Mkuu nipo tofauti nawewe kidogo japokuwa unaonekana umesoma sana vitabu vya dini...Nitakujibu kwa machache:
1. Laana huwezi wewe kumlaani mtu ikampata kama wewe huna laana. Mtu yeyote mdhambi, tiyari kisha laaniwa. Hawezi kujikinga laana kwani laana tiyari ipo juu yake.
2. Hawezi kwenda kumuomba huyo mamake aliyekwisha kufa kwa sababu, Marehemu sasa kishatoka katika mwili na yeye yupo katika mwili. Utamuombaje asiyekuwepo pamoja nasi chochote?? Naomba uelewe kwamba ukiisha kufa, wewe moja kwa moja upo mahali pa kungojea hukumu tu. Kitabu cha Waebrania 9 : 27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja na baada ya kufa hukumu.
Hapo hakuna mahali popote ambapo panasema ati tunaweza kupatana naye tena.
3. Nimesema, Laana hutoka kwa mwenye laana, Mungu ndiye mwanzo wa kila kitu unachokijua, na hata usichokijua. Yeye ndiye Alfa na Omega. Mwanzo na Mwisho. Yaani, hata hiyo laana ni mali yake. Hupenda kufanya atakavyo. Alikuambia, Ukifanya hivi, HAKIKA laana itakupata. Ukifanya hivi, HAKIKA baraka zitakupata. Je, kuna mtu awezaye kumuambia mwingine hivyo?? Jibu ni, HAPANA. Ni Mungu tuu awezaye kusema nayo ikawa.
4. Kilicho nyuma ya laana nimekuambia kuwa, Kama mtu yupo chini ya laana yaani ni mdhambi, huyo akikulaani wewe uliye chini ya laana yaani mdhambi, utallanika.
5. Niliposema; Ampokee Yesu awe Bwana na Mwokozi wake ni kuwa; Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu. Imeandikwa; Amelaaniwa yeye aliyetundikwa juu ya mti. Hivyo Yesu alilaaniwa kwa ajili yetu ili sisi tuliokuwa chini ya kongwa la dhambi tuwe huru kwa kulipiwa hilo deni letu na uhai wake Yesu Kristo.
Njoo PM kwa mafundisho zaidi.
Mtu yoyote anaweza kukulaani katika haki yake.. ukiachana na mambo ya kidunia katika roho na kweli mungu ametuumba kila mtu na haki yake na sisi sote ni watoto wake..
Ikitokea umemdhulumu mtu haki yake(ukamkwamisha katika mambo yake au kumuweka katika wakati mgumu) na muhusika akasikitika sana.. basi ndugu yangu amini laana lazima ikuandame na mungu atakusamehe kupitia kwa huyo mtu uliyemdhulumu(umuombe msamaha kwa njia unayoijua wewe moyo wake uwe mweupe kabisa)
tofauti na hapo maisha yako yatakuwa magumu sana