Mama Samia ni mgombea mpya kabisa wa CCM 2025 - 2030

Issue siyo kuwa mgombea mpya au wa zamani. Issue wanayoulizia watu ni kwa nini mchakato wa kumpata ulikuwa wa magumashi? Kwa nini hakukuwa na mchuano wa kumpata kama ilivyokuwa 2015 alivyopatikana Magufuli (rip)?
 
Ibara ya 37(5) – Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais

"Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano."

---

🗳️ Ibara ya 40(4) – Haki ya kuchaguliwa tena

"Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu, ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu."

📌 Mfano halisi: Rais Samia Suluhu Hassan alirithi kiti cha urais Machi 2021 baada ya kifo cha Rais Magufuli, akiwa amebakiza takriban miaka minne na nusu ya muhula. Kwa hiyo, ataruhusiwa kugombea urais mara moja tu katika uchaguzi ujao.
Jitekenye!
 
Kwa nini? Kwa sababu hakuwahi kugombea kabisa nafasi hiyo (ya kupeperusha bendera) na kuhudumu.

Tukumbuke Kila mgombea aliyeteuliwa alikuja na "falsafa" yake ya kuongoza nchi.
  1. NYERERE - Siasa ya ujamaa na kujitegemea (falsafa mama).
  2. MWINYI - Ruksa.
  3. MKAPA - Ukweli na uwazi.
  4. KIKWETE - Ari mpya, nguvu mpya na Kasi mpya.
  5. MAGUFULI - Hapa kazi tu.(majungu peleka ukawa😂😁🤣).
Baada ya kufariki MAGUFULI ikabidi Mama SAMIA asaidie kufikisha jahazi ukingoni (kikatiba) ndio maana aliiendeleza falsafa ya Rais husika (hayati) kwa kauli KAZI IENDELEE.

Kwa hiyo Rais wa awamu ya 6 ataanza kazi rasmi 2025 - 2030 ambaye ni MAMA DR.SAMIA SULUHU HASSANI kwa kuchaguliwa kihalali na wajumbe wote halali.

HONGERA SANA MAMA !!!

Tukumbushane kidogo kipindi cha nyuma Urais ulizingatia pande mbili "kipindi hiki akitokea bara, kipindi kinachofuata atatokea Zanzibar na kinyume chake" lakini kwa Sasa sheria hii haizingatiwi sana.

Ni utaratibu tu mtakao kubaliana kwa pamoja kulingana na nyakati hizo (huko mbeleni).

Mnavyomlaumu mama wa watu Kama vile amejiteua kipindi hiki kwa nini msingepinga pale pale ukumbini.

ACHENI UNAFIKI.

Namalizia kusema kwamba mama yupo kihalali Hadi 2030 Kama mlivyokubaliana.

KATIKA KUSAKA URAIS KWA MARA YA KWANZA (awamu ya 6) MAMA SAMIA ATAKAPOZUNGUKA NCHI NZIMA ATAKUJA NA "FALSASA" YAKE ITAKAYOIONGOZA NCHI KUENDANA NA KARNE YA 21.

Wananchi tunaisubiri kwa hamu sana "falsafa" hiyo mpya itakayotambulishwa "soon".

Nitarudi baadaye kidogo.........

Ahsanteni.
Hofu imekujaa!
 
kwa nini mnataka kulazimisha vitu, ninyi endeleeni, sisi tunamwachia Mungu, kama Mungu anataka aendelee kuongoza hakuan wa kuzuia, ila kama Mungu kaamua vingine msipoteze muda. ila kitendo cha kufuta makanisa na kuacha misikiti wazi kimemletea doa kubwa sana.
Mungu yupi unaye mtaja..? Na nikuulize kitu mkuu. Samia alipitishwa kule CCM kwa kura zipi..? Na sera zake ni zipi ..? Acheni kivuruga nchi kwa uroho wenu.
 
Ibara ya 37(5) – Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais

"Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano."

---

🗳️ Ibara ya 40(4) – Haki ya kuchaguliwa tena

"Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu, ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu."

📌 Mfano halisi: Rais Samia Suluhu Hassan alirithi kiti cha urais Machi 2021 baada ya kifo cha Rais Magufuli, akiwa amebakiza takriban miaka minne na nusu ya muhula. Kwa hiyo, ataruhusiwa kugombea urais mara moja tu katika uchaguzi ujao.
Umenena vyema mkuu,
Tatizo ni kuwa hawaheshimu hiyo Katiba na hawana haya hata kidogo
 
Kwa nini? Kwa sababu hakuwahi kugombea kabisa nafasi hiyo (ya kupeperusha bendera) na kuhudumu.

Tukumbuke Kila mgombea aliyeteuliwa alikuja na "falsafa" yake ya kuongoza nchi.
  1. NYERERE - Siasa ya ujamaa na kujitegemea (falsafa mama).
  2. MWINYI - Ruksa.
  3. MKAPA - Ukweli na uwazi.
  4. KIKWETE - Ari mpya, nguvu mpya na Kasi mpya.
  5. MAGUFULI - Hapa kazi tu.(majungu peleka ukawa😂😁🤣).
Baada ya kufariki MAGUFULI ikabidi Mama SAMIA asaidie kufikisha jahazi ukingoni (kikatiba) ndio maana aliiendeleza falsafa ya Rais husika (hayati) kwa kauli KAZI IENDELEE.

Kwa hiyo Rais wa awamu ya 6 ataanza kazi rasmi 2025 - 2030 ambaye ni MAMA DR.SAMIA SULUHU HASSANI kwa kuchaguliwa kihalali na wajumbe wote halali.

HONGERA SANA MAMA !!!

Tukumbushane kidogo kipindi cha nyuma Urais ulizingatia pande mbili "kipindi hiki akitokea bara, kipindi kinachofuata atatokea Zanzibar na kinyume chake" lakini kwa Sasa sheria hii haizingatiwi sana.

Ni utaratibu tu mtakao kubaliana kwa pamoja kulingana na nyakati hizo (huko mbeleni).

Mnavyomlaumu mama wa watu Kama vile amejiteua kipindi hiki kwa nini msingepinga pale pale ukumbini.

ACHENI UNAFIKI.

Namalizia kusema kwamba mama yupo kihalali Hadi 2030 Kama mlivyokubaliana.

KATIKA KUSAKA URAIS KWA MARA YA KWANZA (awamu ya 6) MAMA SAMIA ATAKAPOZUNGUKA NCHI NZIMA ATAKUJA NA "FALSASA" YAKE ITAKAYOIONGOZA NCHI KUENDANA NA KARNE YA 21.

Wananchi tunaisubiri kwa hamu sana "falsafa" hiyo mpya itakayotambulishwa "soon".

Nitarudi baadaye kidogo.........

Ahsanteni.

Hizo zote ni bla bla kitu muhimu ni katiba za CCM na nchi.

Na kwa mujibu wa katiba hizo, Samia hakatazwi kugombea urais 2025. Ila akipata urais 2025 katiba ya nchi inamkataza kugombea urais 2035.

Kwa hivyo hakuna haja ya hadithi za bla bla nyingi. Samia anaruhusiwa kugombea urais kikatiba. Amd that is all that matters.

Habari nyingine za utamaduni, desturi, miiko, matambiko, kachezeni ngoma za jadi. Kama ni muhimu sana, ziwekeni kwenye katiba ya chama au hata ya nchi.

Pia mchakato wa kutafuta mgombea wa CCM 2025 umefanywa kwa style ya ambush na bila kufuata mantiki, possibly umevunja katiba..

Hili limeleta maneno mengi sana na kumfanya Samia kuonekana kaogopa upinzani mdani ya CCM katila kumtafuta mgomnea urais.
 
Haswaa !!!
Agiza kinywaji hapo kwa mangi nakuja kulipia 😂😁🤣👍 !!!
Samia anakatazwa na katiba ya sasa ya Tanzania kugombea urais mwaka 2035.

Soma katiba hata kidogo ujielimishe kuhusu urais Tanzania na ukomo wake.

Inapatikana bure online huhitaji hata kuinunua.
 
Mean itakua msimu wake wa kwanza 2025-2030 then 2030-2035?
Kwa katiba ya sasa 2025 - 2030 kama Samia atapata urais ndiyo utakuwa muhula wake wa mwisho kuwa rais.

Hili jambo liko wazi kwenye katiba ya Tanzania.

Ibara ya 40

"4) Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa
mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua
miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili,
lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au
zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu"

Ibara ya 37(5) inajumuisha makamu wa rais kupata kuwa rais kwa kifo cha rais.

Samia amekuwa rais kwa niaka zaidi ya mitatu, hivyo, ataruhusiwa kugombea urais mara moja tu mwaka 2025. 2035 hataruhusiwa kugombea urais tena.

Umeelewa?

Samia mwenyewe kashasema 2030 anarudi Kizimkazi hana ndoto za kuendelea kuwa rais.
 
Back
Top Bottom