William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,389
Mwenyewe Agoma Kuzungumza!
Rais wa Bunge la Afrika, Mama Getrude Mongella, anatuhumiwa kutenda makosa ya kukosa uaminifu, Wizi na utoaji ajira kinyume na taratibu za kazi yake:-
1. WIZI:- anatuhumiwa kutafuna Dola za US, 138,000 ambazo ni sawa na shillingi 180Millioni za Tanzania.
2. UAJIRI:- anatuhumiwa kuajiri ndugu zake kinyume na sheria za kazi yake, akiwemo mkwe wake, yaani mke wa mtoto wake.
Katika kikao cha AU kilichopita nchini Ghana, nchi za Afrika zilimuamuru mama huyo kurudisha hela hizo mara moja huku uchunguzi ukiwa unaendelea, kikao hicho pia kilihudhuriwa na Rais Kikwete.
Mama Mongella, anatuhumiwa kujilipa US/Dola 800, kwa siku akilifanyia kazi bunge hilo la Afrika, na huku akiwalipa US/Dola 400 kwa siku ndugu zake aliowaajiri huko AU, wakati pia akilipwa na bunge la Tanzania kwa kazi hiyo hiyo. Mkwe wake mama huyu tayari ameshaachishwa kazi na bunge hilo na wengine wako njiani kurudishwa tayari Tanzania.
Katibu wa Bunge la Tanzania, ndugu Foka, alithibitisha kupata habari hizo za tuhuma dhidi ya Mama Mongella, na amekiri kwamba ni kweli Bunge letu la Tanzania limekuwa likimlipa mama huyo fedha zote anazostahili akiwa analifanyia kazi bunge la Afrika, kwa mujibu wa makubaliano na bunge hilo la Afrika, ambalo liliwaomba mwanzoni wakati anaanza kuwa liwe linamlipa ili asilipwe na bunge hilo la AU.
Taarifa za uchunguzi tayari zimefanyika na SADC, ikishirikiana na kampuni ya KP GM ya Kenya, ambazo izmeshauri mama huyo kufukuzwa kazi na kurudisha mapesa hayo kwa AU, mara moja. Mbunge mmoja wa bunge hilo la AU, Ndugu Wanyancha,(Serengeti-CCM) amekubali kuwa kweli Mama anakabiliwa nashutuma nzito sana ambazo zitatukosesha urais huo kwa muda mrefu sana ujao, juhudi zote za kuzungumza naye kuhusu hiii sualazimakwama kutokana na kukataa kwake, mama huyo.
Source: Mwana-Halisi.