunizungusha kuiangalia ile nyumba iliyokuwa kwenye hali nzuri sana. Bado sikumuelewa alinitoa nje kufanya nini.
“Mwaija.”
“Abee.”
“Hii nyumba unaionaje?”
“Mmh! Nzuri.”
“Basi mpenzi kuanzia sasa utakaa hapa.”
“Na ile nyumba unayonijengea Boko?”
“Hapa nimekupangia kwa muda wakati unasubiri nyumba yako kuisha ili nami nipate muda wa kuwa na wewe baada ya kazi kwa nafasi.”
“Mmh! Asante mpenzi,” nilimshukuru kwa kumkumbatia.
“Basi vitu vyote unavyoviona ndani vimenunuliwa juzi na kupangwa jana. Baada ya kuridhika ndiyo nikakuleta ujionee nyumba yako.”
“Asante sana,” nilijikuta nikiwa na furaha ya ajabu moyoni na kuona kama Mungu kaamua kunifanyia muujiza.
“Haya ni matunda ya msimamo na tabia zako, sijawahi kuona msichana kama wewe katika kipindi hiki.”
“Mbona tupo wengi tu basi mmekuwa wavivu kuchagua vinavyong’aa barabarani mkadhani vyote ni dhahabu.”
“Nimekubali na kauli yako.”
Tulirudi ndani, kwa vile muda ulikuwa umekwenda nilimuomba aniwahishe nyumbani.

Itaendelea wiki ijayo.
 
MAMA YANGU ADUI YANGU - 23-

ILIPOISHIA:
“BASI mpenzi kuanzia sasa utakaa hapa.”
“Na ile nyumba unayonijengea Boko?”
“Hapa nimekupangia kwa muda wakati unasubiri nyumba yako kuisha ili nami nipate muda wa kuwa na wewe kwa nafasi baada ya kazi.”
“Mmh! Asante mpenzi,” nilimshukuru kwa kumkumbatia.
“Basi vitu vyote unavyoviona ndani vimenunuliwa juzi na kupangwa jana. Baada ya kuridhika ndiyo nikakuleta ujionee nyumba yako.”
“Asante sana,” nilijikuta nikiwa na furaha ya ajabu moyoni na kuona kama Mungu kaamua kunifanyia muujiza.
“Haya ni matunda ya msimamo na tabia zako, sijawahi kuona msichana kama wewe katika kipindi hiki.”
“Mbona tupo wengi tu basi mmekuwa wavivu kuchagua vinavyong’aa barabarani mkadhani vyote ni dhahabu.”
“Nimekubaliana na kauli yako.”

SASA ENDELEA...

Tulirudi ndani, kwa vile muda ulikuwa umekwenda nilimuomba aniwahishe nyumbani.
“Bebi kwa nini leo usilale hapa?”
“Mmh! Peke yangu jumba lote hili?”
“Tutalala wote.”
“Hapana siku nyingine, si unajua mimi mtoto wa mama lazima nikaage nyumbani kuwa naanza kujitegemea!”
“Hakuna tatizo nakusikiliza wewe.”
“Basi kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.”
“Hakuna tatizo.”
Tulikubaliana kuondoka tulizima taa na kufunga mlango wa nyumba na geti na kunirudisha nyumbani. Tulipofika maeneo ya Mwembe Yanga alinikodia teksi hadi nyumbani.
Nilifika nyumbani na kuwa na mawazo mengi juu ya mzee Sambi. Baada ya kuoga na kupata chakula cha usiku, nilimfuata mama chumbani kwake na kumweleza siri yangu.
Aliposikia namgongea alitoka na kuniuliza, kwa vile sikuwa na kawaida ya kumfuata muda ule. Toka nilipoanza kazi baada ya kazi nilikuwa chumbani kwangu nikiangalia CD za filamu.
Sikutaka kukaa nje kwa kuhofia kujiingiza kwenye vishawishi vibaya. Mama aliponiona aliniuliza:
“Vipi mama?”
“Nilikuwa na mazungumzo na wewe kidogo.”
“Sawa, nisubiri sebuleni nakuja.”
“Hapana mama nataka tuzungumzie chumbani kwako.”
“Mmh! Makubwa mazungumzo ya chumbani kwangu?”
“Ndiyo mama.”
“Haya karibu.”
Niliingia chumbani kwa mama na kukaa kitandani kwake karibu yake. Mama alimaliza kuweka vitu vyake vizuri kisha alinigeukia.
“Haya mama niambie.”
“Mama kuna kitu ninacho muda mrefu, ilikuwa vigumu kukueleza mwanzo kwa vile sikuwa na uhakika nacho.”
“Kitu gani hicho?”
“Mama nimepata rafiki wa kiume ambaye amejitolea kila kitu katika maisha yangu.”
“Nilijua, nilisubiri kuambiwa ningekuuliza ningeonekana muongo.”
“Inawezekana lakini mwanzo ilikuwa ngumu kulisema.”
“Haya mwanangu ulikuwa unasemaje?”
“Mama mtu mwenyewe unamfahamu.”
“Mwanangu nimfahamu vipi bila kunifahamisha.”
“Mzee Sambi.”
“Mzee Sambi aliyekuwa mpenzi wa dada yako?”
“Ndiyo.”
“Mmh! Makubwa, kwa nini umekubali kuchangia mapenzi na dada yako?” nilimshangaa mama kuniuliza swali kama lile.
“Hata mimi mwanzo sikutaka kukubali, lakini mzee yule alinieleza mambo mengi kuhusiana na dada kumfukuza na alivyotaka kumfanyia ambavyo vyote dada alivipiga teke.”
“Vitu gani?”
“Alitaka awe nyumba yake ndogo na kumuahidi kumjengea nyumba na kumnunulia gari.”
“Muongo wanaume wa mjini utawaweza, wanataka wakutumie wakitimiza haja zao wanaondoka bila kwa heri. Dada yako aliniambia nikamkatalia.”
“Mama makubaliano yetu ni kuwa naye baada ya kunikamilishia kila alichoniahidi.”
“Atawahi muongo mkubwa, atakuletea nyaraka za uongo ili uamini lakini mwishoni atazichukua.”
“Kwangu tofauti, hivi ninavyo kwambia ameisha ninunulia kiwanja na ujenzi utaanza mara moja.”
“Muongo?” mama alishtuka.
“Tena mama nyumba ikiisha litakuwa bonge la jumba pia amesema ataninunulia gari la kifahari.”
“Mmh! Hongera.”
“Asante na sasa hivi amenipangia nyumba nzima hivi ndiyo nimetoka kuiona yenye kila kitu ndani.”
“Dada yako akijua itakuwaje si unaujua ukorofi wake.”
“Yeye ndiye aliyeniambia kama namtaka nimchukue.”
“Basi mimi sina tatizo, kwa hiyo nyumba aliyokupangia itakuwaje?”
“Nitahamia wakati wowote.”
“Kwa hiyo utakuwa unakaa naye?”
“Hapana, hatujakubaliana hilo bali ametaka niwe huru na kuweza kuonana naye na kupanga mambo yetu kwa uhuru mkubwa.”
“Sawa, umeona ulijifanya mlokole yote haya ungeyapatia wapi?”
“Mama nilitaka kusahau, amesema eti nikimzalia mtoto wa kike atanipa milioni kumi na kiume ishirini.”
“Masuala ya nyumba na gari yanakufa?”
“Walaa hiyo ni bonasi ya furaha ya kupata mtoto.”
“Mmh! Makubwa.”
“Mama mbona unaguna.”
“Ndiyo nasikia kwako kumzalia mtu mtoto akulipe fedha.”
“Mama amesema mkewe hana kizazi hivyo anategemea kwangu.”
“Wewe ndiyo unacho?”
“Mama maneno gani hayo?” maneno ya mama yalinivunja nguvu.
“Siyo maneno gani, kwani huyo mkewe alilokosa kwa Mungu nini?”
“Sasa mama yeye kukosa kizazi na mimi kunaingiaje?”
“Siyo kuingiaje bali nenda na mawili, isije ahadi ya milioni kumi na ishirini ikayeyukia hewani ukachanganyikiwa bure. Mtoto ni majaliwa ya Mungu na si kwa ahadi ya fedha ingekuwa hivyo mkewe angemzalia.”
“Sawa mama nimekuelewa, nilikuja kukufahamisha tu.”
“Hicho kiwanja chenu kipo wapi?”
“Boko.”
“Utanipeleka lini nikakione?”
“Mwisho wa wiki.”
“Basi mwanangu nakutakia kila la heri.”
“Asante mama yangu.”
Niliagana na mama na kwenda kulala japokuwa nilichelewa kulala kwa kauli ya mama labda sina kizazi kwa kweli iliniumiza sana.
Nilijikuta nikiyadharau yote kwa kuamini kila kitu chini ya jua muwezeshaji wa yote ni Mungu pekee si mwanadamu.
Niliamini hakukuwa na haja ya kuendelea kuwa nyumbani kwa vile sifa ya nyumbani kwetu sikuipenda siku zote. Ilionekana Mungu alisikia kilio changu cha kuishi kwenye nyumba yenye sifa mbaya kilipokelewa.
Pamoja na furaha ya kutoka nyumbani lakini suala la kuanza kuishi na mzee Sambi kama mke na mume sikuliafiki kwa vile ilikuwa mapema sana.
Kukaa peke yangu jumba lile niliona haifai lazima nilitakiwa kuwa na mtu wa karibu. Nilikumbuka kuna msichana mmoja aliyekuwa akifanya kazi za ndani kwa jirani yetu niliye kuwa nimezoeana naye. Kuna siku alinifuata kabla ya kuanza kazi super market kuniomba aje pale kwetu au nimtafutie kazi kutokana na manyanyaso na ugumu wa kazi aliokuwa akikutana nao pale.
Niliamini nikiwa naye angenisaidia kazi pia kunichangamsha nikiwa nyumbani peke yangu. Nilijikuta nikipata tumaini la kuwa na mtu wa kukaa naye. Baada ya kuwaza sana usingizi ulinichukua.
***
Siku ya pili kabla ya kwenda kazini nilibahatika kumuona yule msichana ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi na saba.
Kwa kweli alifurahi sana kumpa habari ambazo ilionekana alikuwa akizisubiri kama wokovu.

Itaendelea Jumamosi ijayo....
 
MAMA YANGU ADUI YANGU - 23-

ILIPOISHIA:
BASI mpenzi kuanzia sasa utakaa hapa.
Na ile nyumba unayonijengea Boko?
Hapa nimekupangia kwa muda wakati unasubiri nyumba yako kuisha ili nami nipate muda wa kuwa na wewe kwa nafasi baada ya kazi.
Mmh! Asante mpenzi, nilimshukuru kwa kumkumbatia.
Basi vitu vyote unavyoviona ndani vimenunuliwa juzi na kupangwa jana. Baada ya kuridhika ndiyo nikakuleta ujionee nyumba yako.
Asante sana, nilijikuta nikiwa na furaha ya ajabu moyoni na kuona kama Mungu kaamua kunifanyia muujiza.
Haya ni matunda ya msimamo na tabia zako, sijawahi kuona msichana kama wewe katika kipindi hiki.
Mbona tupo wengi tu basi mmekuwa wavivu kuchagua vinavyongaa barabarani mkadhani vyote ni dhahabu.
Nimekubaliana na kauli yako.

SASA ENDELEA...

Tulirudi ndani, kwa vile muda ulikuwa umekwenda nilimuomba aniwahishe nyumbani.
Bebi kwa nini leo usilale hapa?
Mmh! Peke yangu jumba lote hili?
Tutalala wote.
Hapana siku nyingine, si unajua mimi mtoto wa mama lazima nikaage nyumbani kuwa naanza kujitegemea!
Hakuna tatizo nakusikiliza wewe.
Basi kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.
Hakuna tatizo.
Tulikubaliana kuondoka tulizima taa na kufunga mlango wa nyumba na geti na kunirudisha nyumbani. Tulipofika maeneo ya Mwembe Yanga alinikodia teksi hadi nyumbani.
Nilifika nyumbani na kuwa na mawazo mengi juu ya mzee Sambi. Baada ya kuoga na kupata chakula cha usiku, nilimfuata mama chumbani kwake na kumweleza siri yangu.
Aliposikia namgongea alitoka na kuniuliza, kwa vile sikuwa na kawaida ya kumfuata muda ule. Toka nilipoanza kazi baada ya kazi nilikuwa chumbani kwangu nikiangalia CD za filamu.
Sikutaka kukaa nje kwa kuhofia kujiingiza kwenye vishawishi vibaya. Mama aliponiona aliniuliza:
Vipi mama?
Nilikuwa na mazungumzo na wewe kidogo.
Sawa, nisubiri sebuleni nakuja.
Hapana mama nataka tuzungumzie chumbani kwako.
Mmh! Makubwa mazungumzo ya chumbani kwangu?
Ndiyo mama.
Haya karibu.
Niliingia chumbani kwa mama na kukaa kitandani kwake karibu yake. Mama alimaliza kuweka vitu vyake vizuri kisha alinigeukia.
Haya mama niambie.
Mama kuna kitu ninacho muda mrefu, ilikuwa vigumu kukueleza mwanzo kwa vile sikuwa na uhakika nacho.
Kitu gani hicho?
Mama nimepata rafiki wa kiume ambaye amejitolea kila kitu katika maisha yangu.
Nilijua, nilisubiri kuambiwa ningekuuliza ningeonekana muongo.
Inawezekana lakini mwanzo ilikuwa ngumu kulisema.
Haya mwanangu ulikuwa unasemaje?
Mama mtu mwenyewe unamfahamu.
Mwanangu nimfahamu vipi bila kunifahamisha.
Mzee Sambi.
Mzee Sambi aliyekuwa mpenzi wa dada yako?
Ndiyo.
Mmh! Makubwa, kwa nini umekubali kuchangia mapenzi na dada yako? nilimshangaa mama kuniuliza swali kama lile.
Hata mimi mwanzo sikutaka kukubali, lakini mzee yule alinieleza mambo mengi kuhusiana na dada kumfukuza na alivyotaka kumfanyia ambavyo vyote dada alivipiga teke.
Vitu gani?
Alitaka awe nyumba yake ndogo na kumuahidi kumjengea nyumba na kumnunulia gari.
Muongo wanaume wa mjini utawaweza, wanataka wakutumie wakitimiza haja zao wanaondoka bila kwa heri. Dada yako aliniambia nikamkatalia.
Mama makubaliano yetu ni kuwa naye baada ya kunikamilishia kila alichoniahidi.
Atawahi muongo mkubwa, atakuletea nyaraka za uongo ili uamini lakini mwishoni atazichukua.
Kwangu tofauti, hivi ninavyo kwambia ameisha ninunulia kiwanja na ujenzi utaanza mara moja.
Muongo? mama alishtuka.
Tena mama nyumba ikiisha litakuwa bonge la jumba pia amesema ataninunulia gari la kifahari.
Mmh! Hongera.
Asante na sasa hivi amenipangia nyumba nzima hivi ndiyo nimetoka kuiona yenye kila kitu ndani.
Dada yako akijua itakuwaje si unaujua ukorofi wake.
Yeye ndiye aliyeniambia kama namtaka nimchukue.
Basi mimi sina tatizo, kwa hiyo nyumba aliyokupangia itakuwaje?
Nitahamia wakati wowote.
Kwa hiyo utakuwa unakaa naye?
Hapana, hatujakubaliana hilo bali ametaka niwe huru na kuweza kuonana naye na kupanga mambo yetu kwa uhuru mkubwa.
Sawa, umeona ulijifanya mlokole yote haya ungeyapatia wapi?
Mama nilitaka kusahau, amesema eti nikimzalia mtoto wa kike atanipa milioni kumi na kiume ishirini.
Masuala ya nyumba na gari yanakufa?
Walaa hiyo ni bonasi ya furaha ya kupata mtoto.
Mmh! Makubwa.
Mama mbona unaguna.
Ndiyo nasikia kwako kumzalia mtu mtoto akulipe fedha.
Mama amesema mkewe hana kizazi hivyo anategemea kwangu.
Wewe ndiyo unacho?
Mama maneno gani hayo? maneno ya mama yalinivunja nguvu.
Siyo maneno gani, kwani huyo mkewe alilokosa kwa Mungu nini?
Sasa mama yeye kukosa kizazi na mimi kunaingiaje?
Siyo kuingiaje bali nenda na mawili, isije ahadi ya milioni kumi na ishirini ikayeyukia hewani ukachanganyikiwa bure. Mtoto ni majaliwa ya Mungu na si kwa ahadi ya fedha ingekuwa hivyo mkewe angemzalia.
Sawa mama nimekuelewa, nilikuja kukufahamisha tu.
Hicho kiwanja chenu kipo wapi?
Boko.
Utanipeleka lini nikakione?
Mwisho wa wiki.
Basi mwanangu nakutakia kila la heri.
Asante mama yangu.
Niliagana na mama na kwenda kulala japokuwa nilichelewa kulala kwa kauli ya mama labda sina kizazi kwa kweli iliniumiza sana.
Nilijikuta nikiyadharau yote kwa kuamini kila kitu chini ya jua muwezeshaji wa yote ni Mungu pekee si mwanadamu.
Niliamini hakukuwa na haja ya kuendelea kuwa nyumbani kwa vile sifa ya nyumbani kwetu sikuipenda siku zote. Ilionekana Mungu alisikia kilio changu cha kuishi kwenye nyumba yenye sifa mbaya kilipokelewa.
Pamoja na furaha ya kutoka nyumbani lakini suala la kuanza kuishi na mzee Sambi kama mke na mume sikuliafiki kwa vile ilikuwa mapema sana.
Kukaa peke yangu jumba lile niliona haifai lazima nilitakiwa kuwa na mtu wa karibu. Nilikumbuka kuna msichana mmoja aliyekuwa akifanya kazi za ndani kwa jirani yetu niliye kuwa nimezoeana naye. Kuna siku alinifuata kabla ya kuanza kazi super market kuniomba aje pale kwetu au nimtafutie kazi kutokana na manyanyaso na ugumu wa kazi aliokuwa akikutana nao pale.
Niliamini nikiwa naye angenisaidia kazi pia kunichangamsha nikiwa nyumbani peke yangu. Nilijikuta nikipata tumaini la kuwa na mtu wa kukaa naye. Baada ya kuwaza sana usingizi ulinichukua.
***
Siku ya pili kabla ya kwenda kazini nilibahatika kumuona yule msichana ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi na saba.
Kwa kweli alifurahi sana kumpa habari ambazo ilionekana alikuwa akizisubiri kama wokovu.

Itaendelea Jumamosi ijayo....

asante!! MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Mhh yaani nina hema mimi pekeyangu yaani nahisi kama vile Mzee Sambi atamtosa huyu Binti jamani!! yaani kama naogopa vile. Haya twasubiri tusikie.
 
Umeshamshirikisha mamako, kila kitu kitaishia njiani na huyo mzee sambi, hakuna nyumba wala kuzaa mtoto, pole
 
MAMA YANGU ADUI YANGU - 24-

ILIPOISHIA:
Siku ya pili kabla ya kwenda kazini nilibahatika kumuona yule msichana ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi na saba.
Kwa kweli alifurahi sana kumpa habari ambazo alionekana alikuwa akizisubiri kama wokovu.

SASA ENDELEA...

Nilimweleza nitampitia jioni ya siku ile nikitoka kazini na kwenda naye kwangu. Nilikwenda kazini na kumweleza da Suzy ambaye alizidi kuusifia uamuzi wangu wa kukubali kuwa na mzee Sambi.
Jioni mzee alinipitia, nikamweleza kuanzia siku ile nitahamia kwangu. Alifurahi sana kwa kitendo changu cha kukubaliana naye bila masharti magumu.
“Lakini mpenzi nitakuwa na msichana wa kazi.”
“Wala usiwe na wasiwasi, nilikuwa na wazo hilo maana jumba ni kubwa unatakiwa kuwa na mtu kama mimi sipo,” mzee Sambi alinifurahisha sana, hakuwa mtu wa kunipinga jambo.
“Basi sasa hivi nakwenda kumpitia ili tuende naye kwangu.”
“Hakuna tatizo.”
Tulikwenda hadi Temeke na kumpitia msichana wa kazi ambaye nilimkuta amejiandaa. Kabla ya kuondoka niliwaaga ndugu zangu ambao walishtuka.
“Vipi tena?”
“Nawakimbia kidogo.”
“Wapi?”
“Tabata.”
“Mmh! Vipi Beka karudi nini?” dada mdogo aliuliza.
“Walaa, yupo mwingine, dada anamjua.”
“Siku hizi yupo na mzee Super.”
“Mzee Sambi?” dada mdogo alishtuka.
“Ndiyo, mdogo wetu kaamua kujimilikisha mzee mzima.”
“Ha! Wee Mwaija umekosa wanaume wote mpaka umchukue mpenzi wa dada yako? We si ulikuwa mlokole, imekuwaje leo kuchangia bwana na dada yako?” dada alizidi kushangaa.
“Kila kitu dada anajua.”
“Mwache kwa raha zake, mzee yule mshamba nilimtimua. Eti ataninunulia gari, ooh atanijengea nyumba, utongozaji wa kizamani. Nilimpa penzi la muda siyo kung’ang’aniana kama ruba.
Alichonichefua zaidi eti tukapime ili nimzalie mtoto kwa madai kuwa atanipa milioni kumi, nilimwambia mimi nina shida ya mtoto? Aliambiwa mi kiwanda cha kuzalisha watoto? Mdogo wangu kamzalie mtoto upate hiyo nyumba, gari na milioni kumi.”
“Mmh! Kumbe nimekuwa -----, yaani mambo yanapita juu yangu bila kujua? Kwa hiyo umemruhusu mdogo wako atembee na bwana’ ako?”
“Kipi cha ajabu? Si afadhali Mwaija aliniuliza kuliko wewe uliyekuwa ukitembea na bwana yangu mpaka ukaniwekea fitina nikaachwa,” dada mkubwa alimjia juu dada mdogo.
Niliona mjadala wangu utavumbua yasiyonihusu. Nikaamua kuwaaga.
“Jamani dada zangu mi nawahi, naamini tutaonana mwisho wa wiki.”
“Hakuna tatizo, ukitulia uje utuchukue.”
“Hakuna tatizo.”
Kwa vile muda ulikuwa umekwenda niliondoka kwa kumpitia msichana wangu wa kazi na kwenda naye hadi kwangu, Tabata Savana. Nilipofika nilimweleza kuwa nitaishi naye kama ndugu yangu japokuwa nitamlipa mshahara kama kawaida. Alinishukuru kwa kumtoa kwenye mateso.
***
Niliyaanza maisha mapya ya kuishi kwangu nikiwa na mzee Sambi ambaye wakati huo alikuwa akinitafutia eneo kwa ajili ya kunifungulia ‘mini super market’ maeneo ya karibu na aliponipangia kati ya Tabata Mawenzi au Shiba.
Niliendelea kumshukuru Mungu kwa kuyabadili maisha yangu huku bado nikiwa namkumbuka mume wangu Beka juu ya kunipa talaka bila sababu.
Kila nilipokuwa peke yangu nilimkumbuka sana Beka, mwanaume ambaye niliamini ndiye wa maisha yangu. Nilikuwa na mzee Sambi ambaye nilimpenda kutokana na kujitoa kwa ajili yangu huku akijitahidi kuona naishi maisha ya furaha muda wote. Lakini mapenzi ya kweli yalikuwa kwa Beka.
Lakini lazima niseme ukweli mzee Sambi sikumpenda kwa asilimia zote. Niliapa kumsamehe Beka kama atagundua makosa yake na kuja kuniomba msamaha.
Unaweza kunishangaa, lakini nilikuwa radhi kuishi maisha yoyote na Beka na kuwa tayari kuachana na kila kitu nilichoahidiwa na mzee Sambi.
Beka nilimpenda naye alinipenda hilo nililitambua, lakini kilichovunja mapenzi yetu sikukielewa mpaka siku ile alipokuja na kunipa talaka iliyokosa maelezo ya kina.
Mara nyingi nilipokuwa peke yangu nilijisahau na kuweka mkono shavuni na machozi kunitoka nikimkumbuka. Pamoja na raha nilizopewa na mzee Sambi huku ujenzi wa jumba langu la kisasa ukiendelea, bado nilikuwa na jeraha kubwa moyoni mwangu ambalo siku zote halikupona kwa vile sikujua sababu ya kupewa talaka bila kuelezwa kisa.
Siku zote mtu akihukumiwa kwa kosa analolijua hata kama ni dogo na hukumu kuwa kubwa hujua kosa lake. Lakini kwangu hata nilipokuwa katikati ya furaha, kila nilipokumbuka mazingira tata ya talaka yangu, furaha ilinipotea na kujikuta nikitokwa machozi na kuweka mkono shavuni.
Mara nyingi msichana wangu wa kazi alikuwa akinishtua na kutaka kujua sababu ya mimi kuwa vile. Siku moja uvumilivu ulimshinda na kuamua kuniuliza:
“Dada una tatizo gani?”
“Nipo sawa.”
“Hapana dada si mara ya kwanza kukuona hivi, mara nyingi ukiwa peke yako unakuwa umeshika tama machozi yanakutoka kisha unatikisa kichwa na na kufuta machozi.”
“Mmh! Mdogo wangu ya dunia.”
“Yapi dada, mbona mimi yangu nimemwachia Mungu.”
“Ni kweli mdogo wangu, lakini langu linanitesa kila nikilikumbuka, kwa akili ya kawaida unaweza kulidharau lakini langu ni donda ninalolitonesha kila mara.”
“Kwani dada una tatizo gani?” Mariamu aliniuliza akiwa ananitazama kwa jicho la huruma.

Je, nini kitaendelea? Fuatilia wiki inayofuata
 
MAMA YANGU ADUI YANGU - 25-

ILIPOISHIA:
Siku zote mtu akihukumiwa kwa kosa analolijua hata kama ni dogo na hukumu ikawa kubwa hujua kosa lake. Lakini kwangu hata nilipokuwa katikati ya furaha kila nilipokumbuka mazingira tata ya talaka yangu, furaha ilinipotea na kujikuta nikitokwa machozi na kuweka mkono shavuni.
Mara nyingi msichana wangu wa kazi alikuwa akinishtua na kutaka kujua sababu ya mimi kuwa vile. Siku hiyo tena aliniuliza:
“Dada una tatizo gani?”
“Nipo sawa.”
“Hapana dada si mara ya kwanza kukuona hivi, mara nyingi ukiwa peke yako unakuwa umeshika tama, machozi yanakutoka kisha unatikisa kichwa na kufuta machozi.”
“Mmh! Mdogo wangu ya dunia.”
“Yapi dada, mbona mimi yangu nimemwachia Mungu?”
“Ni kweli mdogo wangu, lakini langu linanitesa kila nikilikumbuka, kwa akili ya kawaida unaweza kulidharau lakini langu ni donda linalonitonesha kila mara.”
“Kwani dada una tatizo gani?” Mariamu aliniuliza akiwa ananitazama kwa jicho la huruma.
SASA ENDELEA...

Kwa vile alikuwa msichana aliyepevuka nilimweleza yote. Baada ya kunisikiliza alinipa pole.
“Duh! Dada unataka kuniambia mpaka leo hujajua sababu ya kupewa talaka?”
“Sijajua, na kibaya dua na maombi yangu yote yalikuwa kwa mume wangu. Hata katika maisha yetu hatukuwahi kugombana.”
“Basi si angekuambia kuliko kukupa mtihani usioujua?”
“Wee acha, kila nikikumbuka moyo unaniuma sana.”
“Lakini dada mbona Mungu kasikia kilio chako.”
“Mungu hajasikia kilio changu, bali kanipandisha kutoka chini lakini jibu la swali langu bado sijalipata.”
“Ungeachana nalo tu.”
“Najitahidi kufanya hivyo, lakini moyo wangu umekataa kupinduka.”
“Na mama anasemaje?”
“Mama ajue nini ikiwa talaka kanipa Beka kwani mama yangu ni familia ya mtalaka wangu?”
“Mmh! Lakini Mungu mkubwa ipo siku utasahau.”
“Ndicho ninachokiomba usiku na mchana mawazo juu ya mtalaka wangu yafutike kichwani mwangu.”
Maisha yaliendelea huku nikiwa sina pingamizi la kumpa mwili wangu mzee Sambi kwa vile sikuona sababu ya kumnyima kwani tuliishi kama mke na mume.
Siku moja tukiwa kitandani tumejilaza, ilikuwa siku ya mapumziko, ambazo mzee Sambi alizitumia kuja kwangu kushinda mpaka jioni.
“Mwaija,” aliniita kwa sauti ya chini.
“Abee.”
“Unayaonaje maisha?”
“Namshukuru Mungu mazuri.”
“Kuna kitu umepungukiwa?”
“Kinaweza kuwepo, lakini kwa sasa nina imani hakuna.”
“Vipi kuhusu ombi langu?”
“Lipi?” nilimuuliza huku nikijigeuza na kumtazama.
“Kuhusu mtoto.”
“Hakuna tatizo.”
“Upo tayari kuzaa na mimi?”
“Ndiyo.”
“Asante sana mpenzi wangu.”
“Ni wajibu wangu kukufurahisha mpenzi wangu kwa vile nawe unanifurahisha. Mungu akijalia nitakuzalia watoto hata kumi.”
“Usiniambie!”
“Tatizo lipo wapi baba ana uwezo na malezi si tatizo.”
“Mi nataka wawili kwanza.”
“Basi baba jitahidi kuwatafuta hao watoto.”
“Kwa furaha hata kabla ya kuwapata leo nitakupa hundi ya milioni kumi kama asante ya kuonesha una mapenzi ya dhati na mimi.”
Siku ile alinipa hundi ya milioni kumi, nami mara moja nikaanza kuitega mimba kwa kutumia kalenda ya kupata mtoto. Sikuwa mvivu siku zote za hatari nilijitahidi kukutana na mpenzi wangu.
Siku zilikatika bila kuonekana dalili za kushika ujauzito kitu kilichonishtua sana. Mwezi wa tatu ulipokatika nilijikuta nikipata wazo labda mzee Sambi ndiye mwenye tatizo na kumsingizia mkewe ndiye hazai.
Siku moja tukiwa tumejilaza kitandani, nilimdodosa mzee Sambi juu ya mkewe kushindwa kumzalia mtoto.
“Samahani mpenzi.”
“Bila samahani.”
“Eti tatizo la mke mwenzangu lilikuwa nini?”
“Tatizo gani?”
“La kushindwa kubeba mimba?”
“Ni historia ndefu haina muhimu kwa sasa.”
“Hapana, nina sababu zangu.”
“Sababu zipi?”
“Naomba kwanza uniambie.”
“Sababu kubwa mke wangu hana mfuko wa uzazi.”
“He! Tatizo nini?” nilishtuka kusikia vile.
“Alipata matatizo kwenye mfuko wa uzazi ukaondolewa.”
“Wakati huo mkiwa ndani ya ndoa?”
“Hapana.”
“Ina maana tatizo alilipata kabla ya ndoa?”
“Ndiyo.”
“Sasa kipi kilichokufanya umuoe wakati ukijua kabisa hazai na kukufanya sasa hivi uhangaike nje ya ndoa kutafuta mwanamke akuzalie mtoto?”
“Ni historia ndefu, mke wangu kabla ya tatizo hilo alikuwa mpenzi wangu wakati huo alikuwa mwanafunzi wa kidato cha sita. Wakati anajiandaa na mtihani alijigundua ana ujauzito.”
“Sasa wewe unajua mwanafunzi kwa nini hamkutumia kinga au kalenda ya mzunguko wa hedhi?”
“Wee acha huwezi kuamini, mke wangu nimeanza naye mapenzi tangu akiwa kidato cha tatu. Muda wote tulikuwa makini, hata sikumbuki tulikosea wapi.”
“Ehe!”
“Kwa vile alikuwa amebakiza miezi mitano afanye mtihani na ujauzito ulikuwa wa miezi mitatu ilibidi tufanye mpango wa kutoa.”
“Mmh! Ikawaje?”
“Kumbe aliyemtoa hakumsafisha vizuri, baada ya muda alianza kusumbuliwa na tumbo. Hata mtihani wa kidato cha sita aliufanya kwa shida. Hatukujua tatizo mapema kutokana na yeye kusafiri kwenda kwa bibi yake kwa miezi mitatu.
“Huko alipokwenda hali ilizidi kuwa mbaya na kulazwa hospitali. Alinieleza alisafishwa tena na kupata nafuu. Lakini ugonjwa wa tumbo ndiyo ukawa tatizo lake.
“Aliporudi Dar nilimchukua na kumpeleka kwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake. Vipimo vilionesha mfuko wa uzazi umeharibika na hakukuwa na njia yoyote ya kumnusuru na hali yake zaidi ya kutolewa.
“Mke wangu alilia sana huku akinilaumu nimemuharibia maisha yake. Sikuwa na jinsi zaidi ya kumuahidi kumuoa na kuishi naye mpaka Mungu atakapomchukua mmoja wetu.
“Basi ilinibidi nijikomiti na kujifunga kwa maandishi kwamba sitamuacha.
“Baada ya miaka saba alitaka tuasili mtoto, lakini nilimshauri kwa nini nisitafute mtoto wa nje ya ndoa. Mwanzo alikataa katakata kwa kuamini mwanamke nitakayezaa naye atamdharau kwa vile hawezi kuzaa.
“Nimbembeleza na kumweleza siri ile itabakia kati yake na mimi na nusu ya mali yangu nitampa yeye ila niwe na mtoto wa damu yangu kutoka kwa mwanamke wa nje atakayenizalia kwa mkataba.
“Ilibidi tukubaliane atakayeingia ndani ya nyumba yetu ni mtoto na si kitu kingine. Hapo ilibidi nianze kusaka mtu wa kuzaa naye. Kwa kweli kila niliyemgusia kuzaa naye alitaka ndoa.
“Kwangu ilikuwa vigumu kutokana na masharti ya mke wangu. Ndipo nilipokutana na dada yako ambaye nilimuahidi kama atakubali kunizalia mtoto ningempa zawadi kubwa.
“Tatizo lingine ambalo lilimtibua dada yako na ndiyo chanzo cha kunifukuza lilikuwa kumwambia kama atakuwa tayari tukapime. Hicho ndicho kilichosababisha mimi na dada yako tukosane.
“Lakini nashukuru sasa hivi nimeangukia kwenye mikono salama.”

Itaendelea ijayo Jumamosi..................
 
Back
Top Bottom