mama salma huyoooo USA


Jamani,
Naomba kutofautiana na wanaosema kuwa hawana heshima kwa mwalimu wa primary na kuwa hao walimu ni wale waliofeli au sijui UPE.tUKUMBUKE TU KUWA SIYO WALIMU WOTE WA PRIMARY NI UPE au siyo kila mwalimu wa primary hajasoma vya kutosha.Hao wanaokandia walimu wa primary labda bahati mbaya sana walikumbwa na wimbi la hao walimu wa UPE ( most were indeed std seven leavers tena failures, na many started out as housegirls before "upgrading to teachers")...

Mimi binafsi nawaheshimu sana walimu wangu wa primary na wengine wao hadi sasa wana nafasi zao sehemu mbalimbali baada ya kubadili profession na hata kupandishwa vyeo.

Tukirudi kwa huyu mama yetu wa kwanza - mama Salma - binafsi namheshimu na sioni ubaya wa mwalimu wa primary kuwa na nafasi hiyo maana kila mtu kaandikiwa bahati yake.

Hata tukimkandia, tukamchambua, tukanuna..anabakia kuwa FL for the time being, na ataingia kwenye annals of history of this nation.
Kama vipi, basi tujilaumu kwa kuwachagua hao viongozi ambao hawatufai - tukaacha wale wanaofaa ( hii ni changamoto kwetu sote).
 
Last edited:

Sikuiona hii,"Hapana wala simpigii debe Mama Kikwete,Mimi kama walio wengi humu naufahamu vizuri uwezo mdogo wa Mama wa kujieleza hata kusoma" Nia yangu ilikuwa ni kutaarifu tu kuwa Mama yupo US kwa ziara inayohusu masuala ya Afya,na si kama Mkuu PDiddy alivyoiweka thread na kuonekana kuwa kaja Kutalii.Ni kweli kuwa Mama atakuwa msikilizaji tu kwenye Mkutano huo,kwa sababu baadhi ya First Ladies walioalikwa, wanashiriki kikamilifu katika suala zima la kutokomeza ukimwi na kumuendeleza Mwanamke wa Kiafrika.

Hata hivyo Mama ameandamana na Dr.Fatma Mrisho (Mwenyekiti wa TACAIDS) kutoka ofisi ya waziri Mkuu na Dr Donan Mmbando anayetoka Wizara ya Afya (Mkurugenzi wa Magonjwa ya Maambukizi),ambao ni Wataalamu katika masuala ya Magonjwa ya maambukizi na wanaharakati wa akina MAMA.Kwa maana hiyo uwakilishi wake (Mama Kikwete) haujapwaya!
 
Mwawado mkuu: kumradhi maana niliona kama unatetea kuwa huyu mama ni true activist atakayeshiriki kikamilifu. Lakini naomba niulize kuwa baada ya kuweka bayana kuwa ameenda na wataalam na ya kuwa atakuwa msikilizaji tu, sasa kulikuwa na haja gani kwake kwenda? Maana sasa hivi serikali ina upungufu mkubwa wa pesa lakini tunaona pesa zinatumika hovyo. Hao wataalam wawili wanatosha lakini wengine kutoka hao 15 au zaidi wameenda kufanya nini?
Ndo maana naendelea kusisitiza kuwa hii ni shopping expedition except for the 2 -3 wataalam!
 

Kwahiyo unanishawishi niamini JF kuna watu wanapotosha mambo?? so JF si sehemu salama kuna nzige vidudu mtu.au JF imekuwa kama maskani sehemu ya kupigia stories??
 
Kwahiyo unanishawishi niamini JF kuna watu wanapotosha mambo?? so JF si sehemu salama kuna nzige vidudu mtu.au JF imekuwa kama maskani sehemu ya kupigia stories??

Mkuu kwanza karibu sana hapa jamvini.!
Hapa mkuu watu wapo huru kujadili michango mbalimbali,fuatilia mijadala mingi watu watataka uambatanishe na uthibisho wako wa kitu unacho ongelea hapa si kijiweni eti unakurupuka tu na story za mitaani unakuja nazo hicho kitu hakipo utabanwa tu weka evidence.
 
Mama Salma ameongea jamani hata kama speech ameandikiwa kwa mujibu wa Gazeti la Daily News la leo , kasema wamewatrain watu wake kwa waume kwenye mambo ya kilimo bora, na pia wamesaidi wajawazito na magonjwa ya mama na mtoto mengine ni maelezo ya hayo hapo juu. na hao wakulima ni paprika farmers na wamesaidia watoto wa kike kupata elimu ya juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…