Mama mkwe wangu ana adabu kupitiliza

Mama mkwe wangu ana adabu kupitiliza

Kweli mama wakwe akiwemo mama yangu hawafanyi yafustayo

1. Kukaa ma mkwe sebleni yaan mkwe akiingia lazima mama mkwe arudi nyuma au anaweza kukaa mlango wa katikati wasalimiane na mkwe kama kuna maongezi ni hapo hapo afu mama mkwe anarudi nyuma.

2. Mama mkwe hawezi kula na mkwe hii kwetu haiwezekaniiii

3.mama mkwe hawezi kwenda hovyo hovyo kwa binti yake labda itokee ugongwa wa mda mrefu ambao utamlazimisha kwenda kuwasalimia. Au anaumwa amelazimika kufikia kwa binti yake.

4.arabarani akikutana na mkwe wake lazima asogee pembeni mkwe wasalimiane then apite
5.kwetu mkwe ana heshima yake kama anayopewa baba na heshima hiyo upewa na wana ukoo wote so long as kaoa kwenye ukoo/ familiya hiyo.

5. Maongezi sawa wanaongea inategemea wanaongea nn ila heshima ya mkwe iko pale pale

Mashemeji zangu wote wanapata heshima hawajuti kuoa kwetu.

Mleta mada hongera sio wengine wanapinga simu binti yake apewe mimba
 
Kuna makabila mengi wazazi hawaishi nyumba moja na waume za watoto zao.... ndio maana anakuwa hivyo na anakupa pia uhuru
 
Angekuwa ni mama yangu asingekupa hata mkono kukusalimia, ni mwiko kupishana wala kukaa karibu karibu, asingekuangalia hata usoni. Kiufupi kuzoeana ni mwiko

Mama Mkwe wako ni kabila gani?
 
Kama amamemzidi maza hauzi, anza kufikiri mawazo mbadala
 
hyo ndio adabu ya kiafrica!hata mm bibi yangu alikua hakai sbulen na baba akiwpo!hasa hsa wasukuma ndo wana mila za namna hyo!mie nawaza tu nikizeeka nitaishije kwa 'sanji'wangu!teh teh!maana nitakuwa bibi wa kisasa i thnk!lol!safi sana huyo bibi!
Bibi tena?? wewe jana kwenye ile thread si ulikuwa unasema wewe ni ME?? sasa uwe bibi au babu?
 
Niuzie huyo mama mkwe mkuu[emoji16] wabebaki wachache sana wa namna hiyo

sent from my land lover 109 using Jamii forums app
 
Mkuu fanya ujenge nyumba nyingine ya kufikia mama mkwe. Kulala/kuishi paa moja na wakwe zako ni mwiko.
Wewe hujiongezi tu kwanini ukiwepo anakosa pozi? elewa fika unampa wakati mgumu sana kuendelea kuwepo hapo na nnaamini hayo matibabu hataweza kuvumilia hadi mwisho.
 
Ulivyosema ana adabu kupitiliza nilidhania huwa anakupa shikamoo huku amekupigia magoti

Hayo uliyoyaandika ni ya kawaida lazima heshima iwepo siyo mtu na mkwe wake mnachekeanachekeana tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom