Mama mkwe hataki niolewe na mwanaye kisa mimi ni Mchaga

Wewe unatafuta mke au malaika! Kama hutaki kuwa ngangari kwa mwanamke yeyote USIOE, sie tuna uzoefu
Sijaona ndoa imara ambayo watu wanakaza misuri kuishi pamoja. Ndio gani unatumia nguvu kuonyesha penzi kwa mwenzako?!

Mimi nikiwa sehemu aje mwanamke anaetaka kuwa hapo na mimi sio mwanamke nitakae mlazimisha kuwa nilipo kwa kumrubuni na pesa zangu au mali zangu ile hali yeye anajisikia kuwapo pahala kwingine....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu kipimo cha mke mzuri ambaye umeamua kumuoa licha ya wazazi kukataa ni baada au kabla ya hiyo ndoa yenu

mwanamke au mwanaume yeyote yule anayejielewa hawezi kukubali kumtenganisha na mume au mke wake na wazazi na ndugu kwa ujumla au kukubali kuona mume au mke wake anacut the ties na ndugu/wazazi wake,ukiona anaunga mkono wewe kucut the ties na wazazi/ndugu zako jua kabisa hapo umepata koroma na hata bila kuambiwa wewe jiondoe upesi

kwa hiyo huyo wa kwako ni mzuri kwa asili ndo maana amekuwa favourite ya kwenu, kwa hiyo wa kwenu walimkataa mwanzoni kwa myth tu bila kujali utu wake yeye kama yeye na yeye ndo akawaproove wrong,

sasa tulio wengi huwa tunafeli kuwaproove wrong wale waliotukataa au labda waliotukataa waliona uhalisia wetu na sisi tuliopenda tukapofushwa na mapenzi na baadae tukaanza kujutia maamuzi yetu na kuona sababu halisi za kwa nini wazazi au ndugu zetu walituonya kuhusu watu hao, na ndo hapo inabakiaga aliambiwaga lakini hakusikia
Mimi nitakupinga kidogo mkuu. Unajua sio ndugu wote wana nia nzuri kwa mwenza wako.

What if mwenzako anatokea zile familia za ndugu lawama wanaotaka kuwa sehemu ya maisha yenu na kutwaachia uhuru wa kufanya yenu?!

Mimi kwa upande wangu naamini jambo la msingi ni ninyi wahusika wawili kusimama imara pamoja bila kujali ndugu wa pande zote wanataka nini. After all, ninyi ndio mtaoishi nyumba moja, ndugu wanawasindikiza tu hadi siku ya harusi, maisha ya ndoa yakianza ndugu watajishughulisha na ninyi endapo mtakuwa na uwezo kifedha, ila kama mtakuwa makapuku hakuna ndugu atakaekuwa na time na ninyi hata kidogo.

So kwanza, ni ninyi wawili mnavyoimarika pamoja na kuwa wapenzi wa dhati halafu mengine yanafuata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hana akili tulienda hadi kwa mchungaji kumwelezea Cha kwanza akamuuliza mchumba angu ulishawahi kumpeleka kwenu akakaa na mama yako hata siku 2 tu akamwambia hapana, mchungaji mwenyewe aliishiwa pozi akasema sasa anamchukiaje mtu ambaye hajawahi hata kukaa nae Bora hata angekuwa amekaa naye tu hata siku 1 ningesema labda Kuna vitu kavisoma yani mchungaji nae haelewi maana ni vituko
Mkwe hana akili tena... Mweeh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wapendwa?

Mwenzenu na matatizo sielewi nichukue uamuzi gani naombeni mnishauri wapendwa, nilianza mahusiano na mkaka wa kimakuwa toka 2016 kiukweli ananipenda sana na Mimi nampenda na Mungu ametujalia mwaka Jana mwezi wa 12 kapeleka mahari kwetu akanivalisha na Pete ya uchumba.

Baada ya hapo wakualiana na wazazi harusi iwe mwezi wa 4 mwaka huu Ila baada ya muda mama yake akamwambia naomba harusi mfanye mwezi wa 7 nataka nijipange sherehe iwe kubwa tukamkubalia kupeleka hadi wa 7 Ila Cha kushangaza juzi kipindi wamekaa kwenye kikao Cha kuandaa kamati ya harusi mama mtu akasema harusi isogezwe tena iwe mwezi wa 10

Baada ya mwanae kumbana mama yake kuwa kwanini kila cku unapeleka mbele akamwambia sitaki uowe mwanamke wa kichaga ndomana nafanya hivi, kiukweli mwanae alichukia sana kuskia hiyo kauli akanipa mrejesho kuwa mama yake hataki anioe kisa mimi mchaga Ila kwakuwa nakupenda tumeshirikiana mambo mengi siwezi kukuacha tutafunga ndoa mwezi wa 8 bila hata ndugu zake kuwepo atasimamia shoo mwenyewe bila msaada wa ndugu zake nikamwitikia sawa

Ila hapa nawaza usikute huu uamuzi ameuchukua sababu ya hasira nahisi Kama akitulia atanibadilikia asikilize ndugu zake aniache na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nimetoka naye mbali kanipotezea muda na hivi kapeleka hadi mahari kwetu watu wanasubiri harusi.

Kama akinibadilikia sijui hii aibu tutaibebaje na familia yangu, nimechanganyikiwa mpaka nawaza sijui nimbebe tu mimba ili azidi kuwa na msimamo aogope kupoteza mke na mtoto!,

Ila nakosa jibu huyu mama simuelewi kwanini ananifanyia hivi Kama alikuwa hataki niolewe na mwanae kwanini hakumzuia kipindi anapeleka mahari wakamsapoti apeleke, kinachoniumiza ni aibu kwetu mahari imeenda alafu ikitokea tukiachana kisa mama yake aibu itakuwa kubwa Bora hata angekuwa hajapeleka mahari.

Ndugu zangu naombeni ushauri wenu nifanyaje kulishinda hili jaribu lililopo mbele yangu, Ndugu zangu Bado sijawambia Kama Kuna huu mgogoro maana hata sijui watalipokeaje nachanganyikiwa Mimi jamani
''nimetoka naye mbali kanipotezea muda'' hapo ndipo mnapokwama wewe hujampotezea muda, uzi za wachaga zilijadiliwa sana humu watu walikuwa wanabisha ona sasa ma mkwe kashtukizia
 
  • Thanks
Reactions: _ID
  1. Je utaishi na wazazi wako milele?
  2. Je wazazi wanaweza kutimiza haja zako za kimwili?
  3. Je historia ya mapenzi yenu wazazi wenu wanajua?
  4. Je wazazi wako ndo wamemchunguza mchumba wako kujua anafaa au hafai?
  5. Je zama hizi ni rahisi kupata wa kuoa au kuchezea?
  6. Akili za kuambiwa changanya na za kwako, otherwise utapelekwa na na mawimbi ya bahari
 
Kuna mambo huwa hayalazishwi. Mama na mtoto wana bound ya milele. Mchumba akitenda kinyume na matakwa ya mama ndoa yenu itakua na changamoto nyingi za upumuaji.

Ni afadhali mpate aibu ya kutolewa mahari na kutoolewa kuliko kuishi kwenye ndoa isiyo na amani. Ingekua uko kwenye ligue na mwanamke mwingine ningekishauri usife moyo lakini ligue na mzaa chema ni ngumu sana.
Ktk hili napngana na dhana ya kuwa ni must mama au mzaz anayemkataa au kumtaka kwamba umfuate anachotaka...... Nnachoamin mm tena kwa ushuhuda ni kuwa mama au mzaz ana nafasi yake ktk kushauri au au kuelekeza lakin si kuamulia hasa linapokuja maswal yahusuyo ndoa.... Pia mahusiano au lolote ligusalo hisia za moyo wa mtu si vyema mtu yoyote kumwamulia muhusika upande wa kwenda au kuwa bal kushaur tu...... Hvyo ktk hlo wahusika ktk mahusiano haya ndio wenye mandate ya kuamua hatma yao vingineo yatabak maumivu yatakayo weka knyongo na lawama nyingi sana kwa mama husika ktk thread hii....
 
Ila chagga and nyaki girls shine banaa. Wapambanaji mnoo
Usikute ndo wanachokiogopa watu.
Maana mwanamke akishaweza jisimamia anaonekana mjeuri...
And yes.. nimejifunza tumelelewa kwa upendo sana makwetu. Na wao wajifunze kulelea watoto wao wa kike kwa upendo wasisahau makwao.

Mtoto wa kike hasahau kwao asilani.
Hapa wanaume wanalalamika tu lakini wanasahau kama sisi ndo watendaji wakuu. Wakishaoaga waanajisahau na ndoa zao sisi ndo tunabaki kuwadekeza wazazi wetu
Unajua watoto wa kike muanze kujifunza kuwa serious na ndoa!

Wewe kuwa mpambanaji na kupambana kwaajiri ya familia yako vinahusiana vipi na ndoa yako na mumeo?!

Haya matabia ndio yanawafanya kuonekana tatizo. Wewe jamii zingine mbona hawasemwi. Unadhani kwamba ni kwa sababu ninyi ndio wazuri sana....?!

Mnawaharibia wadogo zenu wanaonekana nao ni tatizo kumbe ni hiki kizazi cha 1980's ndio mna mawenge ya ajabu ajabu.

Sasa unakazana kusema hapa sijui hamuachi familia zenu kwahiyo unamuona Mwenzako ni mpumbavu kuwekeza jitihada zake kujenga familia yenu ila wewe unatoa kinachotafutwa unapeleka kwa wazazi wako, kama sio kutafuta laaana za ndoa na ukoo ni nini sasa hapo?!

Endeleeni na hayo matabia...... Ipo siku. Wadada wa kimachame nao walianza hivi hivi, kidogo kidogo kutaka kujifanya wanambinu za kimafia katika kuchuma mali katika ndoa. Leo kila mtu hata jamii ya wachagga wanawaogopa.

Ukikutana na mabinti wa kimachame wa kisasa utaona shida wanayopitia. Anaweza kuwa mrembo ila kila Mwanaume inapofika swala la kuoa akisikia ni m'machame hapo hapo ndoa inapigwa stop.

Sasa hii kitu itawageukia mkiendelee na haya matabia..... Haitakuwa mchagga wa rombo, sijui marangu sijui wapi, wote mtakuwa ni tatizo na mtageuzwa tu kuwa incubator za kuzaa watoto na sex toys.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila watu jamaniyaani akajipe na kazi ya kujifunza lugha za watu kisa ndoa?
Sindo maana mtaendelea kusema tuna ego?

Acha tuonekane viburi. Hiyo ndoa ama utopolo? Ajifunze akitaka mwenyewe. English yenyewe inatushinda. Hapo ukute hata kichagga chake hakijui ndo akahangaike na lugha za watu?

Hivi haya yotemumejoweka katika nafasi kama kala zake? Mungejisikiaje?

@miss_chagga... ndoa si utumwa. Ukishaona mambo yanakuzidia kama ub quit haraka sana. Ndoa si kupelekeshana. Khaaa..... kila mtu abaki na asili yake
Ila wangekuwa na pesa na ni familia ya watu wenye pesa ungejifunza hadi mila zao...kudadadeki zako.....

Ndoa kwa mwanamke kujishusha ni must ili mume wako akutetee. Hizo ego peleka moshi mwezi wa kumi na mbili huku nje ya moshi hatutaki viburi.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua watoto wa kike muanze kujifunza kuwa serious na ndoa!

Wewe kuwa mpambanaji na kupambana kwaajiri ya familia yako vinahusiana vipi na ndoa yako na mumeo?!

Haya matabia ndio yanawafanya kuonekana tatizo. Wewe jamii zingine mbona hawasemwi. Unadhani kwamba ni kwa sababu ninyi ndio wazuri sana....?!

Mnawaharibia wadogo zenu wanaonekana nao ni tatizo kumbe ni hiki kizazi cha 1980's ndio mna mawenge ya ajabu ajabu.

Sasa unakazana kusema hapa sijui hamuachi familia zenu kwahiyo unamuona Mwenzako ni mpumbavu kuwekeza jitihada zake kujenga familia yenu ila wewe unatoa kinachotafutwa unapeleka kwa wazazi wako, kama sio kutafuta laaana za ndoa na ukoo ni nini sasa hapo?!

Endeleeni na hayo matabia...... Ipo siku. Wadada wa kimachame nao walianza hivi hivi, kidogo kidogo kutaka kujifanya wanambinu za kimafia katika kuchuma mali katika ndoa. Leo kila mtu hata jamii ya wachagga wanawaogopa.

Ukikutana na mabinti wa kimachame wa kisasa utaona shida wanayopitia. Anaweza kuwa mrembo ila kila Mwanaume inapofika swala la kuoa akisikia ni m'machame hapo hapo ndoa inapigwa stop.

Sasa hii kitu itawageukia mkiendelee na haya matabia..... Haitakuwa mchagga wa rombo, sijui marangu sijui wapi, wote mtakuwa ni tatizo na mtageuzwa tu kuwa incubator za kuzaa watoto na sex toys.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Nachochekagaa sasa.. ni vile yaan wanaume wote wanaooa mabinti wa kichagga ni matajiri na wote watafilisuwa na wanawake wa kichagga. U are very bitter bro. Punguza makasiriko. Halaf kwani lazima kuolewa ama kuoa? Inakuaje uchungu unaupata? Mtu asipoolewa anakufa? haya tuambie una billion ngapi hapo mwenzetu maana huwa wote ni matajiri na wanafilisiwa
 
Ila wangekuwa na pesa na ni familia ya watu wenye pesa ungejifunza hadi mila zao...kudadadeki zako.....

Ndoa kwa mwanamke kujishusha ni must ili mume wako akutetee. Hizo ego peleka moshi mwezi wa kumi na mbili huku nje ya moshi hatutaki viburi.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Peleka ujinga wako huko. Yaani unakaza kweli misuli. Yaan mnavyonena huku utafikiri ndo inavyoapply uraiani. Daily ndoa zinafungwa sijui wasema nini wewe. Jifunze kuwa positive. Utafikiri ulioa ukachukuliwa kila kitu

Whats even more funny ni kuwaza pesa tu.. yaani mnadhani mnanyenyekewa kisa fedha? Hamuwezi tofautisha tabia ya mtu na jamii fulani? Na majority wanaoshupazaga shingo ni makapuku wenzetu tu hela hela hela. Hizi tabia mbona ziko kwenye jamii zote hata uzunguni. Mnasahau majority ya wanaume life expectancy yenu ikoje... munabeba mengi mioyoni mwenu kwa madai ya kujikaza kiume mwisho mnakufa mapema mnaaza singizia fulani kauawa... cha ajabu kesi hatuzioni mahakamani. Mbona matukio kama haya yanatokea jamii zote na hayasemwi? You envy too much. Nawapenda sana wanwake wa kimachame. They work so hard to earn their living. Same to nyakis. Mlifikiri sisi tunataka kushinda vibarazani na khanga? Kama ndo mnachotaka kuwa offered basi nendeni sehemu husika zipo na wanajulikana maana its the only thing wanaweza kuoffer kwa wanaume. Sisi tuacheni tupambane ndo nature yetu. Inashangaza sana dunia ya leo inatamani mwanamke apambane ajikimu kiuchumi lakini kuna mwanaume anaponda eti juu ya uchapaji kazi. Very funny aisee. Au ni kwasababu hatuentertain ujinga wenu mnataka wa kuwapeleka pelek tu eh?
Ukumbuke, waza leo upo kesho haupo unaacha mama wa aina gani kukulelea wanao. Kama u need a housewife u are free. Grab one.
 
Nasikia hiyo kabila huwa inashirikiana na mumewe katika kutafuta lakini baada yakupata mafanikio, anayetangulia kufa ni mwanaume mama anabaki mjane.

Huwenda mama anapaona hapa ndomana hataki kumkosa mwanaye mapema kabla hajamalizia kumjengea kibanda chake.

Ushauri wangu sasa mjengeeni mama nyumba kwanza kisha muoane.
 
Nachochekagaa sasa.. ni vile yaan wanaume wote wanaooa mabinti wa kichagga ni matajiri na wote watafilisuwa na wanawake wa kichagga. U are very bitter bro. Punguza makasiriko. Halaf kwani lazima kuolewa ama kuoa? Inakuaje uchungu unaupata? Mtu asipoolewa anakufa? haya tuambie una billion ngapi hapo mwenzetu maana huwa wote ni matajiri na wanafilisiwa
Aaaagh unazingua. Nyie mnaleta mzaha na ndoa bana sio poa. So we unamkufuru MUNGU kwa kuishi maisha nje ya ndoa au unataka kusomekaje?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aaaagh unazingua. Nyie mnaleta mzaha na ndoa bana sio poa. So we unamkufuru MUNGU kwa kuishi maisha nje ya ndoa au unataka kusomekaje?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa kama nyie kutwa watoto wa watu wamewajaa midomoni mwenu ni lini mutaona uzuri wao?

I have always told my man... mambo ya kusema ujasiri sijui nakufa na shida zangu kiume mimi sitaki.. ndo maana dunia imeturuhusu na sisi wanawake tupambane. Hii ya 50/50 ijapokua sometimes tunazingua lakini ni kutaka na sisi tuwe kwenye fursa. Kuna leo na kesho.

Lets assume umepata ajali ukavunjika viumgo muhimu na huwezi kwenda kutafuta tena umekua mlemavu wa kudumu ama umeparalise... na mimi niwe sina ajira unadhani maisha yetu yatakuaje? Unadhani kuna ndugu watakubeba tu? Wao pia wana watoto wao. Ikatokea hayo na na nina ajira utashukuru ama utalaumu?
Ama tuseme ukawa redundunced ofisini... na maisha ndo haya... wote tuwe hatuna ajira utanidhihaki na upambanaji wangu?

Okey, Mungu tuu akakupenda... ukatangulia.. umeimagine familia yetu itakuaje? Dunia imebadilika jamani. Ndoa has a lot to offer na siyo kitamdani tu. Men love sex yes lakini maisha yetu yanatudai mengi na hatuna budi kuyatimiza kwa kusaidiana. Kwenye jamii yetu hatupendi umaskini. Ukaona yuko asiyehiweza basi either kuna mahali amekosea ama neema tu hazijamtembelea. Siko tayari kuwa housewife. Mume nitamtii ila siyo kusimangwa kisa nimetokea ukanda huo. Mbona nawajua wa makabila mbalimbali wajeuri kama nn na inaaminika wana matatizo kibao lakini wala hawatajwi. Nadhani mumewekeza katika chuki..

Jambo nililojifunza.. HUWEZI ONA ZURI LA MTU ENDAPO ULICHAGUA KUYAONA MABAYA TU. HATA ATENDE JEMA KIASI GANI UTALIONA BAYA TU. Hapa siongelei siasa lakini za hao la saba B
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom