Mama, mpaka mwendokasi unawapa waarabu?🤦🏾‍♂️😳

Mama, mpaka mwendokasi unawapa waarabu?🤦🏾‍♂️😳

Kwa hili nipo na Mama Samia kwa mara ya kwanza namuunga mkono!
Sisi watanzania kila kitu hatuwezi,kwanzia mradi wa mwendo kasi hatuna kitu ni hasara tu.
TRC ,TTCL,kila siku ni kuendesha miradi kwa madeni.
Sasa ni bora tuwape hao waarabu ili tupate uzoefu baada ya kutoka VETA.
Huo mradi wangewapa watanzania waliobobea kwenye sekta ya usafirishaji wasingeshindwa, kwani miundo mbinu yote Serikali imeshaweka. Wanachukua 30% ya profit na Serikali inachukua 70%. Hapo ni baada ya kutoa gharama zote za uendeshaji. Hii ndiyo njia ya kutengeneza mabilioni wazawa kama wanavyofanya China. Tena China ni wazawa wanawezeshwa na kufanya peke yao sababu tayari wana rasilimali watu na rasilimali fedha. Hata waarabu uongozi wa juu wa mashirika yao mengi uko chini ya wazungu kama waajiriwa na si kama wabia
 
Kampuni gani ya mabasi ya wazalendo imedumu hata miongo miwili kuanzia UDA,KAMATA ,SCANDANAVIA, BUFFALO hadi KILIMANJARO?
Abood ni ya kitambo sana mkuu ina zaidi ya miongo mitatu, hata Shabiby ameshakuwa na uzoefu. Hawa ni watanzania wenye asili ya nchi zingine. Hata wakifanya kwa ubia nakuhakikishia watatengeneza ajira nyingi za wazawa. Tatizo la miradi kuwa serikalini ni ukiritimba, wizi na kutowajibishana.
 
Huo mradi wangewapa watanzania waliobobea kwenye sekta ya usafirishaji wasingeshindwa, kwani miundo mbinu yote Serikali imeshaweka. Wanachukua 30% ya profit na Serikali inachukua 70%. Hapo ni baada ya kutoa gharama zote za uendeshaji. Hii ndiyo njia ya kutengeneza mabilioni wazawa kama wanavyofanya China. Tena China ni wazawa wanawezeshwa na kufanya peke yao sababu tayari wana rasilimali watu na rasilimali fedha. Hata waarabu uongozi wa juu wa mashirika yao mengi uko chini ya wazungu kama waajiriwa na si kama wabia
Hakuna unalolijua.
 
Miaka 60 ya uhuru hatuna uwezo wa kuendesha biashara ya daladala🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣. Ninacheka ila sisi ni wangese sana.
 
Pamoja na makampuni yote ya magari mwendokasi eti wanapewa waarabu. Faida inaenda kwa mwekezaji nje wakati kampuni kibao za mabasi bongo🤦🏾‍♂️🤦🏾‍♂️. Mama tumekukosea nini? Unaua demokrasia, unateka vijana wetu, unaiba kura, bandari ya dar bila tendef waarabu wa Dubai, carbon credit dogo Abdul na waarabu, uwanja wa kia kumbe fukuza fukuza yote ni kwasababu ya kuwapa wa Oman, bandari ya bagamoyo kisirisiri wanatapesa Saudi….. sasa ukiondoka tutakuwa na makesi ya kuvunja mikataba kila siku. Reli wamapewa china bila tender

Yaani Mama huyu hata huruma hana tumetumia $1B kuagiza chuma Tsh 500B kuagiza ngano🤦🏾‍♂️ vijana hawana kazi kwasababu ya haya .. wamekuwa machawa. Yaani 10% Mama kwenye kila kitu. Angalia tamaa zako zitakuponza Mungu hajakiweka hapo ufanye haya
Kuwapa kuwapa kuwapa ndio nini ?!!

Nikupeleke DARASANI.....

MWEKEZAJI HUWA hapewi....

Dunia inabadilika kwa kasi.....ukipinga UWEKEZAJI unapinga maendeleo ya taifa kwani uwekezaji wa miradi mikubwa hauhitaji mwekezaji "wa kihindi" ambaye atashinda TENDA na kwenda KUKOPA CRDB.... mwishowe aingie mitini....

Tunahitaji WAWEKEZAJI wenye. NGUVU ZA MITAJI.....

KALAGHABAHO
 
Kabla ya kuandika waraka huu taja mradi mmoja tu umewahi kuendeshwa kwa faida na sisi wazawa? tumefilisi kila kitu na tunajenga vi stand vya bus Billion 5 havina thamani hata ya Million 100 moja. Tutajie shirika moja tumeweza kulikuza zaidi ya kuuwa. Mwendokasi tulikuwa sisi tumefanya nini? Ma bus hakuna na yaliyopo hayatoshi likiharibika ndio basi tena. SGR pale watu wanapiga pesa kwenye tickets hatari hawana hata uchungu wanajali matumbo yao tu. Yaani ni wizi mtupu wewe ukitaka kufilisika mradi wako mpe Mtanzania tu. Nimeona miradi ya barabara imefanywa na kampuni za wazawa ni aibu mashimo tupu mpaka miradi inarudiwa. Badala ya kulaumu tujiangalie sisi tumefanya nini?
Kwenye mashirika yote ya umma ceo wanapewa kwa kujuana na sio kwa kuangalia uwezo

Umempa mtu nafasi kwa kujuana hata akifanya vibaya huwezi mfanya chochote kwa hiyo sio kweli watanzania hawana uwezo hapana wenye uwezo hawana connection
 
Halafu ana account nyingi sana fb huko, ukichat nae jambo anakujibu kisikivu kweli, kesho ukimrudia unaanza upya kumueleza shida yako
 
Kabla ya kuandika waraka huu taja mradi mmoja tu umewahi kuendeshwa kwa faida na sisi wazawa? tumefilisi kila kitu na tunajenga vi stand vya bus Billion 5 havina thamani hata ya Million 100 moja. Tutajie shirika moja tumeweza kulikuza zaidi ya kuuwa. Mwendokasi tulikuwa sisi tumefanya nini? Ma bus hakuna na yaliyopo hayatoshi likiharibika ndio basi tena. SGR pale watu wanapiga pesa kwenye tickets hatari hawana hata uchungu wanajali matumbo yao tu. Yaani ni wizi mtupu wewe ukitaka kufilisika mradi wako mpe Mtanzania tu. Nimeona miradi ya barabara imefanywa na kampuni za wazawa ni aibu mashimo tupu mpaka miradi inarudiwa. Badala ya kulaumu tujiangalie sisi tumefanya nini?
Hakuna uwekezaji mkubwa ufanywao "kihindi".....

Kudos kwa ufafanuzi maridhawa!
 
Umeongea BOKO...

Umeongea KIWEPESI mno....

Huna UELEWA katika mawanda ya uwekezaji wa miradi mikubwa.....

Serikali ya Kenya imeipa KARANDASI kampuni ya AMSONS baada ya kununua kampuni ya BAMBURI CEMENT huko Mombasa.....

AMSONS wameinunua kampuni hiyo ya Mombasa kwa shilingi 427 bilioni ,uwekezaji wao huo unajumuisha jumla ya shilingi bilioni 840....

Uwekezaji si jambo dogo kwani hao AMSONS wataanza uzalishaji wa CEMENT miezi 24 baada ya kuwekeza......

Wewe fulafula hebu ongeza maarifa kabla ya kutuletea "pang'ang'a" humu JF.....

#Rais Samia anaendelea kuuinua uchumi wa Taifa takatifu Tanzania !
 
Kampuni gani ya mabasi ya wazalendo imedumu hata miongo miwili kuanzia UDA,KAMATA ,SCANDANAVIA, BUFFALO hadi KILIMANJARO?
... kama wanafisidi na kuua kampuni ndogo hizo ndio leo wafaulu kupewa UWEKEZAJI MKUBWA ?!!

Hapana kwa kweli....

Serikali yetu iko sahihi sana....
 
mnachosahahu labda ni kwamba kabla ya mapinduzi wote waliweka kambi dubai hata akina mbowe & co. walikuwa huko, sasa mapinduzi yoyote yale dunia hii yanakwenda na reparations, na hii ni dunia nzima, haujasikia D.Trump anataka madini ya ukraine sababu USA imelipia kuilinda Ukraine ?
Ukraine inayolindwa ni ile iliyosambaratishwa vile,labda sijui maana ya uLinzi.
 
Pamoja na makampuni yote ya magari mwendokasi eti wanapewa waarabu. Faida inaenda kwa mwekezaji nje wakati kampuni kibao za mabasi bongo🤦🏾‍♂️🤦🏾‍♂️. Mama tumekukosea nini? Unaua demokrasia, unateka vijana wetu, unaiba kura, bandari ya dar bila tendef waarabu wa Dubai, carbon credit dogo Abdul na waarabu, uwanja wa kia kumbe fukuza fukuza yote ni kwasababu ya kuwapa wa Oman, bandari ya bagamoyo kisirisiri wanatapesa Saudi….. sasa ukiondoka tutakuwa na makesi ya kuvunja mikataba kila siku. Reli wamapewa china bila tender

Yaani Mama huyu hata huruma hana tumetumia $1B kuagiza chuma Tsh 500B kuagiza ngano🤦🏾‍♂️ vijana hawana kazi kwasababu ya haya .. wamekuwa machawa. Yaani 10% Mama kwenye kila kitu. Angalia tamaa zako zitakuponza Mungu hajakiweka hapo ufanye haya
Urefu wa kamba
 
Urefu wa kamba
Urefu wa kamba nao unatafsirika kuwa kwa miradi mikubwa huwezi kukabidhi kandarasi kwa "magabacholi" ambao watakwenda kukopa fedha ya uwekezaji CRDB....
Urefu wa kamba ni hiyo MISULI YA NGUVU ZA UWEKEZAJI ZA WAWEKEZAJI wenye kutujia na MITAJI YAO.....
 
Back
Top Bottom