Mama Rwekatare na siasa za CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Rwekatare na siasa za CCM!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiby, Aug 29, 2010.

 1. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,195
  Likes Received: 1,000
  Trophy Points: 280
  Kanisani kwa mama kuna maombi yanaendelea pale ya wiki nzima kuombea amani ya nchi.
  Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari.

  Sina wasi wasi na maombi ila wasiwasi wangu unajitokeza pale ninapofikiri juu ya huyu mama kwamba ni kada wa ccm na mbunge wa kuteuliwa wa chama hicho.

  Najiuliza huenda labda ana hofu ya kupoteza ulaji wa kisiasa ikiwa chama chake kitapoteza uchaguzi.
  Amani anayoiombea nchini ni ipi? Kwani amani ya kweli na utuamo wa kizazi cha binadamu ni pale watu wanapopata mahitaji yao ya kimsingi ya kila siku.

  Mama huyu anamwomba Mungu awatiishe watu ili wasiwafanyie vurugu wale wanaodhulumu haki zao za kimsingi, nae akiwa mmoja wao? Kwani ni mwajiriwa (mbunge) wa serikali inayompa mshahara na marupurupu yanayozidi milioni saba kwa mwezi huku akijua wazi sii haki haki hata kwa Muumba maana, mfanyakazi mwenzie wa kima cha chini analipwa sh. Laki moja na nne tu.

  Hivyo atafurahi na kumwambia Mungu ahsante kwa amani, pale atakapoona watanzania wametiishwa kwa mkono wa chuma wa dola katikati ya umasikini wao wasifurukute?

  Mama huyu ama chama chake kinatafsiri vipi dhana ya kutochanganya dini na siasa?

  Nahisi huyu mama kaacha kazi ya kuwa wakala wa Muumba kwa kuitangaza imani yake iletayo amani ya kweli na sasa amegeuka kuwa muumini wa amani nje ya Imani, sawa na neno la Bwana Yesu aliposema, 'watakapokuwa wakisema Amani! Amani! Ndipo ubaya utawajilia ghafla'.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hiki kibibi ni kijasiria mali tu kisikupe tabu...hapo kinalinda akaunti yake ya benki tu
   
 3. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  :confused2:
  hahaaaa siyo kweli sema tu una chuki na imani yake, maana posti yako haina mahusiano na posti #1
   
 4. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mjasiria mali hahahahaha...Chama Kwanza...maombi ya sisiemu hayo....akaunti yake iko njema sema anataka kuilinda tu....Go Chadema Gooooooooooooooooo 2010 Slaa
   
 5. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 929
  Likes Received: 696
  Trophy Points: 180
  Kwa hili namshangaa JK anayekemea maaskofu na mashehe kuwa wasijiingize katika siaSa wakati chama chake kinateua viongozi wa dini kuwa wabunge.
   
 6. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  hayo majambo unayashabikia wewe, ukikosa la maana la kusema unakimbilia mambo ya udini udini. Mama Lwakwatare ana shughuli taofauti unaweza kumuongelea yoyote inayohusu maongezi yake, kwa akili kama yako, akiongelewa kwenye mambo ya kisiasa, mishipa ya ulokole inakusimama,nyie wasabato masalia mna kazi kweli..teh! teh! teh! teh!
   
 7. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Tena sana ... kilaghai, kindumila kuwili, kilafi na kiongo. Hamna cha uchungaji wala nini. Hivi ndivyo vile visadukayo vilivyoongelewa kwenya biblia.
   
 8. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,004
  Likes Received: 3,188
  Trophy Points: 280
  Hana lolote, anapiga kampeni tu.
  Flora mbasha kajiweka wazi kabisa.
   
 9. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,195
  Likes Received: 1,000
  Trophy Points: 280
  .
  Aliyepaswa kukataa cheo cha kisiasa ni mama au kama ameamua kuwa mwanasiasa basi angejiuzulu uchungaji. Hapo angekuwa hana kosa kabisa kwani angekuwa ameheshimu kwa vitendo kauli ya Bwana Yesu kuwa 'huwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja' Jk nae alichekecha na akatambua kuwa kama angemteua mchungaji wa kweli wa kondoo kuitumikia siasa angetolewa nje. Hata kama angefanya hivyo kwa imam asingekubaliwa ikiwa huyo imam ama mchungaji asingeachia ofisi ya kukuhani kwanza. Hivyo jk alitambua fika uchochoro wa kupitia ni kwa walikole ambao wengi wao(bali sii wote) ni wajasiria mali wa injili. Hivyo watakubali kuwa chini ya hili kongwa la kumkusanyia kondoo zake atakapofanikisha kupenyeza propaganda za ccm ndani ya kanisa.
   
 10. Wa mmoja

  Wa mmoja Member

  #10
  Aug 30, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dini na siasa wapi na wapi?!
  Awaombee na mafisadi waache kula mahela!
   
 11. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :mad2:
   
 12. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Naomba profile yake? Hivi alisharudiana na mumewe?au kusamehe ni kwa waumini wake tu. Wafanyakazi wake wanasema ana ushirikina wa kutisha.je amewahi kweli kuhusika na biashara za madini? Au anawauza misukule ya albino?
   
 13. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Wenye Roho huongozwa na Roho. Ingekuwa Roho Mtakatifu anayesema yuko ndani yake amemruhusu kumwongoza, asingefanya kitu kama hicho maana huyo Roho angenotice conflicting interest kwani yeye ni kada na mbunge wa ccm.
   
 14. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Ingekuwa chama kingine wangesema kinaingilia dini. Je tuseme thithiem wamekuwa kama CUF wanatafuta umaarufu kupitia majukwaa ya dini.
   
Loading...