Salaam kwako Faiza Foxy. WaTZ wengi hatujui siasa zinazoendelea kwenye nchi zenye migogoro na jambo usilolijua litakusumbua. Mengi yanayoonekana kwenye media ni propaganda kama hizi zinazoendelea sasa kuelekea uchaguzi mkuu.
Ni vema tujadili yanayotuzunguka na tuliyo na ujuzi nayo kuliko kuleta ushabiki wa kidini tena unaoanzia mataifa ya mbali. Mfano leo USA wamesema hospitali ya Kunduz ilipigwa kwa maombi ya serikali ya Afghanistan, nani anajua ukweli wa ndani kwenye hili na kwanini serikali hiyo iombe msaada wa hivyo? Kama suala ni Taleban mbali na kuichukua Kunduz mbona haohao wanashirikiana na serikali hiyohiyo sehemu nyingine!! Yanayotokea Syria yalianzishwa na wa-Syria wenyewe baada ya kuchoshwa na utawala wa miaka nenda rudi wa familia moja. Mataifa yamejaribu kuingilia kati kutaka kusaidia ikiwa ni pamoja na kupambana na vikundi vinavyoamika kuwa hatari kwa ustawi wa mataifa mengine lakini hali inakuwa tete siku hadi siku. Udini umeingizwa hapa lakini mimi sikubaliani na hilo. Narudia kusema tena, usilolijua litakusumbua.
Hakuna vita mbaya duniani kama vita za kidini na tukubali tusikubali kwa Tanzania ni bora turudi tu kwenye ujima wetu wa miaka ya 90 ambao bado umetufnya wamoja hadi hii leo. Mbele ya Mwenyezi Mungu mbora ni yule anayemwabudu, kumuomba na kumshukuru kwa kila jambo. Sasa kama wewe ni Muislam, Mkristo, Mbudha, Mpagani, nk. simama kwenye imani yako na kuendelea kuomba pepo. Wanayohubiri masheikh, wachungaji na viongozi wengine kama yapo kwenye maandiko yanayoaminika matakatifu kwa kila wafuasi na waumini wao na waendelee kuamini hivyo bila kukwaza wengine. Muhimu kujua kuwa ulikuja duniani peke yako ukiwa dhaifu, na utaiacha dunia ukiwa peke yako na dhaifu, sasa vipi umsumbue mwingine!! Sijaona katika vitabu vyote kwamba ukiwa na mihemko katika kuhubiri dini utapata pepo, ni udhaifu tu wa kibinadamu huo.
Mwenye masikio na asikie