Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

N a bado watataka facebook na google nazo zifutwe kwa mwendo huu,kuna vichwa huwa havifikiri kabisa
 
Seriously?
Alifikiria kweli kabla ya kupeleka hiyo hoja bungeni?
Kweli wabunge wa Tanzania ni zaidi ya wanavyoonekana.
 
Ukitaka kuwa Kiongozi Borai, ruhusu njia mbali mbali za kutolea malalamiko ili uyatumie kujirekebisha, ukizifunga huwezi kuelewa watu wako wanawaza nini, na hapo utakuwa hatarini zaidi.
 
hili swala la umiliki mbona ilisha wekwa hadharani siku mingi na inajulikana nani hasa mmiliki wake au ndi wanataka tu wapoteze mda kujadili mambo mengine na kuacha mambo muhimu yanayo gusa taifa kwa ujumla.

Mmiliki wa JF anawahusu nini? kama kuna kosa JF imelifanya waiburuze mahakamani then polisi wataambiwa wamtafute alipo, hiki kimama nakichukia sana, bifu zake na kakobe anataka azihamishie JF. Ukisikia watu walafi ni huyu mama.. hebu fikiria sadaka usimamie mwenyewe, Ada za shule usimamie mwenyewe, posho za bunge usimamie mwenyewe hivi ni kweli mungu anafurahishwa na hili???????????
 
Anaogopa siri zake zitafichuka kama waumini wake wataingia JF
 
Mama Lwakatare ningemfagilia kama angeomba serikali ijaribu kuiblock mitandao yote isiyokuwa na maadili mazuri kwa jamii kwa mfano www.worldsex.com na kadhalika lakini sio JF.

Mtandao ulioko kwa ajili ya kuwafungua macho, kuwapa habari, kuwaelimisha, kuwaburudisha, kuwajulisha wanajamii kuhusu haki zao, kubadilishana mawazo, kushauriana, kukosoana na mengine mengi kwa manufaa ya Taifa letu.

Isitoshe JF ni lazima ujisajili na umri unazingatiwa kufuatana na aina ya Forum. Sio kuingia kirahisi kama hizo worldsex.com n.k.
 
Hivi huyu mama anashindwa kuuliza maswali yenye tija kwa taifa,anauliza upupu ule?!hawaonei ht huruma kina mama wenzie wanaofia kwenye milango ya hospital kwa kukosa huduma anaöngelea jf?mch wa namna gan huyu?..
 
...itakua mchungaji dokta mheshimiwa mbuge mama lwakatare atakua anahasira ya ile issue ya zile clip zilizowahi kuwekwa humu za kummaliza kakobe.....so aliweka donge lake rohoni muda wooooooooooote huo na kulipiza kisasi leo.....atashindwa na atalegea kwa jina la JF....!!!! ameeeeeeeeeeeeen.............!!!
 
kuna tetesi huyu mama aliwahi kuingizwa mkenge na mkongomani.
Stori ilikua ivi,,,,,mkongo alitonywa kuwa huyu mama huwa anawashobekea sana wenye pesa, ikabidi a-act ni muumini mzuri anayetoa fungu la 10. Mkongo akawa anatoa sio chin ya m3 ivi kama fungu la kumi, kwa zaidi ya miezi kadhaa.

Maza akapagawa, ikabidi amwite msaidizi wake ili apeleleze ni nani huyo anayeweza kutoa mafweza hayo, ikibidi aje offisini waonane uso kwa uso.
Zoezi likafanikiwa, mkongoman huyo ofisin. Maza akamuulize huwa anamadili gani anayomwingizia kipato kile?
Mkongo akamwambia mi ni mfanyabiashara wa madini. Maza akazidi kupagawa.
Akamwomba washirikiane, mkongo bila hiyana huku akichekelea kimoyomoyo akamkubalia, maza akaambiwa akachote mpunga wa zaidi ya 500m ili amkabidi akamnunulia madini.
Maza kwa kiwewe akaenda kuchukua na kumkabidhi zigo.

Mkongoman mpaka leo hajulikani alipo.

that was investers trick!
 
Serikali haina ubavu iangalie yaliyotokea Tunisia, Misri, Yemen kunakotumoka mitandao ya kijamii na ianze kuifunga facebook, tweeter
Ze Utamu ilifungwa baada ya watumiaji wenyewe kulalamika na JF imeshajadiliwa Kikao kilichopita kuwa ni ya CDM Bunge likaeleweshwa na waanzilishi walitajwa na share zao.

Mm naona hamna haja ya kufika huko, wakidhubutu wote tutahamia mtandao mwingine na hao wabunge wachache watalala chali kwani viongozi wengi wapo humu hata kwenye fb JK yumo
 
Hata mimi nimeshangaa kumbe huyu mchungaji naye anaijua JF! siajabu ana fake ID na kuchangia labda anachangia humu

Me nina wasiwasi atakuwa anatumia ile ID inayokwenda kwa jina MAMA POROJO.
 
haya swali lenyewe lisaulizwa na majibu yake ni JAMBO AU JAMIIFORUM NI MTANDAO ULIOSAJILIWA NJE YA NCHI,

Hata kamaimesajiliwa nje inaweza kufungiwa isionekane hapa nchini ili kupunguza impact, lakini wakati huo huo inaweza kuwa inaonekana nje ya nchi
 
Mama Lwakatare ningemfagilia kama angeomba serikali ijaribu kuiblock mitandao yote isiyokuwa na maadili mazuri kwa jamii kwa mfano www.worldsex.com na kadhalika lakini sio JF. Mtandao ulioko kwa ajili ya kuwafungua macho, kuwapa habari, kuwaelimisha, kuwaburudisha, kuwajulisha wanajamii kuhusu haki zao, kubadilishana mawazo, kushauriana, kukosoana na mengine mengi kwa manufaa ya Taifa letu. Isitoshe JF ni lazima ujisajili na umri unazingatiwa kufuatana na aina ya Forum. Sio kuingia kirahisi kama hizo worldsex.com n.k.

Mkuu umeweka ya nini hiyo link ya ngono?
 
...anaogopa kuwa jamiiforums itakuja kutoa siri za mganga anayempa dawa za kudondoshea watu kwenye mimbari yake. Hamna ukristo pale,full-uchawi!!

thibitisha!!!!!!!!!! tuhuma nzito hii sikuwahi kufikiri japo hata mimi naamini mama anafanya mchezo wa kuigiza.
 
Mbunge wa viti maalum CCM Mchungaji Dr. Getrud Rwakatare leo ameushambulia mtandao wa jamii forum katika kipindi cha maswali na majibu kwa wizara ya sayansi na teknolojia kwa swali alilouliza kuwa: Mtandao wa jamii forum umekuwa ukisambaza taarifa za uwongo, nani mmiliki wa mtandao huu? Ndugai akaliwekea msisitizo: Mh. naibu waziri majibu kikamilifu maana hili ni jambo la msingi...
 
Back
Top Bottom