Mama yake alimuachia laana 'kamlalia vibaya', mambo yake yanamuendea kombo

Kwanza; Laana huwatoka walio laaniwa na hiyo laana huwapata walio chini ya laana. Hivyo ndivyo laana hutokea. Pili; Kama kweli alimtenda vibaya mamake hadi mamake kufikia kumwapiza kuwa asifike kwenye mazishi yake, alitakiwa apatane naye kabla hajafa. Mapatanisho hutokea baina ya mtu na mtu sio mtu na mzimu. Mzimu ni roho hivyo haiwezi patana na mtu katika kitu kilichotokea kwenye mwili. Neno la Mungu linasema; Patana na mshitaki wako kabla hajakufikisha kwa kadhi.
Sasa, Kwa kuwa hakujali kupatana na mamake akiwa hai alikosa nafasi ya kulimaliza hilo jambo hata kwa kutumia watu wengine. Huyo mama ka angalikataa, na kutokana na juhudi kali za kuomba msamaha, hiyo laana isingalimpata.
Ushauri;
Huyo rafiki yako, kwamza akubaliane na hiyo hali kuwa; Nilimkosea mamangu ambaye sasa hayupo. Amwombe babake radhi na kuacha kuzingua zaidi. Nasema, aombe radhi ila asikubali kuburuzwa kwa kupigwa faini zisizo na kichwa wala mkia. Awaambie hao wazee kuwa, niliyemkosea hayupo hivyo naomba asitokee mwingine kuvaa nafasi ya mama.
Jambo jingine;
Wafu hawana sehemu na sisi tulio hai. Huyo aliyekufa hataweza kukutingisha. Mpokee Yesu awe Bwana na Mwokozi naye atakuponya na milaana hiyo yote
Ahsante
 
Hivi haya mambo ya laana ni afrika tu au wazungu wanayo???
Hiyo ni kwa viumbe wanaadamu wote. Tofauti ya wenzetu wazungu wako zaidi kama wanyama kuliko binadamu. Huwa hawako karibu na watoto zao kama tulivyo sisi. Wao hufukuza watoto wao wa kuzaa nyumbani kama kuku anavyofanya kwa wanawe akipata vifaranga. Hiyo hufanya ule uwezekano wa kutoa laana kuwa finyu kwa kuwa kila mmoja yuko kivyake.
 
Kwanza; Laana huwatoka walio laaniwa na hiyo laana huwapata walio chini ya laana. Hivyo ndivyo laana hutokea. Pili; Kama kweli alimtenda vibaya mamake hadi mamake kufikia kumwapiza kuwa asifike kwenye mazishi yake, alitakiwa apatane naye kabla hajafa. Mapatanisho hutokea baina ya mtu na mtu sio mtu na mzimu. Mzimu ni roho hivyo haiwezi patana na mtu katika kitu kilichotokea kwenye mwili. Neno la Mungu linasema; Patana na mshitaki wako kabla hajakufikisha kwa kadhi.
Sasa, Kwa kuwa hakujali kupatana na mamake akiwa hai alikosa nafasi ya kulimaliza hilo jambo hata kwa kutumia watu wengine. Huyo mama ka angalikataa, na kutokana na juhudi kali za kuomba msamaha, hiyo laana isingalimpata.
Ushauri;
Huyo rafiki yako, kwamza akubaliane na hiyo hali kuwa; Nilimkosea mamangu ambaye sasa hayupo. Amwombe babake radhi na kuacha kuzingua zaidi. Nasema, aombe radhi ila asikubali kuburuzwa kwa kupigwa faini zisizo na kichwa wala mkia. Awaambie hao wazee kuwa, niliyemkosea hayupo hivyo naomba asitokee mwingine kuvaa nafasi ya mama.
Jambo jingine;
Wafu hawana sehemu na sisi tulio hai. Huyo aliyekufa hataweza kukutingisha. Mpokee Yesu awe Bwana na Mwokozi naye atakuponya na milaana hiyo yote
Asante kwa mchango wako muhimu,baba yake hana tatizo naye kabisa na amemsamehe, anataka akamwombe msamaha mama yake na kufanyiwa mila nyingine,hakuingia ndani katika hili yani nini kitafanyika.

Samahani umeanza kwa kusema"laana huwatoka walio laaniwa na hiyo laana huwapata walio chini ya laana" Kwa kuwa umehusisha neno la Mungu,nafikiri sio sahihi kusema hivo maana hata Mungu ametamka laana maranyingi"umelaaniwa","alaaniwe"

Ikiwa wafu hawana sehemu na sisi tulio hai nini kipo nyuma ya laana? Kifanyacho watu kupatwa au kusumbuliwa na laana.

Mwisho,ushauri wako wa kumpokea bwana na mwokozi,nitamfikishia.

Shukrani.
 
Hivi kwann aya mambo yapo africa tu nimekuwa nikisoma case nyingi za wazungu wakigombana na wazazi wao kiasi cha kukataa kabisa kama sio wazazi wao lakini hakuna hata mmoja nimeona analalamika kuwa hajafanikiwa sababu ya laana ya wazazi wake?

Kuna shida mahali nadhani ili swali limekaa kwenye mindset zaidi halina uhalisia hata kidogo jamaa ana psychological issue na wala sio laana kama anavyoamini
wazungu wako huru sana na hueshimu maamuzi ya mtu hivyo hata kama amkane mama yake wala hana muda wa kumuwekea kinyongo (maana ana heshimu maamuzi yake na hana muda wa kumtaka maana anajitosheleza)

huku kwetu hali ya ugumu wa maisha na vile mama zetu wana hangaika kutulea akikulaani lazima udate

kama tunavyo amini dhuluma ya jasho la mtu si nzuri ndivyo laana iko ivyo ila hii ya mama haiitaji uamini ama laah hii ipo.

kwani biblia imesemaje juu ya kupata kheri na baraka dunia si lazima umuheshimu baba na mama kama usipo waheshimu jua heri na baraka zinakupita (ndio tunaita laana)
 
Wanabodi,humu nimekuwa nikijifunza mambo mengi sana toka nimejiunga hapa 2014 .Naamini kuna watu makini wenye uelewa mkubwa wa elimu ya ulimwenguni huku ,elimu au maarifa yasiyosemwa au yaliyopuuzwa na watu wengi zama hizi.

Naamini swala hili litapata ufumbuzi kama mengine mengi yanayoletwa humu. Nina mambo machache na hitaji kujifunza hapa, haya maswali yanaulizwa sana sana,wengi wanajiuliza hasa wakifiwa.Dini nyingi zimejaribu kujibu maswali haya ,nahitaji kujua zaidi ya majibu hayo.Mimi ni Mkristo,nimesoma na dini nyingine Kwa kiasi chake.

Wiki iliyopita nilirudi nyumbani,kwa zaidi ya miaka miwili hawakuniona.Nilipita kusalimia ndugu na jamaa,nilipita kwa baba wa rafiki yangu,kumjulia hali pia kumpa pole ,mke wake alifariki mapema mwaka 2018. Pamoja na hayo nilihitaji kujua alipo rafiki yangu,toka January nimekuwa nikimpigia simu bila mafanikio.

Rafiki yangu alikuwa anajihusisha na biashara na ufugaji,halipiga hatua sana.Tulimuona kijana wa mfano,kupambana na maisha,lakin hakuwa na mahusiano mazuri na wazazi wake.Mama yake alimwambia,asisogelee jeneza lake akifa.Saivi ni mwaka na miezi kadhaa kilakitu amekwama ,amerudi hatua nyingi nyuma. Kama kapagawa ,anashinda ndani au la maporini .

Mazungumzo na baba yake kwa ufupi ni kuhusu matatizo ya rafiki yangu na utatuzi wake.anasema
"Mwenzako yupo gizani,ameandamwa na mikosi,Mama yake amemlalia vibaya huko,ananung'unika hata kwenye msiba hakumuona.Mshauri rafiki yako akaombe msamaha ,pia akubali kufanyiwa mila nyingine atoke kizani,Mimi hataki hata kuniona,nimemtumia wadogo zake,aje nyumbani hataki ,nimemfata kwake mara4 anajifungia ndani"

Baada ya mazungumzo hayo nikajaa na maswali haya.
1:Kudharau au kupuuza mila kunaweza kukuletea matatizo?
2;Je wafu wanaweza kuzuia mambo yetu?kwa namna gani?

3:Je wafu wanasikia ? Wanaona?

4:Je wanasamehe?

5:Je wanachukia?nini kinafanya wachukie?

6:Je wanaweza kutusaidia?kwa jinsi gani?

7;Wapo wapi ?wanafanya nini?

8:Je tunaweza kuonana nao?

9:Ongeza cha ziada,kama kipo kupanua zaidi mada.

NB:Nahitaji kujua , haya nje ya mfumo wa dini,watu wanaelewa nini ? wanafanya nini?, Katika mazingira kama haya.

Asanteni

Mwambie akaombewe tu kila kitu kinakwisha
 
Kwanza; Laana huwatoka walio laaniwa na hiyo laana huwapata walio chini ya laana. Hivyo ndivyo laana hutokea. Pili; Kama kweli alimtenda vibaya mamake hadi mamake kufikia kumwapiza kuwa asifike kwenye mazishi yake, alitakiwa apatane naye kabla hajafa. Mapatanisho hutokea baina ya mtu na mtu sio mtu na mzimu. Mzimu ni roho hivyo haiwezi patana na mtu katika kitu kilichotokea kwenye mwili. Neno la Mungu linasema; Patana na mshitaki wako kabla hajakufikisha kwa kadhi.
Sasa, Kwa kuwa hakujali kupatana na mamake akiwa hai alikosa nafasi ya kulimaliza hilo jambo hata kwa kutumia watu wengine. Huyo mama ka angalikataa, na kutokana na juhudi kali za kuomba msamaha, hiyo laana isingalimpata.
Ushauri;
Huyo rafiki yako, kwamza akubaliane na hiyo hali kuwa; Nilimkosea mamangu ambaye sasa hayupo. Amwombe babake radhi na kuacha kuzingua zaidi. Nasema, aombe radhi ila asikubali kuburuzwa kwa kupigwa faini zisizo na kichwa wala mkia. Awaambie hao wazee kuwa, niliyemkosea hayupo hivyo naomba asitokee mwingine kuvaa nafasi ya mama.
Jambo jingine;
Wafu hawana sehemu na sisi tulio hai. Huyo aliyekufa hataweza kukutingisha. Mpokee Yesu awe Bwana na Mwokozi naye atakuponya na milaana hiyo yote

Cc Kingsmann
 
Tumemabiwa kwenye Quran,usiabudu Mungu mwingine.mstari unaendelea na wafanyieni hisani(wema wazazi wawili)na muwakirimu yatima na masikini..ukitaka baraka na amani hapa dunia waangalie sana wazazi,baraka zao ni kubwa sana hata kama huna kitu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom