Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 274
- 486
"Habari yako kaka George,
Mimi ni mfuatiliaji sana wa post zako. Naomba unipostie na mimi ili watu wasijue kuwa ni Mimi ila nitasoma comments.
Mimi kuna jambo linanitatiza naomba ushauri wako na hata ukipost kweye page zako itakuwa vizuri pia na nitakuja kusoma ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali.
In short ipo hivi juzi hapa nilishika simu ya mama kuna video za send-off ya dada yangu nilikuwa naangalia. Dada yetu wa kwanza ameolewa wiki iliyopita.
Baada ya kuangalia ile video kwenye simu ya mama nilivutiwa kuangalia na picha nyingine mbalimbali kwenye simu yake ndipo nilipojua mengi ambayo sikuwa najua kabla.
Niliona picha kadhaa zenye mikao ya kimahaba ambazo mama alipiga na kijana anaye endesha bodaboda yetu.
Kuna nyingine wamepiga wakiwa chumbani na kwa mazingira nadhani ilikuwa ni guest house kama sijakosea maana mhhm!!
Baada ya kuona zile picha nikaona ngoja niende upande wa messages labda nitagundua mengineyo.
Kweli bwana! Nikikutana na SMS kibao za mahaba. Mala mama anamshukuru yule kijana kwa penzi tamu, mala yeye ndio anamfikisha vizuri kuliko baba na kadhalika.
Imeniuma sana kiukweli kwasababu hata ndani kwetu kwasasa hakuna maelewano mazuri kati ya mama na baba.
Mala zote katika magomvi yao nilikuwa zaidi upande wa mama na nilikuwa nikidhani labda baba anamuonea mama lakini loooh!! Mama anachomfanyia baba sijaenda kwakweli.
Hapa nawaza sijui nimwambie baba kwa kile nilichokiona kwenye simu ya mama? au nimwambie mama kuwa anachofanya sio kizuri? au nimwambie yule bodaboda aachane na mama? au nikae kimya tu?!!
Dah!! Sielewi kwakweli nifanye nini. Naomba ushauri wako na yeyote atakayeguswa na kisa hiki anishauri nifanye nini ili kutatua changamoto hii.
Naitwa Glory Tesha kutoka Arusha - Tanzania."
#No_learnig_No_earning
So We Have To Learn.
Content By Mr George Francis