Mama yake alimuachia laana 'kamlalia vibaya', mambo yake yanamuendea kombo

strategist22

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
655
594
Wanabodi,humu nimekuwa nikijifunza mambo mengi sana toka nimejiunga hapa 2014 .Naamini kuna watu makini wenye uelewa mkubwa wa elimu ya ulimwenguni huku ,elimu au maarifa yasiyosemwa au yaliyopuuzwa na watu wengi zama hizi.

Naamini swala hili litapata ufumbuzi kama mengine mengi yanayoletwa humu. Nina mambo machache na hitaji kujifunza hapa, haya maswali yanaulizwa sana sana,wengi wanajiuliza hasa wakifiwa.Dini nyingi zimejaribu kujibu maswali haya ,nahitaji kujua zaidi ya majibu hayo.Mimi ni Mkristo,nimesoma na dini nyingine Kwa kiasi chake.

Wiki iliyopita nilirudi nyumbani,kwa zaidi ya miaka miwili hawakuniona.Nilipita kusalimia ndugu na jamaa,nilipita kwa baba wa rafiki yangu,kumjulia hali pia kumpa pole ,mke wake alifariki mapema mwaka 2018. Pamoja na hayo nilihitaji kujua alipo rafiki yangu,toka January nimekuwa nikimpigia simu bila mafanikio.

Rafiki yangu alikuwa anajihusisha na biashara na ufugaji,halipiga hatua sana.Tulimuona kijana wa mfano,kupambana na maisha,lakin hakuwa na mahusiano mazuri na wazazi wake.Mama yake alimwambia,asisogelee jeneza lake akifa.Saivi ni mwaka na miezi kadhaa kilakitu amekwama ,amerudi hatua nyingi nyuma. Kama kapagawa ,anashinda ndani au la maporini .

Mazungumzo na baba yake kwa ufupi ni kuhusu matatizo ya rafiki yangu na utatuzi wake.anasema
"Mwenzako yupo gizani,ameandamwa na mikosi,Mama yake amemlalia vibaya huko,ananung'unika hata kwenye msiba hakumuona.Mshauri rafiki yako akaombe msamaha ,pia akubali kufanyiwa mila nyingine atoke kizani,Mimi hataki hata kuniona,nimemtumia wadogo zake,aje nyumbani hataki ,nimemfata kwake mara4 anajifungia ndani"

Baada ya mazungumzo hayo nikajaa na maswali haya.
1:Kudharau au kupuuza mila kunaweza kukuletea matatizo?
2;Je wafu wanaweza kuzuia mambo yetu?kwa namna gani?

3:Je wafu wanasikia ? Wanaona?

4:Je wanasamehe?

5:Je wanachukia?nini kinafanya wachukie?

6:Je wanaweza kutusaidia?kwa jinsi gani?

7;Wapo wapi ?wanafanya nini?

8:Je tunaweza kuonana nao?

9:Ongeza cha ziada,kama kipo kupanua zaidi mada.

NB:Nahitaji kujua , haya nje ya mfumo wa dini,watu wanaelewa nini ? wanafanya nini?, Katika mazingira kama haya.

Asanteni
 
Kwanza; Laana huwatoka walio laaniwa na hiyo laana huwapata walio chini ya laana. Hivyo ndivyo laana hutokea. Pili; Kama kweli alimtenda vibaya mamake hadi mamake kufikia kumwapiza kuwa asifike kwenye mazishi yake, alitakiwa apatane naye kabla hajafa. Mapatanisho hutokea baina ya mtu na mtu sio mtu na mzimu. Mzimu ni roho hivyo haiwezi patana na mtu katika kitu kilichotokea kwenye mwili. Neno la Mungu linasema; Patana na mshitaki wako kabla hajakufikisha kwa kadhi.
Sasa, Kwa kuwa hakujali kupatana na mamake akiwa hai alikosa nafasi ya kulimaliza hilo jambo hata kwa kutumia watu wengine. Huyo mama ka angalikataa, na kutokana na juhudi kali za kuomba msamaha, hiyo laana isingalimpata.
Ushauri;
Huyo rafiki yako, kwamza akubaliane na hiyo hali kuwa; Nilimkosea mamangu ambaye sasa hayupo. Amwombe babake radhi na kuacha kuzingua zaidi. Nasema, aombe radhi ila asikubali kuburuzwa kwa kupigwa faini zisizo na kichwa wala mkia. Awaambie hao wazee kuwa, niliyemkosea hayupo hivyo naomba asitokee mwingine kuvaa nafasi ya mama.
Jambo jingine;
Wafu hawana sehemu na sisi tulio hai. Huyo aliyekufa hataweza kukutingisha. Mpokee Yesu awe Bwana na Mwokozi naye atakuponya na milaana hiyo yote
 
Umemaliza Kila kitu
 
Tuache kutafuta sababu za kuhalalisha kushindwa kwetu kwa kutafuta watu wa kuwatupia lawama tufanye kazi kwa nguvu tuangalie ni wapi tunakosea na sio kusema blah blah za laana hizi ni soga tu za vijiweni hakuna kitu kama hicho, Mwambie jamaa ake ajitafakari ni wapi anakosea mtu wa hivi unaweza kuta anafuja pesa vibaya amejawa na kiburi, hashauriki lakini anasema amelaaniwa
Laana zipo mkuu...Usijakumfanyia ubaya mama yako akakulaani nakwambia Hutafanikiwaa kamwee!! Wazazi ni Mungu wa pili hasa mama walahi chamoto utakionaa..
 
Mkuu mimi mshua na maza ndio watu namba moja kwangu na huwa nashangaa inakuwaje mtu ashindwe kuelewana na wazazi wake hadi wamtakie mabaya
Kwenye maisha watu wanapitia mambo mbalimbali mkuu. Cha muhimu ni kuwasikiliza na kuwasaidia sio kuwahukumu
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom