Nini cha kufanya kuepusha mgonjwa wa Kisukari asikatwe kiungo cha mwili?

George Betram

George Betram

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Messages
2,666
Points
2,000
Age
25
George Betram

George Betram

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2015
2,666 2,000
Ni takribani mwezi mmoja na nusu tangu Aunt yangu azidiwe na ugonjwa wa Kisukari.
Hali ilianza kuwa mbaya alivyopata kidonda mguuni (maeneo ya kifundo cha mguu), kidonda hicho kilianza kama lengelenge tu.
Wiki iliyopita tulimpereka hospital baada ya hali kuwa mbaya,amelazwa hapo hospital wiki nzima.
Leo daktari amepima mguu amesema inatakiwa mguu ukatwe,kwani umepoteza mawasiliano.
Inanitisha na kunipa wasiwasi sana wakuu,hivi kweli hakuna njia nyingine ya kumsaidia Aunt yangu zaidi ya kukatwa mguu???

Nahitaji mawazo yenu juu ya hili jambo wakuu,mara ya mwisho kupimwa kiwango cha sukari mwilini ni leo asubuhi amekutwa na sukari 12.
 
Am the One

Am the One

Senior Member
Joined
Nov 1, 2018
Messages
183
Points
225
Am the One

Am the One

Senior Member
Joined Nov 1, 2018
183 225
Pole sana mkuu..

Remember, your mind is greatest asset.
 
Kingsmann

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Messages
859
Points
1,000
Kingsmann

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2018
859 1,000
Mara nyingi watu wenye kisukari hupata complications ya kupata madhara kwenye neva/mishipa ya damu ya miguuni.

Complication hii hupelekea asiweze kuhisi (anapata ganzi) chochote huko miguuni. Kwa hiyo hata akijikata, akipata mchubuko hatahisi maumivu yoyote.

Na mara nyingi akipata hata kamchubuko hakatapona bali kataendelea kukua na kuwa kidonda kamili sababu hamna blood supply ya kutosha maeneo hayo.

Hivi vidonda huwa ni hatari sana sabab vinaweza kusababisha ascending infections na kupelekea muhusika kupata maradhi mengine.

Kwa hiyo matibabu mazuri zaidi huwa ni kukata mguu husika kwa sababu hivi vidonda huwa haviponi. Huendelea kukua na vinaweza kutafuna mguu wote.

Ni vizuri mkawahi kuukata kwa sababu jinsi mnavyozidi kuchelewa mishipa ya damu inaendelea kuathirika kwenda juu zaidi na itapelekea mguu kukatwa juu zaidi.

The early amputation is the best one.
 
Dah,kwahiyo hakuna njia nyingine tofauti na kukata mguu Kiongozi?
 
Asclepius

Asclepius

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Messages
623
Points
1,000
Asclepius

Asclepius

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2017
623 1,000
Mara nyingi watu wenye kisukari hupata complications ya kupata madhara kwenye neva/mishipa ya damu ya miguuni.

Complication hii hupelekea asiweze kuhisi (anapata ganzi) chochote huko miguuni. Kwa hiyo hata akijikata, akipata mchubuko hatahisi maumivu yoyote.

Na mara nyingi akipata hata kamchubuko hakatapona bali kataendelea kukua na kuwa kidonda kamili sababu hamna blood supply ya kutosha maeneo hayo.

Hivi vidonda huwa ni hatari sana sabab vinaweza kusababisha ascending infections na kupelekea muhusika kupata maradhi mengine.

Kwa hiyo matibabu mazuri zaidi huwa ni kukata mguu husika kwa sababu hivi vidonda huwa haviponi. Huendelea kukua na vinaweza kutafuna mguu wote.

Ni vizuri mkawahi kuukata kwa sababu jinsi mnavyozidi kuchelewa mishipa ya damu inaendelea kuathirika kwenda juu zaidi na itapelekea mguu kukatwa juu zaidi.

The early amputation is the best one.
Naunga mkono hoja
Kuwahi mapema kunasaidia

Ingawa kuna watu wa asili wanadai kuna doctor mwenzangu anadai alitumia kwa ndugu yake alikua na vidonda akapona
Me mwenyewe siamini saaana hizo vitu ila kama unataka jaribu naweza kuku hook up

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suriya

Suriya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Messages
2,600
Points
2,000
Suriya

Suriya

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2015
2,600 2,000
Mkuu tiba pekee apo ni kucontrol hiyo sukari yake ya kupanda ambayo bado ipo juu.

Ushauri wangu, watafute watu wa tiba asili wanatoa dawa nzuri tu kwa qjili ya kutibu kisukar,

Dawa zao zinaanzia sh. 2000 dawa moja, ya aina moja na dawa zao gharama inafika hadi laki 3. Ni tiba nzur ambayo imeonesha matokeo mazuri kwa wengi walio tumia.

Asipo control hiyo sukar anaweza kupata kidonda kingine mguu wa pili na madhala kua yale yale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
George Betram

George Betram

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Messages
2,666
Points
2,000
Age
25
George Betram

George Betram

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2015
2,666 2,000
Mkuu tiba pekee apo ni kucontrol hiyo sukari yake ya kupanda ambayo bado ipo juu.
Ushauri wangu, watafute watu wa tiba asili wanatoa dawa nzuri tu kwa qjili ya kutibu kisukar,
Dawa zao zinaanzia sh. 2000 dawa moja, ya aina moja na dawa zao gharama inafika hadi laki 3. Ni tiba nzur ambayo imeonesha matokeo mazuri kwa wengi walio tumia.
Asipo control hiyo sukar anaweza kupata kidonda kingine mguu wa pili na madhala kua yale yale
Sent using Jamii Forums mobile app
Naweza kupata mawasiliano ya hao wataalamu..?
 
S Sulayman

S Sulayman

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2018
Messages
258
Points
250
S Sulayman

S Sulayman

JF-Expert Member
Joined Apr 21, 2018
258 250
*UFAHAMU UGONJWA WA KISUKARI NA TIBA YAKE* .
www.sangidaherbal.blogspot.com

Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) hutokea pale tezi kongosho (pancrease) inaposhindwa kutengeneza homoni au kichocheo aina ya Insulin, au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho cha insulin na kusababisha kuongezeka kiwango cha sukari kwenye damu (hyperglycemia).
Insulin ni kichocheo au homoni inayotengenezwa na kongosho ili kudhibiti kiwango cha sukari.
Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa kuwa na kiwango kidogo cha Insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili. Ili kuelewa vyema ugonjwa wa kisukari ni muhimu kwanza kuelewa namna chakula kinavyovunjwa vunjwa na kutumiwa na mwili ili kuzalisha nguvu.
Wakati chakula kinapoyeyushwa matukio kadhaa hutokea.

1.Tukio la kwanza ni sukari inayoitwa glucose ambayo ni chanzo cha nguvu mwilini huingia katika damu.
2.Tukio la pili ni kiungo kinachoitwa kongosho (pancrease) kutengeneza kichocheo cha Insulin. Kazi ya Insulin ni kuondoa glucosei katika damu na kuingiza katika misuli, seli za mafuta na ini, ambako hutumiwa kama nishati.
Watu wenye ugonjwa wa kisukari huwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kwa sababu miili yao haiwezi kupeleka sukari kwenye seli za mafuta, ini na misuli ili ihifadhiwe kwa ajili ya kuzalisha nguvu.
Hii ni kutokana sababu zifuatazo.

1.Kongosho kutokuwa na uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha, au--->
2.Seli za mwili haziathiriwi na insulin kama inavyotakiwa ama sababu zote hizo mbili.

AINA ZA KISUKARI
KISUKARI AINA YA KWANZA(TYPE 1 DIABETES MELLITUS)

Hii ni aina ya kisukari inayowaathiri zaidi watoto na vijana. Aina hii hutokea iwapo seli maalumu zinazotengeneza homoni ya insulin zinapokosekana katika tezi kongosho au zinapoharibika kutokana na sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.
Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa seli hizi katika tezi kongosho ni pamoja na kushambuliwa tezi kongosho kunakoweza kufanywa na magonjwa ya kinga ya mwili ya mtu mwenyewe au autoimmune diseases, au kushambuliwa na vyanzo visivyojulikana.

KISUKARI AINA YA PILI (TYPE 2 DIABETES MELLITUS)
Hii ni aina ya kisukari inayotokea zaidi ukubwani. Aina hii ya kisukari husababishwa na kupungua utendaji kazi wa homoni ya insulin, au seli kushindwa kutumia insulin ipasavyo.
Hali hii mara nyingi husababishwa na unene uliopitiliza yaani obesity, au hali ya kutoushughulisha mwili kabisa (physical inactivity).
Kwa vile, katika aina hii ya kisukari, insulin huzalishwa kwa kiwango cha kutosha isipokuwa tatizo lipo kwenye ufanisi na utendaji kazi wake,

KISUKARI CHA UJAUZITO (GESTATIONAL DIABETES MELLITUS)
Ni aina ya kisukari kinachotokea pindi kunapokuwa na ongezeko la kiwango cha sukari katika damu (hyperglycemia) wakati wa ujauzito. Aina hii ya kisukari huathiri karibu asilimia 2 hadi 5 ya mama wajawazito wote ingawa wengi wao hupata nafuu na kupona kabisa mara tu baada ya kujifungua.
Hata hivyo karibu asilimia 20 mpaka 50 ya mama wajawazito wanaopata aina hii ya kisukari huweza kuendelea kuwa na ugonjwa huo hata baada ya ujauzito na hatimaye kuwa na aina ya pili ya kisukari.

SABABU ZA KISUKARI

Sababu za kisukari hutofautiana kulingana na aina ya ugonjwa huo.
Aina ya kwanza ya kisukari ina uhusiano mkubwa sana na kurithi. Aidha aina hii pia husababishwa na maambukizi virusi kama vile Coxsackie virus type B4.
Visababishi vingine ni pamoja na sumu inayotokana na kemikali za baadhi ya vyakula (food borne chemical toxins), na kwa baadhi ya watoto wachanga maziwa ya ng'ombe yanaweza kuchochea kinga ya mwili wa mtoto uushambulie mwili wenyewe na hivyo kusababisha uharibifu katika tezi kongosho.

Aina ya pili ya kisukari kwa ujumla husababishwa zaidi na jinsi mtu anavyoishi na pia matatizo ya kijeneteki. Aidha kuongezeka uzito na unene kupita kiasi (obesity).

Sababu nyingine ni pamoja na kuongezeka umri, maisha ya kivivu na kutofanya mazoezi na pia ugonjwa wa tezi kongosho (pancreatitis) ambao hufanya insulin inayozalishwa kuwa na ufanisi mbovu au ya kiwango cha chini.

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI
Kukojoa mara kwa mara
Kuhisi kiu kali na kunywa maji kwa kiwango cha kupitiliza (polydipsia).
Kuhisi njaa na kula mara kwa mara (polyphagia).
Kuchoka haraka
Kupungua uzito
Vipele mwilini (diabetic dermadromes).
Kutoa harufu ya acetone inayofanana na harufu ya pombe.
kuhisi maumivu ya tumbo na kupoteza fahamu

Na wagonjwa wa kisukari pia huwa katika hatari ya kupata maambukizi katika kibofu cha mkojo, ngozi na kwa wanawake sehemu za siri.
Baada ya mtu kuwa na dalili za ugonjwa wa kisukari matibabu huanza baada ya kufanyiwa vipimo na kuthibitisha kwamba kweli ana ugonjwa huo.

Chini ya 5.6 mmol/l au 100 mg/dl: Sukari kwenye damu yako ni sawa.
Zaidi ya 5.6 mmol/l au 100 mg/dl lakini chini ya 6.9 mmol/l au 125 mg/dl: Hii ni ishara ya tahadhari-unapaswa kufanya mabadiliko katika maisha yako sasa ili kupunguza hatari ya kupata kisukari. Kama matokeo yamekaribia kiwango cha juu, ni muhimu hasa kufanya juhudi za ziada za ulaji wenye afya, na kupata mazoezi au kujishughulisha.

Zaidi ya 6.9 mmol/l au 125 mg/dl: Una kisukari na unahitaji matibabu. Kadri kiwango kinavyopanda, ndivyo kuongezeka kwa hatari ya dharura kutokana na kiwango cha sukari kwenye damu kuzidi kupita kiasi, au matatizo makubwa ya kiafya

MATIBABU YA KISUKARI KWA DAWA ASILI

www.sangidaherbal.blogspot.com
Ni dawa mujarabu sanaa na zinaponesha kabisa kisukari in shaa Allah.

1. ALMUNIYRU
Hii ni dawa iliyotengenezwa kwa kutumia miti shamba na ni nzuri kwa aina zote za kisukari

Ili kuzipata dawa hizi , pia ukihitaji ushauri na tiba ya maradhi mbalimbali wasiliana nasi

+255 655 821 550

Sulayman Sangida----- Dar es Salaam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchira 1

Uchira 1

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2017
Messages
1,342
Points
2,000
Uchira 1

Uchira 1

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2017
1,342 2,000
mkuu doct ABASI anasaidia wengi sana na wale waliotakiwa kukatwa miguu au viungo vyao vimesalimika yupo hapo kariakoo, ila mkuu jitahidi sana tena epukeni vyakula vyenye sukari na wanga, sukari iliwa normal kidonda kinapona
 
stephot

stephot

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2012
Messages
7,545
Points
2,000
stephot

stephot

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2012
7,545 2,000
Amtafute doctor Abbas hapo mitaa ya Kariakoo,sina uhakika kama bado yupo pale ila aulizie fasta...
 
M

marisi schwein

Member
Joined
Dec 3, 2013
Messages
49
Points
125
M

marisi schwein

Member
Joined Dec 3, 2013
49 125
Km miguu umeshaoza kumpeleka mgonjwa kwenye tiba asilia kutapelekea infection kupanda na kusambaa mwilini na kupelekea sepsis au mgonjwa kupata septic shock na kufariki. Ushauri wangu kama mgonjwa yupo Dsm karibu kumpeleka hospitali kubwa yenye specialist wa sukari ( endocrinologist) km atakwambia kwamba miguu unatakiwa kukatwa basi huna budi kufuata ushauri wa daktari
 
NZURI PESA

NZURI PESA

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2011
Messages
5,891
Points
2,000
NZURI PESA

NZURI PESA

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2011
5,891 2,000
M
Ni takribani mwezi mmoja na nusu tangu Aunt yangu azidiwe na ugonjwa wa Kisukari.
Hali ilianza kuwa mbaya alivyopata kidonda mguuni (maeneo ya kifundo cha mguu), kidonda hicho kilianza kama lengelenge tu.
Wiki iliyopita tulimpereka hospital baada ya hali kuwa mbaya,amelazwa hapo hospital wiki nzima.
Leo daktari amepima mguu amesema inatakiwa mguu ukatwe,kwani umepoteza mawasiliano.
Inanitisha na kunipa wasiwasi sana wakuu,hivi kweli hakuna njia nyingine ya kumsaidia Aunt yangu zaidi ya kukatwa mguu???

Nahitaji mawazo yenu juu ya hili jambo wakuu,mara ya mwisho kupimwa kiwango cha sukari mwilini ni leo asubuhi amekutwa na sukari 12.
Mkuu sukari 12 akatwe mguu?Ni hospitali ya serikali au binafsi mlimompeleka?
Kidondankina muda gani tika kitokee
 
George Betram

George Betram

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Messages
2,666
Points
2,000
Age
25
George Betram

George Betram

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2015
2,666 2,000
M
Mkuu sukari 12 akatwe mguu?Ni hospitali ya serikali au binafsi mlimompeleka?
Kidondankina muda gani tika kitokee
Dah,Aunt yangu amekatwa mguu jana Kiongozi...
Kidonda chake kilikua kina kama miezi mitatu hivi...
Hospital ni ya serikali,Temeke hospital..!
Sukari yake kuna wakati ilikua inapanda mpaka kufikia 20+
 
feyzal

feyzal

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Messages
963
Points
1,000
feyzal

feyzal

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2016
963 1,000
Mkuu tiba pekee apo ni kucontrol hiyo sukari yake ya kupanda ambayo bado ipo juu.

Ushauri wangu, watafute watu wa tiba asili wanatoa dawa nzuri tu kwa qjili ya kutibu kisukar,

Dawa zao zinaanzia sh. 2000 dawa moja, ya aina moja na dawa zao gharama inafika hadi laki 3. Ni tiba nzur ambayo imeonesha matokeo mazuri kwa wengi walio tumia.

Asipo control hiyo sukar anaweza kupata kidonda kingine mguu wa pili na madhala kua yale yale

Sent using Jamii Forums mobile app
Nina ndugu yangu alikua na sukari ametumia dawa za asili mpaka leo akipima anakuta 5-7 so kama unavyosema tusidharau hao watu wanasaidia pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NYANYADO

NYANYADO

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Messages
3,058
Points
2,000
NYANYADO

NYANYADO

JF-Expert Member
Joined Jan 8, 2013
3,058 2,000
MUNGU pekee aweza yote Yaloshindikana.
 
Forum statistics

Threads 1,294,031
Members 497,789
Posts 31,162,767
Top