Huu ugonjwa uliwahi kumpata ndugu yangu mmoja, yeye nae kalikuwa ni kaupele mguuni, akakakuna kilichotokea baada ya kukakuna ni kama unavyosema mguu wa mama yako jinsi ulivyo, walimuwahisha hospital bahati mbaya sana nimesahau jina la huo ugonjwa, ila alifanyiwa oparation tatu, na madaktari walisema ni kwa sababu ugonjwa haujafika kwenye mfupa, ungefika kwenye mfupa kungekuwa hakuna jinsi zaidi ya kuukata mguu hadi kwenye goti, ila coz waliwahi walikwangua tu zile nyama na ata the end walikata nyama kwenye paja na kurudishia pale walipokwangua. Kiukweli hali ilikuwa mbaya hata sisi tulidhani ni kisukari but haikuwa kisukari, now anaendelea vizuri sana tu. so Mpelekeni hospital pengine ana huo ugonjwa, kama uko mwanza huyo ndg yangu alitibiwa hapo hospital ya CF, NSSF ya zamani