Mama Mkwe Ndani ya JF

Thanda

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,915
596
Wanajamii, nawaombeni kwa heshima na taadhima:

Humu JF kuna watu wa kada tofauti tofauti, na watu wa age tofautitofauti.

Nimekuwa nikichat na watu humu JF na kama mjuavyo tena humu hatufahamiani au kama ni kufahamiana ni kwa uchache sana. Mmoja kati ya watu ninaochat nao kila siku ni mama mkwe wangu. siri hii kanipa mke wangu kwani anaijua avatar ya mama yake anayoitumia, tena si avatar tu bali na password yake.

Siku moja nikapost kitu cha kumtania (mama mkwe ni mcheshi sana) akaniuliza kwani wewe una umri gani na kwanini unitanie? Akasema mimi ni mama yako ila napenda sana JF, inaburudisha na watu wana mawazo mengi tofauti na ukikaa ndani ya box bila kuelewa mambo.

Ki ukweli hakujua kama anayechat naye ni mkwe wake, ila ni mama mzuri sana.

Ushauri wangu kwa wana JF wenzangu: Unaweza kuchat na mtu au ukamtukana matusi ya nguoni kumbe ni baba yako, mama yako, au hata mke wako bila kujua. Na ndio maana kuna mwana JF mmoja alianzisha thread ihusuyo kufahamiana nani kaoa, nani bado, nani kapigwa ban na mwenzake nk, mimi nilijibu hivi: Thanda- I am the luckiest man on earth with happy marriage. Wife alipoiona hii akaamua kunitobolea siri kuwa huwa nachat na my inlaw.

Tuwe makini sana humu wapendwa!!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
hahaha! Thanda my dear... I have a feeling una behave sababu unajua wife anakufahamu humu. lol, Alafu huyo mama mkwe huyoo.... Labda kama sijaelewa story. (I kid)
 
AshaDii, its true lakini si kubehave bcoz of my wife, nimetahadharisha tu kwani humu JF kuna mambo mengi sana.
 
Bangoo hata ukiniita jina lolote baya, elewa tu ukweli ndio huo. Unaweza nitukana halafu ukaja juta siku moja utakapojua uliyemtukana ni nani kwako.
 
Sasa naanza kufunguka akili, nilikuwa naona siku zote kuwa nachat na watu wa age yangu ya 30,s
 
tiqo, una utani mzuri sana ila ukikutana naye ana kwa ana utamwambia nini? Au tuseme ndo mnaulizana majina halafu unashuka na lako kisha unadanganya kuwa hujaoa/olewa, hapo vipi?
 
Bangoo hata ukiniita jina lolote baya, elewa tu ukweli ndio huo. Unaweza nitukana halafu ukaja juta siku moja utakapojua uliyemtukana ni nani kwako.

Kijana una behave sababu wife yupo, maana wife angekuwa hafamu ID ungerusha kavu kavu.
 
Mkuu si unajua maadili yalivyo?..halafu kama kuna ka-ukweli ndani yake....ila si kivile.
 
kweli bwana mimi mama yangu yumo halafu sijui antumia jina gani na mbaya zaidi yeye alijiunga mapema kablya yangu ila huwa najiachia wasi sina japo kiukweli sina maneno makali kivilee ila naipenda jamii forum inanibeba mno
 
Dah!Kwa sisi tulio single raha sana,tunajiachia mpakaaa . . . . . . . !!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom