Kiby
JF-Expert Member
- Nov 16, 2009
- 6,900
- 4,624
Kanisani kwa mama kuna maombi yanaendelea pale ya wiki nzima kuombea amani ya nchi.
Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari.
Sina wasi wasi na maombi ila wasiwasi wangu unajitokeza pale ninapofikiri juu ya huyu mama kwamba ni kada wa ccm na mbunge wa kuteuliwa wa chama hicho.
Najiuliza huenda labda ana hofu ya kupoteza ulaji wa kisiasa ikiwa chama chake kitapoteza uchaguzi.
Amani anayoiombea nchini ni ipi? Kwani amani ya kweli na utuamo wa kizazi cha binadamu ni pale watu wanapopata mahitaji yao ya kimsingi ya kila siku.
Mama huyu anamwomba Mungu awatiishe watu ili wasiwafanyie vurugu wale wanaodhulumu haki zao za kimsingi, nae akiwa mmoja wao? Kwani ni mwajiriwa (mbunge) wa serikali inayompa mshahara na marupurupu yanayozidi milioni saba kwa mwezi huku akijua wazi sii haki haki hata kwa Muumba maana, mfanyakazi mwenzie wa kima cha chini analipwa sh. Laki moja na nne tu.
Hivyo atafurahi na kumwambia Mungu ahsante kwa amani, pale atakapoona watanzania wametiishwa kwa mkono wa chuma wa dola katikati ya umasikini wao wasifurukute?
Mama huyu ama chama chake kinatafsiri vipi dhana ya kutochanganya dini na siasa?
Nahisi huyu mama kaacha kazi ya kuwa wakala wa Muumba kwa kuitangaza imani yake iletayo amani ya kweli na sasa amegeuka kuwa muumini wa amani nje ya Imani, sawa na neno la Bwana Yesu aliposema, 'watakapokuwa wakisema Amani! Amani! Ndipo ubaya utawajilia ghafla'.