Mama ni mgonjwa

miss strong

JF-Expert Member
Jul 4, 2012
7,012
3,694
Habar wa MMU.......aiseee nahitaji mnikumbuke katika maombi,mama yangu ni mgonjwa na hatujui tufanye nini maana hospital ugonjwa hauonekani.

Alichomwa na kitu mguuni wiki 5 zilizopita ikaota kama kipele then lengelenge na baadae mguu wote ukawa umepata vidonda.

Kapimwa magonjwa mengi lakini hamna kitu......leo roho imeniuma sababu mguu umeanza kutoa harufu na tena ukijan umeanza.

Naumia sana....nahitaji maombi yenu anaitwa Vicky

Nashukuru kwa maombi na ushauri wenu.....hali ya mama bado haijatengamaa,amelazwa muhimbili kibasila!!
Endeleeni kutuombea jamani
 
Pole sana...tupo pamoja.

Karibu Richmond ministries kwa maombi.
 
Plz plz plz mara uonapo comment yangu Tafadhali nipm utamshangaa mungu alivyo wa ajabu atapata maombi maalum na utaushuhudia ukuu wa mungu plz namuhitaji huyo mama..Vicky Pamoja nawewe nikupeleke mahali ulipo muujiza wake.asante
 
Pliz niambie ni wapi....wakuu.Siwezi kulala jinsi navyoumia!!!Yaan leo karudi toka kwa dada yake yaan mama mkubwa ndo nimezidi kuumizwa nilivyouona mguu.
 
Pole sana miss strong kwa kuuguliwa mama. Mungu yupo na wewe, awape faraja na uponyaji wake uwe juu ya mama yetu kipenzi.
 
Last edited by a moderator:
Najaribu kujichanganya ila wapiiiii..... sijui nifanyeje wapendwa.
 
amechomwa nini kwemye mguu binti?kama amechomwa intravenous/intramuscular injections ambazo hazikuwa sterile zinasababisha infections sehemu alochomwa au vev damage n.k chunguza alichomwa nini au dawa ilikuwa expired alochomwa?
 
Mungu wetu ni mwema!naamini soon atakwenda kupona kwa maombi ya wapendwa pamoja na mm tunayoenda kuyafanya kwa ajili ya mama!pokea uponya mama!
 
amechomwa nini kwemye mguu binti?kama amechomwa intravenous/intramuscular injections ambazo hazikuwa sterile zinasababisha infections sehemu alochomwa au vev damage n.k chunguza alichomwa nini au dawa ilikuwa expired alochomwa?

Kilichomchoma hasa hata yeye ana hisi kati ya jiko o chelewa....
Alianza kutibiwa nearby hom hapa Massana hosptl na baadae lugalo ambapo alikuwa anachomwa sindano za powercef.
Sasa sielewi hapo ni nini haswa
 
acheki hospital kwa dokta Abbas yupo fire kama upo daslam huenda ni diabetes kwasababu kuna mtu wangu wa karibu naye alipata dalili kama hizo mguuni mguu ukapata lengelenge ukavimba kupima kumbe ni diabetes(kisukari) bac anatumia dawa na kucontrol diet lyf linaenda
 
Asante mkuu.....ila kidonda kinaweza kikapona???Mungu wangu
 
Back
Top Bottom