Mama mkwe amekataa kuwapokea washenga wangu

Dj Composer

Member
Apr 3, 2019
24
43
Naombeni kushauriwa hapa kidogo, nilipata Binti tukaingia makubaliano ya kuoana, tukapanga mshenga wa kwenda kwao ila akapata dharura kidogo tukaahirisha. Tukaomba kwenda Jumatano ya week kesho kupeleka barua Kagera maana mama Mkwe wangu anatokea Bukoba.

Amesema kwa kumwambia binti yake kwamba hataki kuona mshenga yeyote kwake, kisa walishindwa kufika siku ya kwanza ilihali wameshajiandaa kwenda kwake Jumatano kupeleka barua.

Washenga sijawaeleza chochote kuwa Mkwe kasema hataki kuona mgeni yeyote pale. Washenga wanajua shughuli ipo kama kawaida.

Najiuliza nifanye nini asee?
 
''tukaomba kwenda jumatano ya week kesho kupeleka barua kagera''.

Mlivyoomba kwenda jumatano, mama mkwe alijibu nini?
 
We mamaa kumbena, we mama kumbe mama kumbeee mama kumbeena, tunapeta posta hata Kama ukitutosaaaa.

Kaka unawafanyia ihsani alafu wanakuletea jeuri, mwambie binti afute namba yako ya Simu, aje geto achukue vile vi holding device (chupi na sidiria) alivyoacha hapo kwako maana ushapata chuma kingine Toka Sumbawanga kinaingia soon.

Alafu uone kama Mama mkwe hajakupigia yeye simu kuomba poo.
 
Wewe umekataliwa jiongeze mkuu,umenikumbusha shangazi yangu aligomaga kuipokea barua akawaambia nendeni ntawapangia siku ya kuja nikiwa nimejiandaa kumbe hamtaki yule bwana ni fukara na kalelewa na mama babaake hajulikani
 
Wewe umekataliwa jiongeze mkuu,umenikumbusha shangazi yangu aligomaga kuipokea barua akawaambia nendeni ntawapangia siku ya kuja nikiwa nimejiandaa kumbe hamtaki yule bwana ni fukara na kalelewa na mama babaake hajulikani
Niliwahi kukataliwa siku za nyuma! Leo hii nikikutana na wale ndugu wanatamani ardhi ipasuke wajifiche
 
Back
Top Bottom