Powel Mizengo
Senior Member
- Jan 20, 2014
- 126
- 24
Wewe mwenyewe unahitaji overhaul ya fikra zako kimapenzi. Achana na kutanguliza pesa mbele acha mtu afuate moyo wake sio pesa zako. Unapigiwa debe la mdgo mtu watu wapate pa kuendelea kuponea baada ya dada mtu kuharibu this is not love.
Tamaa zakp inabidi uzishinde maana washakujua vizuri hao na kama vipi mrudie mpz wako na umakalishe china maana yaonesha bado unampenda
Impecunious idea!No thnx!Naah don't jump the broom with the little sister. Just smash it and quit it and tell everybody that you did it.
And if the mother is easy on the eye, go right ahead and smash her too.
It's called buy one get two free. It doesn't get better than that.
Si hivyo ndugu yangu mimi nlikuwa nafanya hivyo coz nilikuwa nampenda na wala sikuwa naona kama namuhonga niliona ni wajibu wangu kumpendezesha!lakini baada ya hapo nilikoma!Wewe mwenyewe unahitaji overhaul ya fikra zako kimapenzi. Achana na kutanguliza pesa mbele acha mtu afuate moyo wake sio pesa zako. Unapigiwa debe la mdgo mtu watu wapate pa kuendelea kuponea baada ya dada mtu kuharibu this is not love.
Ni kweli unachosema lakini yeye bado hajamaliza starehe zake mara ananitumia picha yuko na jamaa yake huko Kenya mara mwingine ni Muhindi wote hao ananambia niwaite mashemeji zangu! Tena ananifanyia makusudi tu anatuma picha kila akijisikia kwenye whatsup account yangu!Huku Dar kwa mara ya kwanza nilimleta mimi lakini sasa hivi kumbi zote za starehe na kona zote za mjini anazijua!
Akili Kichwani mapenzi hayalazimishi ........Muombe Mungu akupe ubavu wako hao wa kupewa utapewa picha badala ya mke
Siwezi kubadili namba ya simu!Pole sana kaka, achana naye na ikiwezekana badili namba ya simu uwe free.
Nilikuwa na mpenzi wangu tulisoma wote chuoni na tulipendana sana kiasi kwamba nilikuwa namgaramia kwa kiasi kikubwa na kuna kipindi aliumwa akalazwa hospitalini mimi nikawa siattend vipindi kwa ajili ya kumuhudumia yeye,Zaidi nilishaenda nae kwao japo sikwenda kwa utambulisho rasmi lakini wazazi wake walielewa kuwa mimi ni mtarajiwa kwa binti yao!Wazazi wake walitokea kunipenda saana hasa mama mkwe ndiyo alikuwa ananipenda mpaka naogopa yani nikienda kwao napokelewa kama Rais vile sasa sijui ni kwa sababu nilikuwa naprovide mahela sana ila nachojua nilikuwa napendwa na hao wazazi! Tuliporejea chuoni kwa masomo mwenzangu tabia yake ikaanza kubadilika akawa anaondoka chuoni sometimes haniagi na nikimpigia simu hapokei!mi nikawa nashinda kumtafuta kila kona ya hosteli bila kupata!Nikaja kuambiwa kuwa jamaa yangu wa karibu ambaye ni mfanya biashara alikuwa akitoka naye! Mi sikuamini!Hali iliendelea hivyo mpaka mimi nikaja kuhitimu masomo yeye nikamwacha akimalizia mwaka wake wa mwisho nilipoondoka mambo kwake yakazidi kuwa balaa alikuwa anatembea na yeyote atakayemtangulizia pesa!Nilikuja kusikia kuwa ametembea na mfagia vyoo vya hosteli akampa 60elfu! Hapo mi niliamua kumpiga chini baada ya kugundua ukweli wa mambo anayoyafanya! Sasa wazazi wake bado naendelea kuwa na mahusiano nao mazuri sometimes nawatumia pesa za matumizi licha ya kwamba wanajua binti yao sipo naye ktk mahusiano ya kimapenzi zaidi ya mawasiliano na tunaitana kaka na dada! Sasa Mama yake alinipigia simu akaniuliza "endapo binti yake atakuwa amebadilika kitabia na akataka turudiane Je niko tayari?" Mi nimemjibu sipo tayari,Basi tokea hapo yule mama ananing'ang'aniza akanambia nimwoe hata mdogo wake na yule mdada niliyekuwa naye! Sasa wadau naomba ushauri nifanyaje manake napatwa na kigugumizi manake hata huyo mdogo wake ni mzuri sana wa umbo ila sijajua tabia yake!Na je ntakuwa sahihi endapo nitaoa mdogo mtu!?
Kwanza kabisa tutake radhi watu tunaofanya kazi kama hizo za kusafisha vyoo kuzibua chemba na kazi nyinginezo kama hizo ambazo nyie wasomi na watu wenye ukwasi huwa mnawadharau wanaozifanya kuwa kuna vitu hawawezi kuvipata hususani hao warembo wenu,Kwa upande wa mamkwe najua kutokana na roho yako ya kuwakarimu Ameona usikwachie huo ukarimu wako upeleke kwenye familia nyingine so ameona ni bora Akuozeshe tu mdogo wake Flani, na pia nadhani mama anataka kulipa fadhira zako kwake..Sio mbaya
Heading ilinifanya nifungue thread nisome fasta hahahahaaa kumbe inamuhusu mtoto
Upo sahihi lakini sikuwa na maana ya kuwadharau watu wa aina hiyo ila iliniuma kwa kunidharirisha mimi kwanza huyo jamaa mwenyewe ni bubu alafu wkt mi nipo chuoni alikuwa mtu wangu sana ambae namwagiza mambo yangu mengi tu! Kuhusu mamamkwe nami nilikuwa na mtazamo kama wako labda huenda anataka kulipa fadhila kwani bado mpaka sasa nawatumia pesa pindi waniombapo nami huwa sina shida nawapa! Ndiyo hapo sasa nikizingatia niliyotendwa na binti yake nashndwa kutoa maamuzi ya kuoa mdogo mtu!