Mama Kilango v/s Sophia Simba ndani ya uchaguzi wa UWT...

JK atasema kwamba mwaka huu ni zamu ya Wazanzibari kupata u-enyekiti wa UWT.

Na huo ndiyo utakuwa mwisho wa Kilango na Simba. Ingawa mimi sio Sheikh Yahya lakini subiri mtaona!
 
Sophia Simba aliingizwa kwenye kiti hicho cha akina mama kwa pesa chafu ya MAFISADI KWAAJILI YA MASILAHI YA HAO MAFISADI.Sasa ni muda mwafaka wa kumng'oa kama creative stratergy ya kuisafisha CCM yetu toka mikono ya mafisadi. Big up Kilango, mpambanaji mashuhuri uliyetengeneza histotia hapa TZ hasa ktk kipindi nyeti cha kashfa ya RICHMOND.

MY TAKE: Kilango is the best for the good ends of CCM.
 
wote siwapendi, UWT wangebadili jina UMOJA WA WANAWAKE WA MAGAMBA UWCCM

UWT ni ile ya wakina mama Lucy Lameck, Sophia Kawawa, Bibi Titi Mohamed. UWT ilikuwa na mwelekeo, ililinda heshma ya mwanamke tofauti na sasa ambapo UWT imekuwa kijiwe cha matusi, na aibu kwa wanawake. UWT ya sasa haiwezi kusema bila kumumunya maneno kuwa imemsaidia mwanamke wa ki-tanzania. Fedheha!
 
Sophia Simba aliingizwa kwenye kiti hicho cha akina mama kwa pesa chafu ya MAFISADI KWAAJILI YA MASILAHI YA HAO MAFISADI.Sasa ni muda mwafaka wa kumng'oa kama creative stratergy ya kuisafisha CCM yetu toka mikono ya mafisadi. Big up Kilango, mpambanaji mashuhuri uliyetengeneza histotia hapa TZ hasa ktk kipindi nyeti cha kashfa ya RICHMOND.

MY TAKE: Kilango is the best for the good ends of CCM.

Mh wote ni wale wale. Sofia simba alimwambia Anne Kilango eti sio msafi wa kupinga ufisadi maana harusi yake ilifadhiliwa na hao hao anaowaita mafisadi. Kumbukeni kipindi hicho mama kilango alikuwa anavizia U first lady. CCM ni wale wale tu
 
...Kwangu mimi hii ni taarifa nzuri kusikia kuwa Mama Kilango ameanza kuonyesha nia ya kugombea uenyekiti wa UWT...hii ni habari nzuri kwasababu,Anna Kilango Malecela ni mpinzani mkubwa wa Sophia Simba..Na hii inakumbwa kwa mara ya kwanza walioneshana ubabe wakati wa kukaribia uchaguzi wa mwaka 2010 pale Sophia Simba alipowatuhumu Mzee Malecela na Mama Kilango kusaidiwa pesa toka kwa mafisadi kufanikisha ndoa yao.Na ndipo Mzee Malecela aliposema inapaswa sasa watu kupimwa akili kabla ya kugombea au kupewa uongozi.

...Kwangu mimi hii ni vita nzuri ambayo itaendelea kumong'onyoa hiki chama chetu cha majambazi.Well done Mama Kilango kwa maamuzi yako.

source:Mwananchi.

Mama kilango anachukua hiyo nafasi kwa kuwa anatakiwa na mwenyekiti katika mpango wake wa kujivua gamba kwa kukiondoa chama mikononi mwa mafisadi,Da Sophy licha ya kuwa na ujamaa na wa muda mrefu na jakaya lakini amekuwa mtiifu zaidi kwa mafisadi hasa lowassa ana rostam ambao ndio walimbeba kumshinda Janet kahama uchaguzi uliopita,nakumbuka wajumbe wa mkutano wa uchaguzi wa uwt walipewa kila mmoja shs laki tano mpaka milioni kwa wale wabishi usiku wa kuamkia uchaguzi.Jakaya hamtaki da sophia kwa kuwa natetea ufisadi ma mafisadi kwenye vikao vya chama
 
You are absolutely right.Sophia Simba yupo upande wa mafisadi ambao Jk na Nape wamewakaba shingoni ili kuisafisha CCM.Kwa mantiki hiyo Sophia Simba lazima atoke(ashindwe) katika uchaguzi huu ili asiingie CC na NEC. Huu mpango ni very professional, technical and well skilled.
Sophia mwisho wake ndo huu, hata afanye nini, she must be out, kutokana na logistics ambazo zipo dhida yake.
 
Mi nasubiria kuangalia picha hilo maana halieleweki kama ni la kiindi au la kichina
 
Kwa UWT wote hawa wawili Kilango na Simba hawafai kuiongoza. Wanafaa wakaendeleze majigambo nje ya UWT. Kazi yao kubwa ni kuonyeshana ubabe na si kuisaidia Jumuia. Inafaa wengine wajitokeze zaidi na mapema ili tuwafahamu.
 
Ni mpambano mkali kwa kweli,
Pamoja na sifa zao zote mlizotaja tutarajie mnyukano ambao utakuwa historia hapa TZ
 
Hawa wote ni bongo lala. Simba ni mipasho na kilango ni mpayukaji pasipo point.uwt ni hawa tu? Wamedumu kwenye ndoa zao?
 
wanaanza kuvaana kabla wakuwavaa hawajafika:-
mfano. Sofia v/s kilango
sita v/s naodha.
Manumba v/s mwakyembe.
Jk v/s el
mwakipesile v/s mwakyembe.
.
.
.
.
Ongeza wengne kama umeelewa !
Huo utawala umefitinika tayari hatuhitaji wala mapambano! Bwana yuko kazini na upanga!!
 
Mwenyekiti wa UWT taifa Sofia Simba, ameanza kupangua shutuma zinazoelekezwa kwake na kumkwaza kutetea nafasi yake dhidi ya Anna Kilango ambaye anadaiwa kuiwania nafasi hiyo kwa udi na uvumba.

Hoja ambazo zinatumiwa na kundi la Mama Kilango kumuangamiza Sofia simba ni pamoja na ile ya kutaka kuwepo kwa ukomo wa wabunge wa viti maalum na kuwa miaka kumi, baada ya hapo wabunge hao wakatafute majimbo na sio viti maalum tena.

Sofia simba akiwa Dodoma, amewahutubia wenyeviti wa UWT wa mikoa na wilaya zote wanaohudhuria semina elekezi na ametumia jukwaa hilo amekanusha kuwa sio yeye aliyeanzisha hoja hiyo ya ukomo wa viti maalum, lakini akasema ni vema ukawepo ukomo huo.

Amesukuma zigo hilo kwa Anna Abdala, Anna Komu na Thabita Siwale kuwa wao ndio waasisi wa hoja hiyo ya ukomo na anachokifanya yeye ni kutekeleza aliyoyakuta.

Kambi ya Mama Kilango imeibeba hoja hiyo kama fimbo dhidi ya Sofia Simba ambapo wabunge wengi wa viti maalum CCM ambao wanaonekana kutokuwa na uwezo wa kwenda kuwania ubunge majimboni wamekuwa wakipinga wazo la ukomo wa vipindi viwili, na hivyo kwenda kinyume na mwenyekiti wao.

Uchaguzi wa UWT taifa unatarajia kufanyika baadae mwaka huu ambapo kuna mchuano mkali wa chini kwa chini kati ya mwenyekiit wa sasa Sofia Simba na Mama Kilango ambaye ameanza kampeni za chini kwa chini.
 
Ni kweli hoja hiyo ilianzia kwa mama Anna Abdallah, Sophia ameikuta hiyo hoja. Lakini ni sawa, kwanini hawa wabunge wanawake wanang'ang'ania viti maalum? Kuna watu wamekalia viti maalumu kwa zaidi ya miaka 15 -20 kama vile Elizabeth Batenga, Mariam Mfaki, Maua daftari, Diana Chilolo, Zakia Meghji, Kidawa salehe na wengineo. Uzoefu walioupata unawatosha waende wakapambane majimboni, wanaogopa nini?
 
Lazima mtu atoe ulimi nje hapo... Hako kazee ka Anna Abdallah si kamekuwa kabunge ka kupewa kwa miongo kibao kanazidiwa hata na Halima Mdee ambaye amepambana kivyake...

Hoja ya msingi ni kufuta kabisa hivyo viti maalumu period!!
 
Ni kweli hoja hiyo ilianzia kwa mama Anna Abdallah, Sophia ameikuta hiyo hoja. Lakini ni sawa, kwanini hawa wabunge wanawake wanang'ang'ania viti maalum? Kuna watu wamekalia viti maalumu kwa zaidi ya miaka 15 -20 kama vile Elizabeth Batenga, Mariam Mfaki, Maua daftari, Diana Chilolo, Zakia Meghji, Kidawa salehe na wengineo. Uzoefu walioupata unawatosha waende wakapambane majimboni, wanaogopa nini?

Mkuu, nadhani Zakia Meghji sio mbunge wa viti maalu, ni mteule wa Rais kwenye nafasi zake 10 kama sijakosea. Daima huyu mama viti maalum huwa anashindwa na kuokoka katika kapu lakini kuanzia 2005 aliachana na viti maalum akabaki na jimbo lake la IKULU
 
Back
Top Bottom