Huyu naye hajapata nafasi tu ya kufisadi, ufisadi na CCM wameoana!
Halafu masatu unashangaa kwa nini hupati kazi foreign!
B]a tena KAZI KWENU kikosi cha CSI cha JF[/B]
Malecela ana watoto wangapi? maana kwa jinsi walivyotajwa hapo naona kuna wengine hawako
ama kweli foreign hapafai
Mbona jujamtaja mtoto wa kigogo mwingine aliyepewa kazi tuuu kwa sabubu yuko hapo UN muda mrefu?
Anapogoma kuliongelea swala hili anakubali kwamba ameiba na kakosea, anakubali kumwajiri mkwe wake kimyemela. Inabidi ajiuzulu haraka sana ili asitutie aibu zaidi kwa sababu kuna mengi ambayo bado hayajasemwa. Hii ni tabia mbaya ambayo inaendekezwa hata na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa sababu mawaziri kama Karamagi ambao wanatuhumiwa na kashfa nzito za kusaini Buzwagi bado wanapeta, waziri mkuu ambaye Richimonduli gate imemkumbatia naye anapeta tu kwa hiyo tabia mbaya kama hii na yeye anayo ndio maana anaficha ficha uvundo na uozo ambao mnuko wake unasikika duniani kote hadi makao makuu ya IMF World Bank n.k.Mwenyewe Agoma Kuzungumza!
Field Marshall Es, maneno mazuri mkuu wangu mazito na kweli tupu. hadi hapo tutakapoweza kuweka sheria kuzuia ajira za Undugunization kama ya UN ama Taasisi nyinginezo, hakuna aliyevunja sheria na itaendelea kuwa tabia ya mwafrika.
Wenzetu nchi za nje hufanya haya (ajiri ndugu) ktk biashara binafsi kwani hapo pekee ndipo undugu hufanya kazi vizuri.
Kitila,
Mpe heshima zake Shein, makamu wa rais ni nafasi kubwa ya kutosha, kama anataka kuwa fisadi tungeona tayari anajichukulia mashamba, nyumba na hata kampuni.
Hata mimi naona huyu ni katika Watanzania wasafi.
While I give Dk. Shein the benefit of doubt as stated in my earlier post whick asked Kitila not to speculate and taint somebody without evidence, I still think Dk. Shein is not the right leader, mainly for two reasons.
1.Ukikaa na wezi, hata kama hujaiba lakini umekubali kuacha wizi ukiendelea bila kusema basi na wewe ni mwizi by association.Hata kama Dk Shein ni safi personally usafi wake unachafuliwa na fact ya kwamba amekuwa complacent mbele ya wizi. Tukumbuke huu "uzuri" "upole" na "usafi" ndiyo ulitupa Kikwete ambaye matokeo yake tunayaona. Hapa in one sense Kitila anaweza kuwa validated kwamba kama Shein anaweza kukaa kimya mbele ya wezi hawa, inawezekana anapalilia image ya usafi ili ije kuwa strong point yake ya kupata urais halafu akipata ndiyo ataonyesha makucha kama Kikwete, but I do not want to speculate too much in advance (ndiyo maana nikasema kuhusu post ya Kitila kuwa kama anasema Shein is guilty by association he should say so)
2.Hatuchagui mtu, tunachagua chama.Watu kama Shein ambao wame-demonstrate complacency hawana nafasi katika uongozi wa Tanzania kwa sababu siamini kama watakuwa na uwezo au guts za kubadilisha mwenendo wa uozo uliotapakaa katika ngazi zote za juu za CCM. Kwa hiyo hata kama yeye safi ndiyo ataleta mambo ya Mwinyi ya kwamba "mimi walii, we fanya utakavyo".Tumeona hii kwa kiasi kikubwa kwa Kikwete, mtu anayecheka cheka mpaka anashindwa hata kumuondoa Katibu Mkuu wake mwentyewe au hata kulibadili baraza la mawaziri linalopigiwa kelele kila kukicha.
Shein hafai, kwanza mpaka leo sijui amefanya nini Tanzania zaidi ya kuwakilisha nchi kwenye talkshops na ziara zisizo idadi ambazo mtu yeyote makini anaweza kufanya.In other words Shein hajaji=distinguish vya kutosha kweza kuwa promising kama rais anayeweza ku turn around Tanzania.
Brazameni,
Wasoijua CCM hata siku moja hawatakubali ukweli. Watu clean siku zote hawana maisha nadhani hiyo iwe ndio ishara yetu kubwa ya kiongozi mzuri.
Kifupi CCM wamejaa viongozi wa kudumu na maisha yao ni marefu sanaaa! Huyu Shein is clean - so far ktk CV ya kishwahili!
Field Marshall Es,
Mimi nadhani viongozi wasipewe ruksa ya kuajiri wao ndugu zao hasa sehemu wanazoongoza wao. Nje ya hapo uwanja wazi kwa kila mtu.
KM.....
hapo kaka sikubaliani na wewe,the guy almost 5yrs ameshakaa pale lakini still yupo fresh tu.
mie naamini wampe nafasi 2015 awe rais wa MUUNGANO au waonaje?[/B]
Brazameni,
Duh, umenikumbusha Dr. Omar damn. hapo ndipo utakapo koma na mazingira ya kiafrika. Ule msemo Wema hawana maisha! hii hutokea only in AFRICA. Wenzetu kwao hao wema huishi miaka mingi zaidi (kina mama Theresa) na wakifa huacha kazi zao zikiendeleza wema wao sio sisi.
Kisha yaonyesha kuwa viongozi wengi toka Zanzibar ni clean zaidi kuliko bara tukiwa ondoa Karume na Seif Shariff Hamad.